Ubunifu wimbo wa Jumuiya Afrika Mashariki una kasoro ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunifu wimbo wa Jumuiya Afrika Mashariki una kasoro ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bikra, May 13, 2009.

?

Je ! Staili hii ya Wimbo inakubalika ?

Poll closed May 23, 2009.
 1. Ndio

  0 vote(s)
  0.0%
 2. Hapana

  33.3%
 3. Sina Uhakika

  33.3%
 4. Sijui

  33.3%
 1. Bikra

  Bikra Senior Member

  #1
  May 13, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  CD yenye nyimbo sita ambazo ni mbilimbli kutoka Kenya Tanzania na Uganda imezinduliwa.

  Hivyo basi, Watanzania sasa ni wakati wenu kutoa maoni juu ya nyimbo hizo bila ya woga wala kificho, kwani hii ni ‘last chance kwa kila Mtanzania’ kusema ukweli kama nyimbo hizo zinavutia na kupendeza.
  Kwa kuanzia, si jui niseme ule ulikuwa ni mkutano wa ‘Listen Party’ ya nyimbo za Jumuiya ya Afrika Mashariki au namna gani, hapo nilibaki njia panda kidogo, hasa pale nyimbo hizo zilipoanza kwenda hewani, yaani kwa ufupi mirindimo yake ni ya kidini mno, katika hilo hawajawatendea haki Watanzania walio wengi.

  Si kwamba nyimbo hizo si nzuri, ni nzuri lakini zimelalia upande mmoja, hazina hamasa, japokuwa zina tungo nzuri, yaani nyimbo zote zimepooza.
  Raha ya wimbo ni kurindima kwa vyombo pamoja na uchangamfu na ucheshi wa waimbaji husika, hivyo wanakwaya hao walipaswa kuwapa wasikilizaji hamasa na ari ya kusikiliza wimbo huo.
  Watanzania wataungana na Wakenya na Waganda katika kutoa maoni yao ni wimbo upi kati ya hizo sita unafaa kuwa wimbo wa jumuiya.
  Laiti kama ingelikuwa ni amri yangu, mimi ningeamuru nyimbo zote zifutwe, hasa za Tanzania na kuwaamuru wamiliki wa bendi zote kukaa na watunzi na waimbaji wao, nina imani katika hilo Tanzania ingeibuka na wimbo mzuri na wenye mvuto na kuzikonga nyoyo za wanajumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.
  Wanahabari ambao walikuwapo kwenye uzinduzi huo walianza kunong’ona chinichini kuwa nyimbo zote ni mbaya, hazifai, hivyo basi ziligawanywa karatasi za kutoa maksi na maoni binafsi kutokana na nyimbo hizo, wengi walitoa maoni yao huku kila mmoja akikosoa kisiri na dhahiri.
  Nyimbo hizo zitasikilizwa kupitia redio mbalimbali na kuonekana katika vituo vya televisheni, maoni ya wananchi yataratibiwa na wimbo utakaopendekezwa kuwa unafaa utatolewa maamuzi.
  Kwa mtazamo wangu, nasema hivi, jambo hili lilipaswa kuwashirikisha wasanii wote na si vikundi vya kwaya 35 kama tulivyoambiawa ama kama ilikuwa ni ngumu zaidi, ni bora wangewataka walimu shuleni kutunga na wanafunzi kuimba, hapo kidogo mambo huenda yangekuwa safi kutokana na kwaya za shule zinavyokuwa na mpangilio mzuri wa sauti na mara nyingi huwa na nyimbo nzuri.
  Lakini kama suala lilikuwa ni kutaka wimbo, tena wa kushindanisha bendi, si zipo wangewaambia tu nadhani ingekuwa taabu kwa Jopo hilo kupitisha wimbo gani.

  Siku zote mdharau kwao ni mtumwa, nini maana ya kuwa na bendi nyingi nchini tena zenye watunzi mahiri na wenye tungo zenye ujumbe mzito?
  Katika hili, Watanzania tumechemsha, tukumbuke wanamuziki waliweza kutumika vyema na kutoa hamasa wakati wa vita ya Tanzania na Uganda kati ya 1978 -79. Bendi ya jeshi ya Kimulimuli wakati huo ikiwa na mwanamuziki mmoja Zahir Ally Zorro, aliyetunga nyimbo kama ‘Mashujaa’, ambao ukiusikiliza hata leo utafurahi na kuona kama unaangalia sinema.
  Labda kwa kukumbushia tu mashairi machache yaliyokuwapo ndani ya wimbo huo wa kuhamasisha wapiganaji wetu ni haya:

  'Wazazi wazazi wetu eeh, mashujaa walokufa wamekufa kishujaa, mashujaa walorudi wamerudi kishujaa, lengo na nia yetu wazazi ilikuwa moja kuilinda hadhi yetuee'.

  Licha ya nyimbo hizo, pia tuchukulie mfano wa nyimbo nyingi za kitaifa, tena za zamani ambazo hata watoto wetu wanaozaliwa sasa na wanao chipukia humudu kuziimba kama ‘Tazama ramani’ uliotungwa na kiongozi wa 'Police Brass Band', Mayagilo; Tanzania, Tanzania, wimbo wa taifa na nyinginezo nyingi, bado nzuri na zitaendelea kuwa nzuri.

  Hivi kwanini mmekurupuka katika jambo kubwa kama hilo halafu eti mnataka watu watoe maoni ya kuchagua wimbo tena kwa lazima mnataka wimbo mmoja upigiwe kura ilhali nyimbo zote hazifai.

  Hii ni tofauti na ilivyo sasa wimbo hauimbiki wala hausisimui hivyo kwa maoni tu ni bora Wanajamii katika Blogu yetu Hii tutunge wimbo na tuupendekeze kwa Waziri! , Ama Mnasemaje ?
   
  Last edited: May 13, 2009
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  wimbo kama wa dini vile
  haujabeba ubantu au uasili wa afrika mashariki.
  walioweka vigezo vya wimbo ni western brain washed
   
Loading...