Uchaguzi 2010: CHADEMA jifunzeni siasa za kisasa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uchaguzi 2010: CHADEMA jifunzeni siasa za kisasa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by W. J. Malecela, Nov 13, 2010.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Well, uchaguzi uliomalizika umetoa mafundisho mengi sana kwa maoni yangu mojawapo ni kwamba wanawake ni lazima wapewe nafasi katika vyama vyetu vya siasa, sio siri kwamba wanawake wengi wameipigia kura CCM zaidi,

  - Sasa Chadema wajifunze kuwapa nafasi za juu kina mama katika uongozi wa taifa wa chama na pia wa-soften kidogo the image ya viongozi wanaume wanaonekana wana hasira sana, inawatisha sana kina mama ni ushauri wangu wa bure tu!

  Thaanks!  Mukulu William.
   
 2. K

  Katebe Member

  #2
  Nov 13, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesikika kwa waJF
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280


  Huna pointi kwa sababu una-generalize.

  Na zaidi ni kuwa wewe ndiyo unawatisha wanawake na maneno yako, na siyo Chadema.

  Wanawake wote mpuuzeni huyu jamaa na mawazo yake ya hovyo.
   
 4. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  maneno yako mazuri sana mkuu.. lakini huyu spika mpya .. kuna habari kwamba amesikika akisema hatambui kama kuna kitu kinaitwa UFISADI, fisadi anye mjuwa yeye ni yule mtu mwenye kuckuwa waume za watu .. sasa hapo sijui tumueleweje au ni dongo alilielekeza kwa mtu fulani.
  Amekidhalilisha sana chama changu. na amewatia aibu wanawake wote ndani ya tzn
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  William good observations Sir;

  Mkuu unaweza kudhibitisha haya kabla hatujaendelea na tafakari yako:

  1. ...Wanaonekana wana hasira

  2. ...Wakina Mama Wametishika sana..
   
 6. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Wewe machela,
  1. Umefanya utafiti au mkeo/mpenzio ndio kakueleza anavyojisika yeye
  2. inaonekana mkeo/hawalayako andanganyika kwa kofia na kanga kisha kuacha mafisadi wanavuna mabilioni ya pesa.
  3. inaonekana mkeo/changudoa wako anaipenda sana sura ya chekibobu jk.

  Nakushauri uwe makini sana na hao wenzi wako, ushauri wa bure
   
 7. October

  October JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Unawezaje kujua mtizamo wa wanawake na wakati jina lako linaashiria wewe ni mwanaume?
   
 8. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kaka inaelekea chadema wakupa homa ya ajabu eeee.......Chadema inawaheshimu sana wanawake na tunao wengi tu kwenye uongozi wa chama, au mpaka umwone mwanamke mwenyeti au katibu ndio ujue kwamba chadema inawapa nafasi wanawake?
   
 9. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mkuu mimi siungani sana na wewe kwa maneno yako machache ya wanawake wapewe nafasi. kama wanawake wangeegemea point yako basi kila jimbo alipogombea ubunge mwanamama basi ushindi ulikuwa dhahiri maana wao ndiyo wengi. But sikushangai kwa sababu hizo ndo propoganda na magharibi unakoishi.
  CCM unayoizungumzia katika top Leadership ya Chama hakuna mwanamke hata mmoja. Washauri waanze wampe mwanamke uenyekiti wa chama kabla hujazungumzia vyama vingine
   
 10. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mi i si mwanacadema lakini hivi ccm ina wanawake wangapi katika uongozi wa juu? nafikiri all parties in tz are facing the same fate in this case. sababu za wanawake kupigia kura ccm ziko obvious. refer case ya wagombea wanwake watupu kwa nafasi ya spika.

  kuwa na uke ni dili kubwa sana ndani ya ccm
   
 11. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  No comment until mtoa mada arudi kwanza kujibu maswali ya wadau hapo juu.
   
 12. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  JWTZ ndo iliwatisha raia na lile tamko lao ofcourse na pamba za FFU siku ya uchaguzi
   
 13. Ikimita

  Ikimita JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 302
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu nadhani wazo lako ni zuri sana.

  Lakini sio Chadema tu na CCM pia. CCM na Chadema so far wako sawa tu kwa upande wa chama wote hawajatoa nafasi za juu za uongozi ndani ya chama. Wanawake wanaanza kuonekana kwenye Kamati Kuu na Halmashauri Kuu.

  Chadema hawana serikali (ukiacha huo mtanange wa uspika) labda wao wanaweza kutoa fursa kubwa zaidi kwa akina mama zaidi ya CCM wakipata serikali :smile:
   
 14. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  William, mimi nafikiri sio kweli kwamba wanawake wengi hawakuipigia kura CHADEMA eti sababu ya muonekano wa hasira wa viongozi wa chama hicho. Kwangu mimi sababu kubwa ni ile hatua ya Jeshi kutoa vitisho vya machafuko na ile kauli mbiu ya umwagaji damu ambayo CCM waliigeuza kuwa mtaji wao wa kampeni. Kumbuka hata kule Songea JK alisema wasiwachague watakaoleta umwagaji damu kwani baada ya kuwachagua wao(wapinzani) wataleta vita na kukimbilia ulaya na kuwaacha wao wakipigana, sasa kwa kauli kama hii unategemea nini kwa mwanamke hasa hasa yule wa kijijini asiye na ufahamu wa kupambanua mambo kuwa yule atakaye leta vita ni yule aliyeko madakani ambae atakataa kuondoka na ataleta vita ili aendelee kubaki na huyu angekuwa ni CCM

  Hii ni stategy ambayo CCM wamefanikiwa kwa kiasi fulani kwani binafsi nilitumia kazi kubwa sana kumconvice mama yangu kule kijijini kuondoa kasumba hii hadi akafahamu ukweli. Siku ile ya mdahalo wa Slaa ITV nilimtumia hela ili anunue petroli aweke kwenye kajenereta kake yeye na mzee waangalie ITV na waone wenyewe kama yale wanayosikia kwenye mikutano ya CCm ni sahihi hii ni baada ya ushawishi mwingi sana akakubali na believe me kipindi kilipoisha alisema huyu ndo anafaa kuwa rais na zile alizokuwa anasikia ni porojo na huyu Silaha hayuko kama vile wanavyomsema. Siku ya JK nilimwambia afanye vile vile tena na yeye mwenyewe akasema mbomna maswali ya huyu wa leo ni tofauti na yule mwenzake, mbona huyu ni kama waandishi wameandaliwa???

  sasa huu ni mfano wa huyo mama mmoja tu, hebu fikiria ni mama zetu wangapi ambao hawana elimu sahihi na chanzo chao cha habari ni radio tanzania ambayo wakati wote iliifagilia CCM???? Kwa hiyo kusema CHADEMA imeshindwa sababu haina wanawake wengi kwenye nafasi za juu za uongozi sio sahihi. Wako wanawake kama Regia,Rose kamili,Kaihula,Letisi nyerere na wengine ambao walishindana vilivyo na bado wako wanawake huko waliochagua wagombea wa CCM wanaume sababu ya hizo nilizotoa hapo juu japo hawa wanjawake wenzao walikuwepo?

  CCM wamekuja na sababu ya kumpiga chini Sitta kuwa walitaka bunge liongozwe na mwanamke safari hii, lakini believe me kama huyu mama akifeli kwenye kazi yake kulinganisha na spika aliyetoka basi hizi harakati za kuwawezesha viongozi wanawake will face huge dissapointment
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa hana tofauti na vuvuzela ..niulize kwa nini
   
 16. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280

  Great Thinker Malecela,

  sidhani kama umefanya analysis zako vizuri za uchaguzi uliokwisha, na hiyo tathimini yako unayoitoa ni kama vile wewe umesoma ama kuambiwa, na chanzo chako hicho hakikuwa sahihi kwa sababu kilikuwa kinakupa habari za Wanawake na Chadema tu, na wala sio vyama vingine na wanawake

  1) Vyama vyote vya siasa Tanzania viko sawa kwa agenda yako hiyo ya wanawake unayoizungumzia, hakuna hata chama kimoja (Hata CCM) chenye mwanamke katika post za juu za uongozi wake, sasa hilo la Chadema sijuhi limekujaje hapo, ungekuwa fair labda ungezungumzia vyama vyote viliangalie hilo,
  kwa kifupi hiyo haikuwa sababu ya Chadema kufanya vibaya

  2) Viongozi wa Chadema wana hasira,
  labda ungefafanua wana hasira ya nini? ama ya namna gani?, maana kuna tofauti ya hasira na uchungu, ungeniambia viongozi wa Chadema wana uchungu sana na nchi yao, wana uchungu wa haki, na wana uchungu wa kuwapa raia wote wa Tanzaznia maisha bora hapo ningekuelewa,
  Huwezi kuwa na Rais kama JK, kazi ni kuchekacheka tu, hakuna seriousness ya chochote anachoongea, anachotenda wala anachotekeleza

  Ndugu yangu William,
  kuna sababu nyingi mno za Chadema kushindwa(Kama kweli walishindwa) uchaguzi uliopita, na hizo ulizozitaja hakuna hata moja,

  nadhani swali lako labda lingekuwa ni nini chanzo/sababu ya Chadema kushindwa uchaguzi? hapo ndipo ungepata hoja ya kuanzisha, lakini kwa kifupi wewe elewa hivi

  WANAOPIGA KURA NI RAIA (WATANZANIA) NA WANAOCHAGUA NI NEC/CCM/JWTZ/UWT/POLICE
   
 17. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #17
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Mawazo yangu ya hovyo lakini yamekugusa mpaka umekuja kujibu mtumzima, halafu unawadanganya wengine vipi brother ha! ha! ha! ha! hivi kwa nini mkiguswa na ukweli huwa mnakuwa na hasira sana unajua mnaogopesha sana eti!


  - Otherwise, ni kweli nina-genenralize kutokana sample za matokeo ya uchaguzi wa Rais, zinazo onyesha kwamba wanawake wengi sana wamempigia kura mgombea u-Rais wa CCM na pia wameulizwa katika nyakati mbali mbali za uchaguzi na kujibu hivyo!


  William.
   
 18. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #18
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Historia yake na ufisadi yaani Spika mpya iko wazi sana na inajulikana sana, kujua au kutokujua ufisadi kwa mantiki yako wewe eti inaweza kumfanya mhusika awe au asiwe kiongozi anayefaa, bado sijaelewa hii mantiki!


  William
   
 19. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #19
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Kina mama wengi waliohojiwa kuhusu upigaji wao wa kura kwenye huu uchaguzi wamesema kwamba waliogopa kwamba kutoipa CCM kura ni kukaribisha vita kutokana na hasira za ajabu zinazoonyeshwa na upande wa pili!


  William.
   
 20. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #20
  Nov 13, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Kama unayaamini haya uliyoandika hukuwa na sababu ya kujibu mkuu, lakini umesikika sana!.

  William.
   
Loading...