Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,377
- 217,440
Mamlaka husika isijaribu kumkufuru Mungu kwa kutengeneza hadithi ya kutunga kuhusiana na Uchafu uliokubuhu ndani ya Uwanja wa soka wa Mkapa.
Ukweli ni kwamba Wizara husika imeshindwa kabisa kusafisha uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watu elfu 60, kutokana na ubahili, uwezo mdogo wa viongozi, hulka tu ya uchafu ambayo imewajaa viongozi wa uwanja huo au Ushamba.
Wakati wa Kongamano la Mwamposa la VUKA KABLA YA KUVUKA, kulikuwa na kikosi kazi cha waumini waliojitolea kufanya usafi kwenye maeneo yote pamoja na Chooni, baadhi ya Waliojitolea kufanya usafi kwenye vyoo kwa usiku ule WALIBARIKIWA na kufanikiwa mambo yao baada ya Mungu kuwatendea, nimeona Ushuhuda wa Msafisha choo wa kujitolea kwenye kongamano lile, akidai kulipwa fedha alizokuwa anadai kwa muda mrefu, ambapo alidai Mungu alimfungulia milango baada ya kujitolea kusafisha vyoo.
Hii maana yake ni kwamba Mwamposa na kundi lake walikwishajipanga kwenye maswala yaliyohusu Usafi wa eneo lile na walifanikiwa.
Kwahiyo kushindwa kwa mamlaka husika kwenye usafi wa uwanja huo, wasimwangushie jumba bovu Mwamposa.