Uchache wa Magari ya Mwendokasi barabarani kutokana na mengine kuharibika na mvua, wananchi tunateseka

Hayo uliyoandika ungewashauri wangekusikia kuliko kuja na conclusion ya kuondolewa. Kuna watu yanawasaidia sana tofauti na unavyodhani
Binafsi, pamoja na kero hususani uchache wa mabasi mida ya abiria wengi lkn yamenisaidia sana kupunguza muda wa kukaa barabarani. Suala la tiketi sio ishu, kama ni mtumiaji wa mara kwa mara wa usafiri huu nunua kadi, hutapata shida yoyote kupanga foleni kusubiri tiketi.
 
Wee bila shaka ni mmoja wa wale wabeba samaki wanaosumbua asubuhi na makelele yao.
Alafu ni mabasi yaendayo haraka sio mabasi ya mwendo kasi!
Nina gari yangu kaka
Sina biashara ya samaki japo nayo ni kazi kama kazi nyingine
 
Mimi pamoja na kero hususani uchache wa mabasi mida ya abiria wengi lkn yamenisaidia sana kupunguza muda wa kukaa barabarani. Suala la tiketi sio ishu, kama ni mtumiaji wa mara kwa mara wa usafiri huu nunua kadi hutapata shida yoyote kupanga foleni kusubiri tiketi.
Kadi hazipo kaka nisingepata shida hivi
 
Wewe ni Mbinafsi, unataka Mabasi yetu yaondolewe kwa sababu tu hayaendani na matakwa yako? Vp maelfu kwa maelfu ya wakazi wa Dar wanaofaidika nayo kila siku?
Kama ungesoma mada vzr usingekurupuka hivi
 
sisi wakazi wa huku mbaagla hatuuoni umuhimu wa mwendokasi, ukikubaliana nao hao jamaa zako sawa tu yaondoeni hakuna shida
 
Jioni magari mengi ya mwendo p9ole pole hayapakii abilia na kuacha abiria vituoni. Unakuta gari lina display DEPOT, hasa yanayotoka kimara. Kingine inashangaza sana unakuta saa moja magari wameshapaki kimara.
 
Nunua kadi urecharge kwa muda wako,unakata vile vitiket vya karatasi afu hutaki usumbufu?mimi nina kadi mbili na nimehama mkoa niambie nakupaje hizo kadi wewe na shemegi naye asipate usumbufu?sio Masikhara nilinunuua kadi ikapotea au nikaimisplace,ikabidi ninunue nyingine,Siku moja akaja mdogo wangu Amina akafanya usafi akaiona nikawa nazo mbili sasa sema tufanyeje uzipate ili uwe unajaza tu kiasi na kumjazia shemegi kuepuka huo usumbufu.
 
Jioni magari mengi ya mwendo p9ole pole hayapakii abilia na kuacha abiria vituoni. Unakuta gari lina display DEPOT, hasa yanayotoka kimara. Kingine inashangaza sana unakuta saa moja magari wameshapaki kimara.
Kuna kambinu nimeamua kukatumia kaka naona kanamanufaa kiasi fulani
Nikitoka zangu town napanda mwendo pole pale fire nakuja kushuka korogwe sio kimara halafu nachukua daladala za kawaida naunga mbezi ila ukishuka kimara inatafuna kwako kaka
Naona ndio mechanism na plan b hiyo kaka
 
Habari za jpili wandugu

Aiseee binafsi haya mwendo kasi sioni umuhimu wake kiviiiile kutokana na mambo yafuatayo:-
a. Yanaitwa ya mwendo kasi lakini yako slow sana njiani ukilinganisha kwamba yanabarabara yake yenyewe lakini wako slow sana mpaka wanakera aisee

b. Ukataji wa tiketi ni wa shida sana yaani ni kero kwa kweli, sijui wanampango gani na hizo tiketi kama ikiwezekana waweke hata makonda tu potelea mbali

c. Haya mabasi ya kutoka kivukoni,gerezani kwenda kimara ni machache sn kama wamekuwa waelewa basi ni afadhali waende na movie ya abiria kwamba kuanzia majira ya asbh na jioni watumie mabasi mengi zaidi kuwatoa watu kwenye vituo halafu mchana wanakuwa wanapumzika

d. Ikiwezekana mabasi yatoke kivukoni kwenda mpaka mbezi sio kuishia kimara wengine tuna mizigo

e. Na kama ikionekana hakuna namna basi waruhusu dala dala zitoke mbezi kariakoo uone kama watapata watu kwanini wanawazuiaaaaaa

Aiseee nina povu jingi nivumilieni tu inakera sana, sio kwamba hatuna magari ila kila siku hatuwezi kwenda nayo job kutokana na parking, mafuta, foleni nk

Mimi nadhani suluhisho kubwa la matatizo yako ni kununua tu Gari yako au Pikipiki yako au uwe tu unakodi Bajaji kama siyo Teksi.
 
Kadi hazipo kaka nisingepata shida hivi
Labda zimeisha. Wengine tulinunua kadi mara tu zilipotangazwa kuanza kutumika. Huwa nawashangaa tu watu wamepanga foleni ndefu ya kukata tiketi kila siku wakati bei ya kadi ni 500 tu unalipia na kifurushi cha 4500.
 
Nadhani kusema yaondolewe si vyema hasa ukizingatia kiasi cha gharama za miundombinu yake zilizotumika mpk sasa nk..




Bali nakiri kuwa huduma ingeboreshwa ili iwe bora zaidi..
 
Back
Top Bottom