Uchaguz wa USA 1960, Aliye Iba Kura Zaidi Ndiye Alishinda

Iceman 3D

JF-Expert Member
Sep 3, 2016
20,629
2,000
Uchaguzi wa Rais wa USA ulio fanyika mwaka 1960, ulikuwa ni kati ya Richard Nixon wa Republican ambaye alikuwa pia ndiye makamu wa rais kwa wakati huo VS John Kennedy wa Democrat aliyekuwa Senator kijana, handsome , tajiri na mtoto wa baba yeke mpendwa aliye kuwa na ushawishi mkubwa Mr Kennedy sr.
Uchaguzi huu ulihusisha wizi wa kura ambao haukupata kutokea kwa Marekani, pia ulihusisha michezo michafu mingi sana kwa wakati huo, kwa kuwa ulikuwa ni uchaguzi ambao yeyote angeweza kushinda.
Mshindi wa jumla
Kennedy alishinda kwa tofauti ya kura laki moja (113,217) kati ya kura zilizo hesabiwa milioni 68, electoral votes zilikuwa 303-219, majimbo yaliyo mpa ushindi kannedy ni mawili Texas na Illionois ambayo ukijumlisha yana electoral votes 51, jimbo la California siku ya uchaguzi alishinda kennedy, lakini baada ya wiki 3, absentee ballots zilifanya ushindi wa California upelekwe kwa Nixon tena, na kuna madai kuwa kura za absenteeism zilikuwa nyingi kuliko data za uchaguzi zilivo kuwa zina onesha kwenye jimbo hilo.

Huko Hawaii, mwezi mmoja baada ya uchaguzi jaji aliamuru Kennedy anyang'anywe ushindi na apewe Nixon kwani waangalizi wa uchaguzi walikosea katika kumtangaza mshindi wa jimbo, nadhani walibadilisha majina ya mshindi na mshindwa

Texas, Kennedy alishinda kwa tofaut ya kura 46,000, lakini Watu wa Republican walidai mgombea mwenza wa Kennedy bwana Johnson alikuwa na mwizi mzuri wa kura na hata kwenye useneta alizoea kuiba kwani mwaka 1948, Johnson alishinda u seneta kwa kura 87 lakini maboksi yenye kura zaidi ya 20,000 yalipotea na hayakupatikana hadi leo, kwa hiyo jamaa alikuwa ni mzoefu wa wizi, na pia kura nyingi za Nixon ziliharibika kwani, ilitakiwa mpiga kura akisha mpigia anaye mtaka, afute jina la asiye mtaka, hivo wengi walio mchagua Nixon kura zake karibu 50,000 zilitupwa nje na hazikuhesabiwa.

Illinois, huko Chicago ndio ilikiwa ni vituko, Kennedy alishinda kwa kura 8,800 tuu kati ya kura milion 4, lakini Kennedy alishinda county moja inayo itwa Cook kwa kura zaid ya 450,000, ilikuwa ni maajabu kwani county karibu zote nyingine alishindwa, pia kuna kura za vijiji zilizo kuwa na wapiga kura 500 lakini Nixon naye alishinda kwa tofauti ya kura zaid ya 700 kwenye vijiji hivo, wakati kura za vituo 405 vya Cook county zilivo rudiwa tena kuhesabiwa zilionesha karibu asilimia 40 ya idadi ya kura za Nixon ilizidshwa.

Nixon alishindwa Illinois kwa sababu meya wa Chicago alikuwa ni wa chama Kennedy na alikuwa ni rafiki mkubwa wa baba yake Kennedy, lakin pia inadaiwa wiki mbili kabla ya uchaguzi ali waambia watu wa chicago hata wakipiga kura kwa namna gani ata hikisha Kennedy ana shinda. Uchunguzi wa baadaye ulibaini kuwa wasimamizi wa vituo na wasimamizi wengi wa county walikuwa wana amrishwa na Meya wapige kura kwa Kennedy na wahakikishe wamejaza maboksi ya kura, pia kulikuwa kuna kesi za wapiga kura kupewa lunch siku ya uchaguzi, watu waliokufa miaka ya 1940 walipiga kura, pia inasmekana kwenye vituo zaidi ya 1300 wapiga kura walikuwa wakikabidhiwa mvinyo kabla au baada ya kupiga kura na timu za kampeni au wasimamizi wa vituo, pia hata watoto wenye miaka 9 na 10 walipiga kura kinyume na sheria, pia kuna vituo ambavyo vilileta kura lakini vilipo fuatiliwa vilikuwa ni vituo hewa hasa vingi vilikiwa majina ya maeneo ya kuzikia na hakuna aliye piga kura huko, mpaka uchaguzi unaisha takribani watu 670 walifungwa kwa makosa yaloyo tokana na uchaguzi hiyo county ya Cook Illinois. Wakiwemo watu 7 ambao waliandaa mabasi yaliyo kuwa yakihamisha wapiga kura wakapge kura vtuo zaidi ya kimoja. Lakin matokeo ya Cook bado hayakubadilishwa. Na Kennedy akawa Rais wa 35 wa Marekani.

Nixon alijua kuwa kapokwa ushindi, pia Rais Ike na bosi wa FBI Edgar Hoover walijua hilo lakini walimsihi Nixon akubali yaishe ili nchi isiingie kwenye machafuko na kuonesha image mbaya ya demokrasia, hasa kwa kuwa kilikuwa ni kipindi cha Cold war. Nixon pia alikubali lakini tukio hili lilibadilisha kabisa maisha yake ya siasa na ndio mwanzo wa safari ya Nixon kuelekea kwenye majanga zaid kama Watergate kipindi alipo upata Urais.

Nixon naye yeye ali iba na alifanya kila faulo, ila Kennedy na Johnson wali mzidi kwenye utaalam wa kuiba mnooo na kumnyang'anya ushindi wake.

*Pengine hata bongo mwaka jana ilikuwa hivo. Lakini wenzetu USA katika wizi huo walipata mmoja ya viongozi bora katika historia ila sisi pengine tulimpata kiongozi mbovu katika historia. Kama kweli ilitokea uibaji wa kura lakini. Kila chaguzi zina vituko vyake lakini 1960, ilitisha zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom