Msulibasi
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,836
- 7,492
Natazama uchaguzi wa Tanzania 2020 naona upo baridi kupitiliza. Hakuna vuguvugu kuanzia kwenye media mpaka mitaani. Kenya uchaguzi mkuu ni 2o22 lakini mijadala imeshika kasi. Mihemko ni ya kiwango cha juu kuliko Tanzania utadhani Tanzania ndio 2022.
Hali hii si yenye afya kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi kwani uchaguzi huibua mijadala mingi miongoni mwa jamii na mawazo mbadala.
Ni wakati muafaka kwa taasisi mbalimbali kutoka hadharani kuweza kuusisimua uchaguzi wetu vinginevyo natabiri utakuwa uchaguzi wa UVCCM, BAVICHA, JUVICUF ,NGOME nk raia wasio wanachama wa vyama hawaelekei kuguswa.
Kenya mijadala ipo huru sana ,vijembe vya kisiasa, burudani vichekesho vya kisiasa na mashambulizi ya ana kwa ana ya kisiasa yametamalaki na watu wa Kenya wanaonekana kuzoea na kuchukulia positive. Kambi zinajengwa na kubomolewa kila uchao na maisha yanendelea.
Mazingira ya Kenya ya kisiasa ndio yalikuwapo Tanzania kabla ya Hapa kazi tu. Uchaguzi ulikua na sura ya elimu uchumi na burudani. Nani Katuloga?