Uchaguzi 2010: Inakuaje wagombea urais CCM & CHADEMA wafunguliwa kesi mahakamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: Inakuaje wagombea urais CCM & CHADEMA wafunguliwa kesi mahakamani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 6, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
  [FONT=&quot]Mwaka huu duh! Kuna kazi kweli kweli. Wagombea urais wawili wakuu wanaochuana vikali katika kampeni – yaani JK wa CCM na Dr Slaa wa Chadema wote wawili wamejikuta wanafunguliwa kesi za madai mahakamani. JK anashitakiwa na Mwalimu mmoja ambaye anapinga uteuzi wake kwa sababu hana sifa za kuwa rais!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Na huyu wa pili, Dr Slaa naye amefunguliwa kesi na mtu mmoja ambaye anadai amemchukulia mke wake!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Inakaa vipi hii – kwani haijapata kutokea huko nyuma hata siku moja.[/FONT]
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Ni ishara kwamba tunakoelekea siko. Nawaonea wivu Wakenya -- viongozi wao wameona zaidi ya urefu wa pua zao na wamekuja na katiba mpya ya ukombozi a real masterpiece. Hapa bado ni ufirauni tu kila kukicha. Watu kama akina Makamba kweli wana mawazo kama ya hao wa Kenya? Kazi yake kubwa ni kupika uchawi, hajui hata maana ya kuchaguliwa kwa kura!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Loh! Hii ya huyo mwalimu mbona imekaa hivyo -- ati Muungwana hafai kuwa Rais! Nimesoma humu JF habari hiyo, na ilishangaza yule Jaji (wa CCM) alipoonyesha tangu mwanzo ataamua vipi kesi hiyo ili kuridhisha mabwana zake! Kabla hajasikiliza ushahidi, akaanza kuhoji kwa kusema "Eti JK hafai?"
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yanakuja yale yale ya Tendwa!!!
   
 5. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #5
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kwa upande wa huyo mwalimu, kesi ni ya msingi, lakini itatupiliwa mbali.

  Kwa upande wa Dk. Slaa, hii ndiyo tathmini yangu.


  1. Kabla ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari, unaanza mahakamani na kufungua kesi, kwa taratibu zote, kisha ndio unaenda kusema nimefungua kesi kwa sababu hii na hii. Unapoanzia kwenye media, unakuwa umevunja sheria na taratibu za mahakama, kwani unakuwa umeingilia uhuru wa mahakama kutoa uamuzi ulio huru na wa haki. Huwezi kupeleka malalamiko yako kwa media, kisha public waanze kujadili, na wakifikia uamuzi ambao utakuwa tofauti na ule wa mahakama, utakuwa umeingilia uhuru wa mahakama. Kwa mtaji huu, kesi inapaswa kutupiliwa mbali, lakini itapokelewa, kwa kuwa inamhusu Dk. Slaa.
  2. Kesi imefunguliwa Mahakama Kuu dhidi ya Dk. Slaa. Kwa kawaida, kwa mujibu wa sheria, kesi kama hii huanzia Mahakama ya Mkoa (ambayo ni Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kisutu). Kuipeleka kesi Mahakama Kuu kunaifanya iwe na uzito wa juu kuliko inavyostahili.
  3. Mahimbo anadai alipwe fidia ya Shilingi Bilioni Moja, kwa "kuvunjiwa" ndoa yake. Fidia kama hii haiwezi kuwa na mantiki, kwa kuwa, si "tort". Siwezi kuelezea kinagaubaga nini haswa maana ya "tort", lakini, kwa upande wa ndoa kuvunjika, si sawa na mtu kutendewa kinyume na haki. Kwanza, Dk. Slaa HAKUINGILIA ndoa ya Mahimbo, kwani alipokutana na Josephine, tayari Josephine alikuwa AMEONDOKA kwa mumewe huyo, kwa hiyo, hata kama hakukuwa na talaka mahakamani, ndoa ilikuwa imevunjika, na si Slaa aliyeivunja.
  4. Kwa kuwa kesi hii imepewa umuhimu mkubwa, ni wazi kwamba hizi ni hujuma za CCM dhidi yake Dk. Slaa. Wanachofanya hapa ni kuvuruga mambo kwa kuweka mambo ambayo YATAJARIBU KUPOTEZA DIRA. Lakini wananchi na CHADEMA wameshtukia hii toka zamani, wamejiandaa. CCM inatapatapa. Kwa mtaji huu, haifiki mbali kwenye malengo yake. Wanapoteza pesa zao bure.
  Watu wengi wanamshangaa JK. Badala ya kuwaachia Watanzania wafanye maamuzi yao, yeye yuko busy kumfanyia hujuma Slaa!

  Ama kweli aliyefilisika hoja atavamia hoja yoyote ile!

  -> Mwana wa Haki
   
 6. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  N hivi ndivyo ilivyo, debe tupu haliachi kutiika, kibaya hakiachi kujitembeza, huna hoja, bora upayuke! Hii ndio desturi ya mshndwa!
   
 7. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #7
  Sep 6, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Mnaogopa, eee? Na bado! Hahahaha! Wadanganyika si wadanganyika tena! Hahahaha!
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Achana nao hao wanaojibu bila ya hoja. Mgombea urais kufunguliwa kesi ya kusema hana sifa za kuwa urais haijapata kutokea katika dunia hii! Mwenye data za kupinga nilalolisema?
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Huyu mahimbo ndio bure kabisa mke hakutaki unalazimisha nini?si utafute mke mwingine au.?maharinyenyewe ukiukizwa ukikipa mbuzi wawiki wa vingungutinhata elfu 60 hawafiki halafu unataka billion moja.....
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Na hakuna kitu kibaya kinachoweza kutokea kwa mwanaume kama vile kukataliwa na mke. Hapo unaweza kuhisi mengi tu.... Aibu!
   
 11. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #11
  Sep 7, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  kuachwa inaumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...