Uchaguzi 2010: Wafungwa na haki ya Kupiga Kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Wafungwa na haki ya Kupiga Kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by AljuniorTz, Sep 19, 2010.

 1. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2010
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wananchi wenzangu kuna suala nahitaji tuliangalie kwa uzito wake; je ktk uchaguzi wa mwaka huu wafungwa watapiga kura kuchagua rais, wabunge na madiwani?

  Mwanzoni mwa mwaka huu nilibahatika kutembelea gereza fulani hapa nchini; ktk mazungumzo yetu (nilikuwa na baadhi ya staff members) na mkuu wa gereza tulimuuliza suala la wafungwa na kupiga kura kuchagua viongozi wa nchi; akatujibu kuwa suala hilo lipo ktkt mchakato na kuna uwezekano mkubwa sheria ikapitishwa ili waweze kupiga kura ktk uchaguzi wa mwaka huu.

  je hii sheria ilipita? wenye habari zaidi watujuze
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kama mfungwa anaweza akapata nafasi ya kusoma hadi kutunukiwa digrii akiwa gerezani, itashindikanaje kura?
  Labda tuangalie sifa za kuwa mpiga kura kwanza...Ni kuwa raia wa Tanzania, na umefikisha umri wa miaka 18, basi una`qualify kupiga kura!
  Kama hiyo sheria bado haijapitishwa ni kuwacheleweshea haki wafungwa!
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  na watanzania ambao watakuwa safarini kikazi siku ya kupiga kura (ama nje ya majimbo yao au nje ya nchi) kuna utaratibu gani kwa watu hawa?
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sio Tanzania ya leo, labda baada ya miaka 15 ijayo. Watanzania waliopo nje ya nchi hawaruhusiwi kujiandikisha na kama hawajajiandikisha hawawezi kupiga kura. Wengi waliopo huko wanaitangaza tanzania kwa kila hali na wengine wanafanya kazi za serikali lakini hawapewi fursa hiyo.

  Ukiuliza kwa nini hawaruhusiwi hakuna jibu utakalopata zaidi ya kuambiwa kuwa mchakato unaendelea. Mchakato unaendelea Kivipi ? hakuna atakayekujibu.

  Hakuna sheria ya mfungwa kupiga kura ingawa kupiga kura ni haki ya msingi kwa kila mtu pamoja na mtu aliyekosa na au aliyetuhumiwa ( mahabusu) na bahati mbaya siku ya uchaguzi atakuwa mahabusu. Watanzania walio nje hata wanaotumikia serikali yetu hawatapiga kura. wanaosoma na walioenda kwa biashara pamoja na wagonjwa wote watakosa haki hii.

  Wanaoweza kujibu ni mwanasheria mkuu wa serikali na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kama siku ya kupiga kura hutakuwa jimboni kwako ndo haki yako ya kuchagua mbunge ipotee?

  hapa nazungumzia wale wanaoishi jimboni kikawaida lakini wakalazimika kutokuwepo jimboni siku ya kupiga kura tu.
   
 6. AljuniorTz

  AljuniorTz JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2010
  Joined: Jan 6, 2009
  Messages: 544
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunaweza kusema hizi ni mojawapo ya changamoto kwa wapinzani wanatakiwa wawepo kwa wingi bungeni ili kuwezesha kubadilisha sheria hizi za kibaguzi na zinazokinzana na sheria mama (katiba) ambayo inasema kila raia ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa...
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hawa wakiingia bungeni ni kuzungusha viti tu hata miswaada hawafuatilii. Hakuna kitu cha msingi kama haki ya kupiga kura na hakuna mbunge aliyeliona hilo na serikali wala haijali.

  Ni kosa letu, tumewachagua sisi wenyewe wala tusilalamike
   
 8. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Inayopaswa kupitisha sheria ni serikali ya chama cha Mapinduzi, sasa iwapo wananchi ambao wako nje ya gereza wamekuwa akiwapa taaabu ya kuchagua kiasi cha wao kuamua kutumia vishawishi, vitisho kwa wapiga kura leo gerezani watakwenda kuwaambia nini watu wenyewe asilimia 97 wamefungwa kwa kesi za kusinginziwa, E.g: Babau seya ahalafu kesho ukamuombe akuchague
   
Loading...