Uchafu wa NSSF kwa mujibu wa CAG report

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,781
3,209
Utekelezaji wa Mkataba wa Ubia katika Mradi wa Mji wa Kisasa wa Arumeru kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Ltd (AHEL)

Kama ilivyoonekana katika mwaka wa fedha uliopita na katika mwaka huu wa fedha, shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii ilianzisha mradi mwingine wa kujenga mji wa kisasa katika Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha kupitia kampuni iliyoanzishwa kwa ubia na kampuni ya Azimio kwa jina la Hifadhi Builders Ltd Kifungu cha 5 cha mkataba huo kinaonyesha pande zote zimekubaliana kutoa kiasi cha mtaji unaofikia Dola za Marekani bilioni 3.34 (Shilingi Trilioni 7.2) na ushauri wa
kiufundi kwa ajili ya uanzishaji wa mji huo wa kisasa ambapo asilimia 20 (sawa na Dola za Marekani milioni 668.12) imefanywa kuwa thamani ya ardhi ambayo Azimio amekubali kutoa ardhi ya ekari 500 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi huo.

kutoka Azimio Housing Estate Ltd kupitia barua yake ya tarehe 16 Mei 2013 yenye kumbukumbu Na. AZIMIO/NSSF/ARUMERU/13/5. Ambapo Bodi ya Wadhamini iliidhinisha kuingiza katika ubia ardhi iliyotolewa na kampuni ya Azania katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Mwanza na Arusha kwa ajili ya uwekezaji unaofanana na huu.

Ada ya ushauri kwa ajili ya kubuni mradi huo ni Dola za Marekani milioni 218.09 (Shilingi bilioni 468.9) na ilipangwa Shilingi bilioni 2.4 itumike katika awamu ya upangaji wa mradi. Hata hivyo, kiasi hicho kiliongezwa hadi kufikia Shilingi bilioni 102 bila ya idhini ya Bodi. Kiasi halisi cha ada ya ushauri mpaka kufikia mwisho wa mwaka kilikuwa Dola za Marekani milioni 20.1 (Shilingi bilioni 43.9) kutoka katika Dola za Marekani bilioni 102 za ongezeko.

Tarehe 20 Januari 2016, shirika na kampuni ya Azania walisaini makubaliano ya kusitisha utekelezaji wa mradi huu kwa makubaliano ya pamoja. Uongozi wa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii umetoa sababu ya kutokulipwa marejesho ya mikopo yake kutoka kwa Serikali kama sababu ya kusitisha mradi huo. Kama ilivyoainishwa katika makubaliano ya usitishaji, kiasi cha Shilingi bilioni 43.9 ilicholipwa na shirika kama sehemu ya ada ya ushauri ibadilishwe kuwa mkopo ambao utarejeshwa na kampuni ya Azimio kupitia sehemu ya Mauzo ya nyumba katika mradi wa Dege ndani ya miaka mitatu kwa riba ya
asilimia 3 kwa mwaka.

Kuingia katika mradi bila kujihakikishia uwepo wa fedha kungeweza kusababisha gharama zisizo za lazima pamoja na matumizi mabaya ya rasilimali kwa upande wa shirika. Uongozi unatakiwa kuhakikisha uwepo wa fedha za kutosha kuendesha mradi uliopangwa kabla ya kuingia katika mkataba. Pia, linapaswa na kuhakikisha kiasi cha Dola za Marekani milioni 20.1 (Shilingi bilioni 43.9) kinarejeshwa katika muda stahiki kwa kuzingatia mabadiliko ya thamani ya fedha kulingana na muda.

kwa taarifa zaidi tembelea website ya NAO. www.nao.go.tz
 
Fanya hesabu ujue heka moja imenunuliwa bei gani ndio utaumwa kichwa .......its more than 2.87 bilioni sh per heka
 
Hivi hakuna conflict of interest katika uandaaji wa taarifa za NSSF ...kwa ajili ya matumizi ya CAG ?
 
Conflict of interest inatoka wapi ? Yeye kakagua mikataba kakuta ufisadi wa kutisha humo......
 
Hamuelewi mnachokiongea. Weka hapa huo ufisadi tuuone siyo unatuwekea link yenye maripoti kibao.
 
Fanya hesabu ujue heka moja imenunuliwa bei gani ndio utaumwa kichwa .......its more than 2.87 bilioni sh per heka
hawa watu ni wapumbavu ,kwa nini watengeneze mkataba ambao una abei ambayo haiendani na market price ya ardhi.Kuna vitu ambavyo unaweza kudanganya kama gharama za ujenzi lakini hata hizo huendi kwenda zaidi ya plus or minus 200%.Sasa ardhi ambayo price yake inaweza kukadiriwa na mtu wa kawaida una-draft mkataba kwamba 1 acres umenunua 2.87 billions.Watumbuliwe maana hawana hata uwezo wa kuiba kiujanja
 
Mkataba wa Kuendeleza Mji wa Kisasa wa Kigamboni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii limeingia ubia na
Kampuni ya Azimio Housing Estates kuwanzisha kampuni maalumu kwa jina la Hifadhi Builders Limited. Katika
mkataba huo, Azimio Housing Estates itatakiwa kuendelezaekari 20,000 za ardhi zilizopo Kigamboni ambapo kwa hatua
ya awali itaanza na ekaris 300. Katika ubia huu, Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii inamiliki asilimia 45 ya hisa wakati Azimio Housing Estates inamiliki asilimia 55 ya hisa. Jumla ya gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 653.44 na utaratibu wa uchangiaji mtaji ni kuwa shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii litatoa fedha zenye thamani ya asilimia 45 ya gharama za mradi na azimio itatoa fedha zenye thamani ya asilimia 35 ya gharama za mradi pamoja na ardhi ambayo itathaminishwa kuwa asilimia 20 ya gharama za mradi.

Ukaguzi wa hatimiliki umeonyesha kuwa Azimio Housing Estates inamiliki viwanja viwili, kiwanja chenye hatimiliki Na. 81828 kiwanja chenye ukubwa wa hekta 1.98 na chenye hatimiliki Na. 105091 chenye ukubwa wa hekta 114.11. Viwanja vyote vinapatikana katika eneo la Rasi Dege ambavyo kwa pamoja vilihamishiwa kwa Hifadhi Builders kutoka kwa Azimio Housing Estates kwa ajili ya Awamu ya Kwanza ya mradi. Kwa kutumia kizio cha ekari 2.47 kwa hekta, hatimiliki hizi zitakuwa na ukubwa wa jumla wa ekari 286.74, pungufu ya ekari 13.26 kutoka kwenye ekari 300 ambazo zilipangwa kwa ajili ya Awamu ya Kwanza ya mradi.

Sijaweza kupatiwa hatimiliki za ardhi ambayo Azimio aliahidi kutoa kama uchangiaji wa mtaji. Hivyo imekuwa vigumu kwangu kuthibitisha uwepo wa viwanja hivyo. Kwa kukosekana kwa hatimiliki, umiliki wa ekari 19,700 za ardhi ambazo sehemu ya mtaji wa Azimio Housing Estates kwa asilimia 20, fedha za shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii zinakuwa kwenye hatari ya kupotea.

Menejimenti inashauriwa kuwasiliana na Wizara ya Ardhi ili kuhakiki umiliki wa heka 19,700 za Azimio Housing Estates
katika eneo la mradi. Pia, hatimiliki za ekari 13.26zilizokuwa pungufu kwenye Awamu ya Kwanza ya mradi zinahitajika kuonekana
 
someni ripoti ya mashirika ya umma ukurasa wa 31 hadi 33 mtaona haya madudu ....Wanaingia ubia wa mabilioni bila kuona hata hati miliki ya ardhi .....kesho utakuta mwenye ardhi mwingine pesa inazama .....Hii Azimio ni ya kuchunguzwa sana .
 
Kuna watu wanatetea huu wizi ? Ni watanzania kweli hawa ? Wafanyakazi wanapoteza jasho lao kwa masilahi ya kikundi cha watu wachache ambao walijitengenezea Himaya yao......
 
Zitto alituhumu vyombo vya habari kuwa viliandika uongo na alikuwa anasubiria ripoti ya CAG ndio angetoa kauli , kashaiona kaufyata .........Kuna SACOSS zilipata mgawo mpaka shilingi Bilioni Moja na moja ni ile ya Bumbuli Development ......Mwenyekiti ni January Makamba .......CAG kahoji kwenye ripoti yake .......zipo nyingine ni za kufuatilia wamiliki wake ......
 
Back
Top Bottom