Uchaguzi 2010 ni Kati ya Maskini Vs Matajiri..Watanzania Tujiandae katika hili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010 ni Kati ya Maskini Vs Matajiri..Watanzania Tujiandae katika hili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Josh Michael, Sep 1, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa watu makini sana kwa karibu sasa miaka 10 hivi imepita tumeshuhudia mabadiliko makubwa sana mwamko kutoka kwa Watanzania walio wengi katika dimbwi kubwa sana la umaskini.
  Katika hili Vyama vya siasa vilijinadi kuwa mwaka 2005 mpaka 2010 ni kwa ajili ya kufanikisha mafanikio na kuleta maisha bora. Sasa tumepotarajia kuingia kwenye uchaguzi mwaka 2010 kuna kila dalili kubwa kundi kubwa walio matajiri na wachache sana walio maskini kutaka kuchaguliwa kuingia kwenye Bunge Letu la Tanzania.
  Sasa kama wewe ni Mtanzania makini na aliye tayari kusimama imara daima atasimama Imara sana katika kutambua hata kutetea hali kama hii isiendelee hata kuzuia namna yoyote ile ya matajiri kuzidi kuingia kwenye chombo cha kutunga sheria za Nchi.

  Kuna kila dalili kwamba uchaguzi wa mwaka utakuwa kati ya Maskini na Matajiri walio wachache sana. Sasa ni Kazi kwetu kuchagua vyama makini na wenye moyo wa dhati katika kutetea maslahi ya taifa hili na wazazi wetu na watoto walio wengi katika dimbwi la umaskini wa kupindukia.. Tunahitaji watu mwenye moyo wa dhati katika Taifa letu,
  Tunahitaji watu walio wazalendo mwenye moyo wa dhati na mwenye kupenda kusimamia ukweli. Watu hawa wapo katika kizazi hiki chetu maskini kabisa. Na hata katika kuleta usawa katika jamii yetu. Vyama vyote vya siasa kuna watu walio tayari kusema ukweli. na Pia sasa umefika mahali kuunga mkono chama cha siasa makini katika Taifa letu Tanzania.
  Twendeni na ajenda moja tu nayo ni wakati wa matajiri hawa kutowachagua mwakani.
  Napenda kuwasilisha hoja
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kutakuwa na makundi mawili tu ni kati ya maskini na matajiri
   
Loading...