Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 2,474
- 2,646
Wasalaam,
Kitendo cha tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka haraka kukemea makusudio ya vyama vya upinzani kushirikiana katika uchaguzi huu ni cha kibaguzi hakikubaliki. Sababu iliotolewa na NEC ni dhaifu na ni dhahiri ni kuitetea CCM, eti wananchi watachanganyikiwa siku ya uchaguzi na eti watashindwa wampige kura nani.
Hapa najiuliza hawa wananchi NEC inaowasemea ni mbumbumbu kiasi gani hata wasijue wamchague nani? Ina maana watanzania ni vilaza na kwamba vyama vya upinzani vikiungana tutachanganyikiwa tusijue tumchague nani!
Kuna dalili na hisia mbaya kwamba tume ya taifa ya uchaguzi IPO pale kwa maslahi ya CCM na inapokea maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa CCM ambae ndio muajiri wao, kwa kifupi watumishi wa NEC ni makada wa CCM.
Hitimisho: Kila mpenda haki na Amani ya taifa hili aikemee Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuacha uCCM ili uchaguzi uwe kwenye sanduku la kura kwa Uhuru na uwazi wenye nia ya kushirikiana waachwe washirikiane, wananchi wakichanganyiwa itakua vyema maana watampigia kura Mh. Magufuli hivyo kuwa faida kwa NEC yenyewe, CCM, TLP na UDP.
Maendeleo yana vyama.