Uchaguzi 2015; CHADEMA wajiandae kupambana na Ufisadi kura za maoni

coby

JF-Expert Member
Nov 28, 2008
342
39
Ni dhahiri kwamba idadi ndogo ya waliojitokeza kugombea ubunge na udiwani kupitia CHADEMA mwaka huu ilitokana na chama hicho kutokujulikana sana hasa vijijini na vilevile kudhaniwa kuwa hawawezi kushinda kwa hiyo watakua wamepoteza fedha na muda wao.

Kwa ushindi wa CHADEMA mwaka huu ni dhahiri kuwa idadi ya wanaotaka kuwania viti mbalimbali kupitia chama hicho itaongezeka maradufu na kufanya zoezi la uteuzi liwe gumu kama ilivyokua CCM. Ni bora CHADEMA wajipange kuhakikisha vigezo vinavyoeleweka na vilivyo dhahiri vinawekwa kuepusha ufisadi katika mchakato wa kura za maoni
 
Pili nawaomba na nitawaombea kwa Mungu walio CHADEMA sasa wasirubuniwe na mafisadi na kukisamabaratisha chama kama ilivyotokea enzi za Mrema wa nccr! Wanachadema mliochaguliwa utu wenu na wa waliowachaguo ni wa maana zaidi kuliko maslahi binafsi!
 
Back
Top Bottom