Ubungo tunaibiwa !

MwanaCBE

JF-Expert Member
Sep 23, 2009
1,771
804
Wapi SUMATRA....??? Sasa hivi nimepanda basi kuelekea dom (baada ya kusheherekea ushindi ubungo na kawe) linaitwa SHAHBAL, tiketi imeandikwa sh 12,000 nauli lakini unalazimishwa kulipa 20,000 hautaki hauna safari. Na hii ni kwa magari yote yanayoenda Dodoma. Sijui kwenda mikoa mingine..!!!!
 
Nadhani pana kituo cha Polisi hapo...huo ni wizi wa mchana kweupe.
Ripoti mara moja, usilee uzembe!
 
Kidumu chama cha mapinduzi

Vumilia, muziki wenyewe ndio huo, hapo wanarekebisha vyombo, ikifika 2015 mtakoma.

Gharama za maisha ni lazima zitapanda kwa asilimia 2000.(2000%) Bei ya mafuta umeiona ilivyopanda leo.
 
jimbo la ubungo si tumemchagua MNYIKA.......chaDEMA WAMESHAANZA KURUDISHA GHARAMA ZA UCHAGUZI....... YAANI HATA WIKI BADO MSHAPANDISHA NA NAULI?
(haya ndo huwa mawazo ya chadema ambapo hulaumu ccm ilhali haiusiani kabisa na chama)
 
@MwanaCBE..hiyo kali na pole...nauli zote za DOM-DAR/DAR-DOM ni 11000-15000 Tsh..kama ulitoa hiyo,wamekuotea kaka.Next time pakia Shabib wapo poa sana.\
 
Hii ni kawaida ikifika kipindi cha kufungua au kufunga vyuo vikuu hususan udom. Wamiliki wa Mabasi hua wanafanya watakavyo na wala huna pa kushtaki hakuna sheria kaka ni fedha tu.
 
Hii ni kawaida ikifika kipindi cha kufungua au kufunga vyuo vikuu hususan udom. Wamiliki wa Mabasi hua wanafanya watakavyo na wala huna pa kushtaki hakuna sheria kaka ni fedha tu.
its true, yani sasa hivi ukutaka kuelekea sehemu yoyote yenye chuo kikuu ni balaa!
 
Nadhani pana kituo cha Polisi hapo...huo ni wizi wa mchana kweupe.
Ripoti mara moja, usilee uzembe
!

Paka lau kana ungejua kuwa polisi wanahesabu yao toka kwenye haya mabasi wala usingetoa huu ushauri. Tanzania imeoza na inapoelekea ni kwenye kunuka. Kituo cha polisi ndani ya stendi ni sehemu ya stand hiyo
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom