Elections 2010 Uchaguzi 2010: Majimbo 50 yenye utata

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
UCHAGUZI 2010:

:: Ni Chadema v/s CCM Tanzania Bara
:: CCM v/s CUF Tanzania Visiwani
:: Majimbo 50 tata haya hapa

Na Waandishi Wetu

UKIWA umebakia mwaka mmoja ili kufikia uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 tayari kuna kila hatua za kuanza kwa mapambano kati ya wagombea ndani ya vyama wanaotaka kubakiza majimbo yao huku wengine wakiyakodolea macho, Rai limebaini.

Utafiti uliofanywa na gazeti hili kwa kitambo sasa unaonyesha kuwa yapo matukio yanayoyafanya baadhi ya majimbo na wabunge wake kutazamwa sana na Watanzania kama watafanikiwa kubakiza nafasi zao ama kuzipoteza.

Sababu zinazoelezwa na wananchi wengi ni zile za; kuwepo baadhi ya wabunge wanaoonekana kuwa maarufu zaidi kitaifa huku wakiwa na mazingira tata katika majimbo yao kufuatia kutofanikisha maendeleo; tena kukiwa na kundi la wabunge wanaotuhumiwa sana na vyombo vya habari, huku wakiwa na sifa za kuwapa wananchi wao maendeleo.

Sifa nyingine zinazoelezwa ni zile za kuwepo baadhi ya wabunge waliomo katika upinzani wa jadi na waliowadodosha katika uchaguzi uliopita; pia wakiwepo wale wanaotoka katika majimbo ambayo upinzani umeanza kuota mizizi. Majimbo haya ni yale yaliyopo mijini na yaliyopo kwenye maeneo yenye rasilimali ambazo nyingi zinamilikiwa na wageni hasa kwenye migodi ya madini.

Upo pia upinzani ndani ya vyama na chama kitakachoathiriwa na hali hii ni CCM ambacho kina makada wanaopaniana, huku kila kada akitokea katika kundi lake. CCM kwa sasa ina makundi mengi kulinganishwa na wakati wowote tangu kuanzishwa kwake. Makundi haya yamepanga safu za Viongozi katika matawi na mashina hasa baada ya kusikika kuwa, chama hicho kitatumia wanachama wote katika kura za maoni zitakazochuja wagombea.

Mtindo huu mpya unaelezwa kuanzishwa ili kupambana na vitendo vya rushwa na ununuzi wa kura, lakini baadhi ya makada wa chama hicho wanaeleza kuwa, huu si mwisho wa rushwa bali mwanzo mpya kwa kuwa kama mgombea aliweza kutoa sh100.000/= kwa wajumbe 800 waliokuwa wakipiga kura hapo awali, sasa itakuwa kuzigawanya fedha hizo na kuzifikisha kwa wanachama kwa kutazama idadi itakayomuwezesha mgombea kushinda.

Lakini hata hivyo macho na masikio ya wengi yanawatazama wabunge wafuatao na majimbo yao katika mabano. Hawa ni; Said Arfi (Mpanda Kati), Samuel Chitalilo (Buchosa), Stephen Galinoma (Kalenga), Balozi Khamis Kagasheki (Bukoba Mjini), Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini), Charles Kajege (Mwibara), Eustace Katagira (Kyerwa), Charles Keenja (Ubungo), Estherina Kilasi (Mbarali), Aloyce Kimaro (Vunjo), John Komba (Mbinga Magharibi), James Lembeni (Kahama), Anne Kilango (Same Mashariki), John Malecela (Mtera) na Ramadhani Maneno (Chalinze).

Mengine ni; Vedastusi Manyinyi (Musoma Mjini), Nimrod Mkono (Musoma Vijijini), Profesa Philemon Sarungi (Rorya), Wilson Masilingi (Muleba Kusini), Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini), Mwinchoum Msomi (Kigamboni), Benson Mpesya (Mbeya Mjini), (Mbeya Vijijini) lipo wazi, Suleiman Saddiq (Mvomero), Lucas Selelii (Nzega), Christopher Ole-Sendeka (Simanjiro), Peter Serukamba (Kigoma Mjini), Kabwe Zitto (Kigoma Kaskazini), Philemon Ndesamburo (Moshi Mjini), Basil Mramba (Rombo), Edward Lowassa (Monduli), Dk Harrison Mwakyembe (Kwela), Samuel Sitta (Urambo Mashariki) na Rostam Aziz (Igunga).

Pia orodha hiyo ina majimbo ya; Dk Wilbrod Slaa (Karatu), Dk Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini), Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini), Hawa Ghasia (Mtwara Vijijini), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), John Cheyo (Bariadi Mashariki), Rita Mlaki (Kawe), Hamad Rashid Mohamed (Wawi), Lawrence Masha (Nyamagana), (Biharamulo Magharibi) lipo wazi, Fuya Kimbita (Hai), Prof David Mwakyusa (Rungwe Magharibi) na Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki).

Katika makundi ya wabunge hawa waliopo, lipo kundi linalojumuisha wabunge ambao wamekuwa wakizungumzwa kwa taswira hasi na vyombo vya habari lakini bado wana nguvu kubwa katika majimbo yao.

Hawa wana nafasi kubwa ya kushinda na kurejea katika nafasi hizo kwa kuwa wana rekodi ya kusimamkia shughuli za maendeleo majimboni mwao. Katika orodha hii kuna majina kama; Edward Lowassa, Rostam Aziz, Basil Mramba, Nimrod Mkono, Vedastus Matayo, Andrew Chenge na Nazir Karamagi. Katika orodha hii pia wamo wabunge wa upinzani ambao majimboni kwao wana nguvu kw akuwa wametekeleza majukumu yao ambao ni Dk Wilbrod Slaa na Philemon Ndesamburo.

Hata hivyo kwa upande wa Slaa kuna tetesi kuwa hatawania nafasi hiyo kwa kuwa upo mkakati wa kumfanya kuwa mgombea urais kupitia upinzani kwa mwaka 2010. Mwingine anayeweza kuungana na Slaa katika misheni hii ni Mbunge wa Wawi Hamad Rashid.

Kundi lingine ni lile linalohusisha wabunge ambao wameonekana kuwa machachari katika kuibua hoja mbalimbali bungeni. Hapa kuna Zitto Kabwe anayesifiwa kuibua masuala mbalimbali ya Kitaifa huku akiwa na kazi ngumu jimboni kwa kuwa hajafanikiwa kukidhi ahadi alizotoa, pia yupo Anne Kilango atakayekuwa anakwana tena na Kuga Mziray ambaye mara kadhaa amelalamikia kuibiwa kura, Dk Harison Mwakyembe ambaye siku za hivi karibuni kabuni mtindo wa kulala vijijini, kwa kisa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile amekuwa akiliwinda jimbo lake.

Tena yupo Lucas Selelii ambaye kigezo cha elimu na kusambaratika kwa Mtandao wake kinaweza kumfanya mpinzani wake mwaka 2005 Hussein Bashe kumdondosha, Christopher Ole Sendeka pia anaweza kuwa akikwaana na Mwenyekiti mpya wa UVCCM mkoa wa Arusha James Milya.

Orodha hii pia inao wabunge kama Said Arfi ambaye jimbo lake linatazamwa kama lulu na CCM, huku jimbo la Kahama likiwakutanisha wapinzani wawili ndani ya CCM, James Lembeli ambaye anaweza kuwa na kibarua kizito dhidi ya Mgombea yoyote atakae ungwa mkono na hasimu wake Mkubwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga.

Jimbo la Nyamagana linaweza kuleta mtafaruku katika CCM ambapo Lawrance Masha ameshaanza kutangaziwa upinzani ndani ya CCM, jimbo la Kawe likitazamwa kwa macho ya umakini na Halima Mdee wa Chadema. Pia jimbo la Ubungo lililo chini ya Charles Keenja licha ya taarifa ya yeye kuliwania, lipo kundi linalotaka kumshawishi kada machachari wa CCM Nape Nnauye kuwania ili iwe rahisi kwa CCM kukwaruzana na John Mnyika wa Chadema. Katika jimbo la Mvomero, Mweka Hazina wa CCM Amos Makalla ameonekana kupiga jaramba kwa kipindi sasa hali inayoashiria ugumu kwa mbunge wa sasa Sadick Murad hasa baada ya Amos kuonekana kama Kijana Msafi Ndani ya CCM na Kupewa Madaraka Makubwa.

Katika jimbo la Songea Mjini kuna hali ngumu kwa mbunge wa sasa Dk Emmanuel Nchimbi hata baada ya kuliletea maendeleo makubwa jimbo hilo, huku pia la Muleba Kusini kukiwa na hati hati ya mbunge wa sasa Wilson Masilingi kukwaana na Kamanda wa zamani wa Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam Alfred Tibaigana.

Jimboni Mwibara hali ya hewa bado ni nzuri kwa kada wa TLP Mutamwega Mugaywa, huku jimbo la Mufindi Kaskazini, mkongwe wa siasa tangu awamu ya kwanza Joseph Mungai ambaye anaonekana kutokata tama ya kuwnaia tena kiti hiho, akiwa katika ushindani mzito dhidi ya Mahamoud Mgimwa.

Uchaguzi wa 2010 Ndani ya CCM unaonekana utaendelea kuwa mgumu hasa kutokana na mabadiliko ya siasa za nchi hii na wananchi wengi kuanza kufatilia taarifa nyingi kupitia vyombo vya habari. Mbali na hilo, mtikisiko ulioikumba nchi hasa tuhuma za ufisadi na uchaguzi wa Tarime, umekifanya chama cha Chadema kuwa maarufu hasa katika kundi la vijana ambalo safari hii limeonekana kujiandikisha kwa wingi katika maboresho ya Daftari la wapiga kura.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kuwa, Chadema imekuwa maarufu kwa vijana wa umri wa miaka 18 mpaka 40, na hasa kundi la wasomi. Mbali ya hilo, sekendari za kata na kuwepo kwa TV katika Vijiji imekuwa Nyenzo kubwa ilo kifanya Chama hicho kuwa maarufu Tanzania Bara na Vijana wengi kumfanya Zitto Kabwe kama mfano wa kuigwa.

Chanzo: RAI
 
aisee! ni kule kwa Mdhihirimdhiri? Makweta? Ndesamburo? Anne Makinda? huu utafiti upo shallow!
 
Warombo wako 'busy' na biashara zao na maduka.

Sijui kama kuna kijana (30 - 40) anayejulikana atakayeweza kumtoa Mramba....Mramba bado labda bado ni ana umaarufu?

Hakuna tetesi za kuwa ni nani atakayekuwa mpinzani wa Mramba?
 
mimi na Mkono tu huko musoma vijijini.Yaani huyu jamaa yeye anasaidia huko juu kwao tu.Sasa kipindi hiki ngoja.Watu wa Majita A na B wamemchoka MNO
 
... Dk Harrison Mwakyembe (Kwela), ...

Masahihisho
Dr. Mwakyembe yupo Kyela sio Kwela. Huko Kwela yupo Dr mwingine, Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, ambaye kwa maoni yangu, alitakiwa kuwemo kwenye list hiyo kwani hata 2005 watu walipigwa butwaa kusikia amemshinda Didas Mfupe wa NCCR-Mageuzi !
 
mimi na Mkono tu huko musoma vijijini.Yaani huyu jamaa yeye anasaidia huko juu kwao tu.Sasa kipindi hiki ngoja.Watu wa Majita A na B wamemchoka MNO

Divide and Rule?
Unaota?

A ndio nani na B ndio nani?

Afadhali sisi wa Pwani!
 
... Said Arfi (Mpanda Kati), ...

Hapa kweli, CHADEMA inabidi wawe makini wasije kupoteza jimbo hilo, maana influence ya uwaziri Mkuu wa Pinda (Mpanda Mashariki) inaweza kuvuka mipaka ya jimbo na kumuangusha Arfi.
Kwa maoni yangu Said Arfi achiwe muda zaidi kulitumikia jimbo kuliko chama kazi za (CHADEMA), maana nimeona muda mwingi amekuwa kwenye kampeni za Tarime na Mbeya Vijijini kabla hawajazuiwa, pamoja na Opereshini Sangara.
 
Warombo wako 'busy' na biashara zao na maduka.

Sijui kama kuna kijana (30 - 40) anayejulikana atakayeweza kumtoa Mramba....Mramba bado labda bado ni ana umaarufu?

Hakuna tetesi za kuwa ni nani atakayekuwa mpinzani wa Mramba?

Mkuu,


Mimi nitapambana nae ingawa kwa hicho kigezo chako cha miaka30-40 sija-fit hapo,niko below 30 mkuu.Suala ni hoja na jinsi utakavyoweza kuwa shawishi wapiga kura na kama una uwezo wa kuwawakilisha wananchi wako.Infact ni beyond kujulikana mkuu
 
aisee! ni kule kwa Mdhihirimdhiri? Makweta? Ndesamburo? Anne Makinda? huu utafiti upo shallow!

Gazeti lenyewe la mafisadi unadhani wataandika nini zaidi ya kujifagilia wanamtandao maslahi wachukue majimbo 2010?
 
Habari hiyo ya Rai imeandikwa kwakuwapaka mafuta mafisadi.JK alishasema watu watenganishe biashara na siasa.Sijaona wapi Rai imemtaja Mohamed Dewji na wengine wengi wafanyabiashara kama watagombea au la.
Musoma Mjini ndugu Vedastus Mathayo lazima ango'ke hatuwezi kukubali kutawaliwa na kihiyo wa darasa la saba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom