Uchaguzi 2010: TBC1 are doing good job! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: TBC1 are doing good job!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Aug 28, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Tangu kuanza kwa kampeni, Ijumaa iliyopita, ni jana, leo na kesho, ndio nimepata nafasi kutulia nyumbani kufuatilia uchaguzi kwenye Electronic Media.

  Jana nimeshuhudia TBC ikionyesha live uzinduzi wa kampeni za CUF, na leo nimeshuhudia Live ya uzinduzi wa kampeni ya Chadema.

  Nimedokezwa TBC imetenga masaa 4 kwa kila chama kutangaziwa uzinduzi wa kampeni na ufungaji wa kampeni zao.

  Pamoja na TBC kukatiza matangazo hayo na Mkurugenzi wake Tido Mhando, amelitolea ufafanuzi, wale ambao sio washabiki maandazi, tumemuelewa na tunaungana na TBC katika kuhamasisha kampeni za kistaarabu.

  Pongezi hizi nazitoa kufuatia saa hizi, nashuhudia live ya kipindi kingine kipya kiitacho Mchakato Majimboni. Hiki ni kipindi cha mdahalo live kati ya wagombea ubunge jimbo kwa jimbo wakijieleza live.

  Kitendo hiki cha TBC kuvipa nafasi sawa vyama vyote, ni jambo la kustahili pongezi.

  Kwa mfano Channel Ten kwa muda mrefu imekuwa TV huru isiyo na upendeleo. Leo kwenye news zote, uzinduzi wa kampeni za Chadema ndio umekuwa lead story, lakini kwenye news za Channel Ten, leo yao ni muendelezo wa kampeni ya CCM. Inawezekana upendeleo huu maalum, unafuatia umiliki wa Tanil na RA kwenye kituo hicho, hivyo kwa sasa TV huru ya uchaguzi, imebaki ni TBC Pekee.

  Big Up TBC!.
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Aug 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Pasco nakubaliana na wewe kwa sehemu.

  TBC sio chombo huru kwa kweli.Wamekuwa biased several times.Samahani kusema hivyo.
   
 3. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  What are you trying to say bro? Tafsiri ya kampeni za kistaarabu ni nini? Na ni nani anaweka hizo criteria? Muda mwingine tunatumia misamiati mizuri sana kujustify matendo machafu, kwa hiyo TBC ni chombo kinachocensor maneno watu watamkayo? Na hiyo inafanyika tu pale CHADEMA wanapoyatamka? Pale ambapo wapinzani wanatukanwa kwenye majukwaa ya kampeni za CCM tafsiri ya ustaarabu inabadili maana? Hizi double standards muda mwingine tujaribu kuziangalia, maana zinatupotezea credibility za uchambuzi. Sheria ziko wazi, kama kuna matusi aliyetoa anaweza kupelekwa mahakamani kuliko TBC kuanzisha mahakama yake. Hii kwa maoni yangu haistahili kutetewa, hata na ninyi washabiki wa kichapati, acha wale washabiki maandazi!!!
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kuna siku moja umma utawafuata pale walipo na kuwachoma moto
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Huna haja ya kuomba radhi sista!! Hilo linajulikana wazi hata Tido anajua hilo, halafu inafika sehemu mnaniambia kuwa wasomi sijui, waliokaa ughaibuni wanaweza kuleta mabadiliko, si huyu Tido alikuwa BBC what the hell is he doing now? si ajabu wengi wapo huko busy kuanzisha matawi ya CCM badala ya kutafuta elimu na mbinu za kuikomboa nchi kutoka kwenye lindi la umaskini wa mawazo!!
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wamenichefua sana TBC leo..yaani natamani kutapika kwa kitendo walichokifanya leo
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mpiga Filimbi nakuunga mkono kabisa. Huyu Tido nilidhani kwa kukaa ughaibuni tena kwenye nchi za kidemokrasia kwa muda mrefu angekuwa chachu ya mapinduzi, lakini badala yake analeta udikteta. Hii haiingii akilini kabisa. Tido huyu wa TBC si yule wa BBC. Kuna tofauti kubwa mno. Kama kuna unafiki basi mwogope mwanadamu anavoweza kubadilika na kuvaa mask alimradi akidhi mahitaji yake.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  Regia Mtema, asante kukubaliana na mimi kwa sehemu, hiyo tuu inanitosha, nimesema TBC is doing a good job tangu kampeni zimeanza, hivyo kama wako biased several times, hilo sio la juombea msamaha bali ni la kulisemea maana mishahara yao ni mimi na wewe, yeye na yule, wale na wao, au sisi sote ndio tunawalipa kwa kodi zetu, hivyo tuwasema mpaka wanyooke.
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2010
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Talk of possibility.

  Leo hii tu wakati TBC1 wamekatisha matangazo na habari kutufikia pale uwanjani, palitaka kuwaka moto. Lile gari lao la matangazo lingepondwa vibaya. Sikuwa mbali sana na lile gari. Ni Marando aliyetuliza munkari; na baadaye Mbowe pia.

  Mwaka huu hapatatosha.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  live ya Kipindi cha Mchakato Majimboni kinachorushwa live na TBC-1 kinaendelea, nimewasikiliza wagombea wote, kwa maoni yangu, ubunge wa Ubungo, njia ni safi na nyeupe kwa JJ Mnyika, Mama Hawa Ngumbi na CCM Kwish ney!, wamemuuliza swali provocative, na kweli akawa provoked, ala loose control na kutishia kupeleka watu mahakamani.

  CCM itakuwa na kazi kubwa ya kumsafisha huyu mama ndidi ya tuhuma alizotwikwa, na kama zina chembe ya ukweli, hilo ndilo jeneza rasmi la mgombea wa CCM.

  Pia naomba kuchukua nafasi hii kumpongeza Mtangazaji Shabani Kissu wa TBC-1.
  Tangu kile kipindi cha Kiti Moto Kilipokufa, leo ndio nimeona tena kipindi cha level ile.

  Big Up nyingine TBC-1, Big Up Shanani Kissu!.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  MpigaFilimbi, Live Broadcast is a challenge, mnapoweka rules za matusi hapana, au kampeni za kistaarabu, then rules must be followed only kwenye live broadcast.
   
 12. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #12
  Aug 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu Mama naona ana matatizo makubwa, hakupaswa kupanic namna ile wakati anajua umma unamtazama Live.

  Sielewi aliwezaje kuwashinda Nape na Mama Mangunga kwenye kura za maoni.
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Aug 28, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ndio maana leo vijana wa CHADEMA walitembeza kichapo kidogo kwa Marine kwani kodi zao zilikuwa zinawauma halafu haki ilikuwa inataka kubakwa.Kwenye taarifa ya habari ya usiku imeoshesha wazi kuwa Marine amekasirishwa sana na kitendo kile bila kujua kuwa haki haletwi kwenye sahani.
   
 14. kinya

  kinya JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2010
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 482
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  kwa mfumo wa vyombo vya habari kaz bado ngumu kuleta mabadiliko binafsi nawaamin mno MLIMAN TV ila leo wameungana na tbc kunichefua kwa kutokuonyesha taarifa kwa wakati sijui walikuwa wanasubiri go ahead baadaye wanatuzuga wanamatatizo habari baadaye japo walikuja onyesha lakin iman yangu kwao imeshapungua...! :mad2:
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  ,
  Wengi wa kinamama waliopewa UDC ni either wamebebwa, au chakula ya wakubwa, nilivyomuona huyu mama anavyojieleza, lazima ama alibebwa na CCM, alikata sana, au alifanya mambo. Kesema kweli, CCM ingempitisha Nape Ubungo, Mnyika angekuwa na kibarua kigumu, lakini kwa huyu mama, kazi mbona ni rahisi kwake, ni kama kumsukuma mlevi, halafu amejieleza ana digree nne za vyuo vukuu!.
   
 16. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Sijakuelewa unaposema "Pamoja na TBC kukatiza matangazo hayo na Mkurugenzi wake Tido Mhando, amelitolea ufafanuzi, wale ambao sio washabiki maandazi, tumemuelewa na tunaungana na TBC katika kuhamasisha kampeni za kistaarabu".

  Unaodai walimwelewa mnayafahamu makubaliano kati ya TBC na vyama vinavyofanya Kampeni ili muweze kuwa katika nafasi ya kuelewa zaidi; au ndio ule uvivu wa Kitanzania wa kufikiri ukisikia jambo unaamini.

  Professionally Tido amefanya blunder kubwa pamoja na waahariri wake kwa kurusha ufafanuzi huo bila ya kubalance hayo madai ya Tido kuwa kuna ukiukwaji wa makubaliano. Kiuandishi wanaotuhumiwa walitakiwa kupatiwa nafasi ya kujibu tuhuma hizo ili tuweze kufanya informed decision na sio kama decision zako za upande mmoja.

  In short ufafanuzui huo ilikuwa ni namna ya kujisafisha ya TBC na Tido kujisafisha kutokana na kupokea maagizo kutoka kwa viongozi wa CCM kukatisha matangazo. Nakuhakikishia wote TBC na CHADEMA wanahatajiana kwa kuwa CHADEMA hivi sasa ina wafuasi wengi wanaofuatilia matukio yake kuliko chama kingine chochote na wafanyabiashara wanaotoa matangazo yao wanalijua hilo na wanataka kutangaza na Tv inayotazamwa na watu wengi zaidi.

  Kilichofurahisha na watamnzania walipa kodi kuionyesha TBC na uongozi wake resentment ya aina yake na inayotuma ujumbe TBC. Kuwa wawe wangalifu na hujuma zao kwa CHADEMA, kwa kuwa ndio jahazi la mabadiliko linalotegemewa na watanzania wengi sana waliokwisha tambua namna ya kudia haki zao ikiwemo haki ya kupata jabari sahihi zisio za kificho.

  Ni vyema TBC wasijiingize kufanya shughuli z amahakama. Mahakama ziachiwe kuamua nani alimkashifu mwingine na sio kazi hiyo kufanywa na Tido na Marin Hassan.

   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #17
  Aug 29, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Kusema ukweli umekuwa SIO USTAARABU siku hizi?

  Kwa hiyo Tundu Lissu alipouonesha hadharani mkataba wa Bulyankhulu, akawaeleza wananchi kilichomkuta mpaka akakamatwa, akalazwa ndani Central, SHIMONI, hakuwa mstaarabu? Waliomkamata bila kosa, na kusema kwamba yeye MCHOCHEZI, huku leo JK akisema kwamba anawalipa wahanga wa Bulyankhulu fidia, yeye ndiye mstaarabu, ila aliyehoji kuhusu wahanga hao si mstaarabu, ndio unachosema?

  Ndugu, funguka macho. Ustaarabu unaoutaka wewe HAUPO. Watanzania hatuna uoga tena. Tutasema ukweli daima, hata kama ukweli huo unawahusu viongozi wa CCM.

  Simwonei aibu FISADI yeyote! Ila NAMWOGOPA MUNGU aliyeniamrisha NISITOE wala KUPOKEA rushwa!

  Endeleeni kula rushwa, lakini fainali Al-Qiyama! Leo, mtaepuka kifungo, lakini siku hiyo, mtaogelea kwenye jasho lenu!

  Ujumbe umefika!

  -> Mwana wa Haki

  P.S. Sina jazba, naongea ukweli tu. JK alihusika na mkataba wa Bulyankhulu, na mingi mingine. Hukumu yake 31 Oktoba 2010! Siku ya FURAHA KUBWA KWANGU! Tena tutamsindikiza kuondoka Ikulu kwa MATARUMBETA!
   
 18. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #18
  Aug 29, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Msema kweli mpenzi wa Mungu. Nimefurahishwa na kipindi cha Mchakato Jimboni cha mdahalo kwa wagombea wa ubunge. TBC wamejirekebisha, wameendelea vizuri. Wagombea wote wa Ubungo walipata nafasi sawa, hata yule aliyechemka - KAMA KAWAIDA YAO - wa CCM. Chama Cha Mafisadi!

  Hawa ameonesha wazi ufisadi wake. Daima, ficha upumbavu wao, onesha hekima zako!
   
 19. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Butola mama mgombea wa CCM Ubungo alipanic kwa kuwa ile stori ni ya ukweli nyumba ya UWT iliwahi9 kuuzwa wakati yupo katika uongozi wa Kinondoni. Nakumbuka kusikia madai hayo siku za nyuma, ndipo Lowassa akamnusuru kwa kumpatia UDC ili aondoke wilaya ya Kinondoni kwa muda watu wasahau. Alichopanic ni kuwa kashafa hiyo imeibuka upya tena wakati wa kampeni.

  Uwezo wa kuwashinda akina Nape aliupata baada ya kuwa na fedha za EL na RA ambao walitaka kuhakikisha mgombea wa JK yaaniMama Mwangunga apiti kabisa. kwa kuwa TAKUKURU inamilikiwa na EL hakuwa na wasi wasi wowote wa kukamatwa. Ilipoamiriwa kuwa kura zitarudiwa katika Kata ya Msumi TAKUKURU ndio wakaibuka huko ili kumzuia Mwangunga kufanya vitu vyake huku wakiwaachia watu wa mama huyu kuwahonga wajumbe wanavyotaka.
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  MWANAHAKI ina maana haukuona jinsi yule mwendeshaji wa kipindi alivyo kuwa akmitetemekea huyo mama aliyepandsha wa CCM kiasi cha waliohdhuria kuanza kumzomea ndipo akapata ujasiri wa kuchukua role ya kuongoza kipindi kwa kutoa haki saswa kwa wagombea wote?
   
Loading...