Ubunifu wa Mamsapu Wangu Umezaa Matunda Sasa Anakula Kile Roho yake Inapenda

Dumelambegu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,052
257
Wandugu,
Mwenzenu niliugua ugonjwa wa amoeba kwa muda wa miezi kama mitano hivi. Kama baadhi mnaweza kujua kwamba ugonjwa huu, ukishaingia kutoka kwake ni kazi sana. Ilikuwa nakunywa dawa mara kwa mara lakini nikipima naambiwa bado amoeba ipo. Baadaye nilishauriwa ninywe dozi tatu mfululizo. Nilifanya hivyo na kupona lakini wakati natibu amoeba kumbe nilikuwa nasababisha madhara kwa "mzee" wangu. Ghafla nilishangaa mzee hanyanyuki na kushindwa kabisa kupanda mlima. Pamoja na jitihada za mamsapu wangu kumshikashika lakini wapi.

Kwa kweli wadau nilikosa raha. Nilijua udume wangu wa mbegu ndiyo umeishia hapo. Lakini siku moja mamsapu wangu katika pitapita yake alisikia kwamba supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa njegere mbichi bila kuungwa chochote ni mlo muhimu sana kwa wanaume. Basi bila hata kuniambia chochote akaanza kuniandalia huo mlo kila asubuhi. Bahati nzuri mamsapu wangu ni mfugaji mzuri sana wa kuku wa kienyeji. Kila baada ya siku mbili au tatu ilikuwa lazima nipate hiyo menu. Nimefanya hivyo kwa mwezi mzima.

Baada ya wiki kama mbili hivi tangu nianze huo mlo tukiwa tumetulia kwenye 6x6 mamsapu wangu akaanza fujo zake. Nilishangaa sana kwani haukuchukua hata dakika mzee alisimama kwa hasira isiyo ya kawaida. Nilimpa haki yake mamsapu wangu na performance yangu siku hiyo ilikuwa no record tangu tuanze huo mchezo miaka takribani minane iliyopita. Kuanzia siku hiyo mpaka leo wikiendi zote angalau mara mbili au tatu lazima nipate supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa na njegere mbichi. Kwa hiyo, wale wenzangu na mimi kama nanyi mmepitia mabonde na milima kama yangu, tafadhali anzeni kupata mlo huo. Unarejesha heshima ya Baba ndani ya nyumba.
 
Sawa mzee tukisha fikia hatua hio tutajaribu, lakini mimi bado na amini wazi sex inaenda na family route kama babu yako alikuwa anawasukumia rungi wanawake mpaa ana miaka 130, unaweza kuwa mrithi mzuri sana but do not forget this one thing, sex drive varies from one to another....Some men are sex addicts, while there are those who have extremely low interest in sex hata wale nini :biggrin1:
 
Ndio maana kwenye avatar yako kuna jogooooo...........Tahadhari hapa JF unatakiwa kuwa kama mbayuwayu
 
Ha ha ha haaah!! JF kuna vituko....!! Sasa ukiacha hiyo supu hali ya mtalimbo ikoje??
 
Kwa hyo wwe ni udume wako wangùvu ya supu.....? Tafuta suruhisho lakudumu

Najaribu kufikiria kuwa inawezekana Dumelambegu alikuwa anamaanisha kuwa akina dada au wanawake wanaoishi kindoa na wenzi wao wanamchango mkubwa na pengine wanaweza kuwasaidia waume zao wenye matatizo ya "kupiga mambo" kwa jitihada zao binafsi kama alivyofanya mkewe badala ya kumkimbia au kwenda kutafuta viserengeti vya kwenda kuburudika navyo.

Na kwa sababu tatizo lake lilisababishwa na amoeba, na kutibika kwa supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa njegere mbichi, naamini akitumia kwa muda fulani huenda akapona kabisa. Najaribia kumfikiria kuwa inawezakana aliandikia hii kuwatia moyo akina dada kutumia ubunifu wao kusolve matatizo kama hayo badala ya kulalamika na kutoa siri nje ya ndoa na kuishia kujiachia bila heshima wala utu kwenye vifua vya wakware.

Hata hivyo, nafikiri wenye matatizo kama haya wanaweza kuanza kujaribu kutumia supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa njegere mbichi na kutupa ushahidi kama imefanya kazi vzr. Zaidi ya hapo, wenye taalum ya udaktari ni vyema nao wakatueleza kama kweli kuugua amoeba kwa muda mrefu kunaweza kuleta tatizo hili ...

Shukrani kiongozi kwa kufikisha ugunduzi wako JF, yumkini kuna baadhi ya watu wanaweza kunufaika kwa namna moaj au nyingine! ....

HorsePower.
 
Jamani siyo uwongo supu ya kuku wa kienyeji na njegere ni kiboko kwa kumshtua mzee. Mimi niligundua muda mrefu na huwa najitahidi kupata mlo huo angalau mara moja kwa wiki. Muziki siku zote umekuwa mzito.
 
Tena kuku mwenyewe awe jogoo mchanga; duh yaani unarudi kama ulivyokuwa 16yrs!
 
Back
Top Bottom