Uchaguzi 2010: Jaji Lewis Makame - Samwel Kivuitu wa Bongo ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Jaji Lewis Makame - Samwel Kivuitu wa Bongo ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mag3, Jun 30, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Waziri awatahadharisha wapiga kura wa Busanda kuwa wasipomchagua mgombea wa CCM watabambikiwa kodi na kunyang'anywa leseni -
  Makame kimya !

  Katibu Mkuu wa CCM amtisha msimamizi wa uchaguzi Biharamulo kuwa akithubutu kutangaza CCM kushindwa ajue hana kazi -
  Makame kimya !
  Viongozi wa CCM wanakamatwa na raia wema wakinunua shahada za uchaguzi na kufikishwa kwenye vyombo vya dola -
  Makame kimya !

  Hii mifano mitatu tu inatoa ishara ya hali ya hatari inayotunyemelea kuelekea kwenye uchaguzi mkuu 2010. Inatisha haya mambo yanapofanyika wazi wazi bila kukemewa na mamlaka husika wala hatua madhubuti kuchukuliwa. Sheria za uchaguzi zinavunjwa lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame ameamua kwa makusudi mazima kufumbia macho vitendo hivyo.
  Jaji, sisi wapenda amani tukueleweje ?
  Unataka kutupeleka pabaya ili iweje ?
  Yakitokea japo machafuko utasemaje ?
  Ya Kivuitu Kenya tupishie mbali ewe Jaji
  Tuwe na amani Tarime, Mbeya hadi Ujiji
  Tuishi bila hofu Rukwa, Geita hadi Rufiji.
   
 2. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  jaji kachaguliwa na ccm kwa ajili ya kuitumikia ccm .....nyie mnategemea aseme nini?
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Mag3 na Gaijin,

  Mko sahihi kabisa! Jaji Lewis Makame ni:

  (1) Mtu wa CCM.
  (2) Kapewa kazi na Mwenyekiti wa CCM
  (3) Mwenyekiti wa CCM anaweza kumwachisha kazi siku
  yoyote atakayo
  (4) Mtu wa kawaida; sio jasiri.

  Katiba ina dosari kwani inaruhusu msimamizi wa mashindano ya kura achaguliwe na mmoja kati ya wanaoshindana!

  Aliyofanya Makamba ndio kawaida ya matendo ya viongoozi wa CCM. Wakati wa kesi dhidi ya ushindi wa Dr.Slaa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ulitolewa ushahidi wa wazi kwamba CCM ilipita huku na huko ikiwashinikiza wasimamizi wa uchaguzi watangaze matokeo ya uongo.

  Swali la msingi ni hili: CCM wanapenda amani? Nasikitika kusema jibu ni hapana, kwani viongozi wa CCM wameshawahi kusema wazi chama chao kisiposhinda hakutakuwa na amani. Yaani amani ipo as long as tunakubali kutawaliwa na CCM. Siku tukikataa basi tujue ndio mwisho wa amani.
   
  Last edited: Jun 30, 2009
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi niishasema kuwa kuna Sheria na Vyombo vya CCM, hivyo havipo huru kabisa na pia ndio maana kuna wanaJF humo hawaoni mambo kama haya
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Jibu ni tume huru tuu hatutaki kuona ya kenya,zimbabwe na Iran hapa Mungu tuepushie Janga
   
 6. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hafai ni kibaraka na si jasiri
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni KATIBA yetu inayompa mamlaka Rais kuteua Tume ya Uchaguzi. Tunaifanyaje KATIBA hii? Wanaonufaika nayo ndio wenye BUNGE, SERIKALI.
   
 8. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wapinzani wadau katiba Huru na Tume Huru ya uchaguzi na sio kama hivi tulivyo leo
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nasema hivi, kwa kuwa hatuna uwezo wa kuwatoa tuanze kuwapigia watu kama hawa kelele bila kuchoka. Tuwanyoshee vidole na tuwaonye kuwa tutawalaumu kwa lolote baya litakalotokea. Jaji Lewis Makame aliapa kuwa atatekeleza wajibu wake kulingana na katiba ya nchi na si katiba ya CCM. Sasa kama anakubali kuyumbishwa na kushindwa kusimamia haki na sheria, ni mapungufu yake binafsi kama Lewis Makame. Itakuwa unafiki mkubwa kwake kujitetea kuwa anashinikizwa na huku katiba inamlinda.

  Tusinyamaze na tuwapigie kelele watu hawa- hiyo nayo ni haki yetu kikatiba. Pamoja naye kwenye hili wako IG, AG, JM na wengineo wanaotakiwa kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa haki na bila upendeleo wowote. Kunyamaza kwetu kunawapa nguvu na kiburi cha kufumbia macho matendo ya uvunjifu wa sheria - hili halikubaliki hata kidogo. Wanawaruhusu watawala kuwatumia kwa sababu ya woga wao na mapungufu yao na si vinginevyo lasivyo wangepata ujasiri angalau wa kujiuzulu nafasi zao.
  Kwako Mh. Jaji natuma ombi hivi leo
  Kama huwezi kutimiza wajibu wako
  Kwa haki bila uonevu wala upendeleo
  Heri ung'atuke kabla uchaguzi ujao.
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ameonekana mara nyingi sana katika chaguzi nyingi sana sana, maana kuna watu wananunua shahada na hakuna alichukuliwa sheria mpaka leo
   
 11. K

  Kitoto Akisa Member

  #11
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii sio huku bara tu hata kule zanzibar mwenyekiti wa tume ni kibaraka wa CCM, lakini mimi naamini uwezo wa kubadili katiba uko mikononi mwetu sisi wananchi, kuna mbunge mmoja simkumbuki jina ila nakumbuka ushauri wake aliutoa nafikiri ilikuwa ni katika gazeti la Mwanahalisi la wiki iliyopita nanukuu alisema" wananchi ndio wenye jukumu la kudai mabadiliko ya katiba, wakisuburi hadi serikali ilete muswada wa mabadiliko ya katiba watasubiri sana, maana katiba iliyopo inainufaisha serikali. Kwa hiyo nawashauri wananchi na wasomi mbalimbali wakusanye maoni yao, na saini zao, kisha wampe mbunge yeyote awasilishe bungeni kama hoja binafsi, nawahakikishia spika hatakuwa najinsi atakubali tu hoja ijadiliwe" mwisho wa kunukuu, na kwa msisitizo tu huyu alikuwa mbunge kutoka CCM!
   
 12. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee apumzishwe tu kwani "hekima" zake zimetosha kwa sasa.
   
Loading...