UCHAGUZI 2010: Nilipokutana na 'MALARIA SUGU' ndani ya Safari,ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU 14 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UCHAGUZI 2010: Nilipokutana na 'MALARIA SUGU' ndani ya Safari,ZIKIWA ZIMEBAKI SIKU 14

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Donyongijape, Oct 17, 2010.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Poleni na majukumu ya hapa na pale wana JF.
  Wiki hii nilikuwa katika safari za hapa na pale nchini kwetu humu kutafuta riziki.Katika moja ya safari yangu moja iliyofanyika jana jumamosi kutoka Kiteto mpaka Dodoma,nilikutana na vimbwanga vya hapa na pale,lakini kikubwa ni kukutana laivu na mtu ambaye kwa kweli nilimfananisha na 'malaria sugu' iliyopanda kichwani.

  Ni mwendo karibu wa saa 4.30 hv,ndani ya basi kubwa lililokuwa limejaza abiria kama kawaida ya mabasi mengi hasa hizi njia za vumbi ambapo magari mengi mazuri ni nadra kuyakuta yakifanya safari zake.

  Tukiwa tumefika kama robo ya safari sehemu moja inaitwa DosiDosi,aliiingia mtu mmoja mtu mzima kiasi (mwenye rika km miaka 40-45 hv) aliyekuwa katika kofia iliyokuwa imepambwa na sura ya bwana mmoja akiwa anatabasamu,si mwingine JK. Huyu bwana alikuwa muongeaji sana na kwa bahati nzuri alikutana na rafiki yake humo ndani ya gari wakaendelea kumimina stori. Mojawapo ya stori waliyoiibua ilikuwa ni kuhusu siasa za tanzania zinavyoenda.

  Hapo sasa ndipo tulipoanza kusikia vimbwanga vya malaria sugu huyu..mwanzoni alikuwa akipingana na mwenzake huyo juu ya maendeleo yaliyoletwa na bwana JK na serikali yake. Alitoa hoja nyingi kusifia JK lakini zisizo na mashiko na hata kufanya abiria wengi kuguna(kumbuka alikuwa akiongea kwa sauti kubwa kujidai kuwa ccm imefanya hiki na kile).

  Baadhi ya watu walijiunga katika mjadala huo na mimi nikiwa mmojawapo,lakini cha ajabu hakukuwa na mtu hata mmoja aliyekuwa upande wa bwana yule.Hoja motomoto zilitolewa na watu wale ambazo zilikuwa na mashiko juu ya ulinganifu kiuwezo kati ya Dr Slaa na JK(mind you,wengi wa watu hawa ni wa kiwango cha kati na chini kimapato na asilimia kubwa ni wakaazi wa vijijin) wakimweleza juu ya ulinganifu wa sera mbalimbali za vyama vyao.

  Huyu jamaa baada ya kuona anelemewa akasema HATA MSEMEJE MIMI NA JK TUU, HATA AKITAKA KUNIOA MIMI NAKUBALI,KWANI M"#%?KO SI YANGU...

  Hapa mjadala ulikolea moto mpaka akina mama waliokuwa kimya kuibuka na kuzomea,ndani ya muda mfupi tu gari zima lilikuwa likiongea na kuponda juu ya uwezo wa chama na jk na mustakabali wa nchi yetu..Niliweza kusikia watu wakisema,"huyu Kikwete atashinda kwa wizi tu,lakini mimi na ukoo wetu wote hatumpi kura japo ni CCM",wengine " hakyamungu sijawahi piga kura lakn mwaka huu napiga km kuiba waibe lakini watajua siwapend',mmoja wa akina mama wakina mama alisimama na kuhoji kwa nguvu ndani ya basi lile lefu kabisa, " hivi nani hapa asiyetaka mwanae asome bure??'", Gari zima wakajibu "Hakunaa",wengine,"akiwepo chizi au kama hana mtoto basi hana ndugu masikini,lazima huyo tajiri"

  KURA ZA MAONI:
  Uliibuka mjadala pia juu ya uhalisia wa kura za maoni za wasomi wetu.Hivyo ikabidi Malaria Sugu wetu aendeshe yeye mwenyewe kura hizo kwa mtindo wa u-spika ili kumaliza ubishi ndani ya basi letu.." Nani anamtaka JK???",..KIMYAAAAA..."Akasema Duh,nani SLAA???'' watu wakasema "woteee".. Yeye binafsi akatoa majibu " SLAA asilimia 90.9"

  Lakini cha ajabu,mpaka tunafika Malaria sugu pamoja na kupewa hoja zote nzito nzito zinazoeleweka,juu ya kuwezekana kutoa elimu bure,utajiri wa nchi yetu na kuona kwamba watu asimia kubwa katika walikuwa hawakubaliani na hoja zake pamoja na kura ya maoni aliyoiendesha yeye mwenyewe,aliendelea kubwabwaja na kutetea kubwa Akisema JAMANI UKITAKA 'MAMBO YAKO' YAKUNYOKEE KUWA CCM.

  My take:
  Mwamko ule niliouona katika Mkutano usio rasmi ndani ya basi lile,kuanzia konda,dereva abiria wote kasoro 'malaria sugu' wetu na (labda wengine walioamua kukaa kimya)..ulinipa picha kwamba watanzania wengi wamepata mwamko wa hali ya juu mwaka huu na wengi hawadanganyiki,kwani kuna baadhi walisema hata matisheti yao tunavaa lakini kura siri yangu..

  JK JIANDAE KUKABIDHI IKULU KISTAARABU NA AKINA 'MALARIA SUGU' WAJIANDAE KURUDISHA PESA ZETU LA SIVYO WAKACHEKI VIZURI PASSPORT ZAO KAMA HAZIJA-EXPIRE...!
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh mwaka huu CCM wana kazi kubwa ya kuiba maana kwa mwamko huo. Hata wakiiba 2010 je 2015 itakuwaje? Wanaandae kaburi na malaria sugu akubali kumeza dawa kwa kufuta masharti ya daktari(wananchi)
   
Loading...