Ubungo mataa kumekuwa pango la wanyang’anyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubungo mataa kumekuwa pango la wanyang’anyi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mokoyo, Dec 14, 2011.

 1. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,019
  Trophy Points: 280
  UBUNGO MATAA KUMEKUWA PANGO LA WANYANG’ANYI Tarehe 12 Desemba 2011 nilichelewa kutoka katika mihangaiko ya maisha yangu mpaka kwenye saa mbili usiku. Kwakuwa mimi ni mwenyeji wa Kibaha na kesho yake tarehe 13 Desemba 2011 nilitakiwa kuwahi kwenye majukumu. Basi ilinibidi kulala kwa rafiki yangu mitaa ya Ubungo Kibangu. Wakati wa kuelekea Ubungo Kibangu nilipita mitaa ya Ubungo Mataa kunakokuwa na biashara nyingi ndogondogo. Kila mtu alikuwa bize na maisha yake wa kununua akinunua, wa kuuza akiuza, na wale waliokuwa wanapita kuelekea makwao wakifanya hivyo. Kutokana na kazi zangu kuwa za kitafiti, ghafla nilipata wazo la kufanya utafiti mdogo kuhusiana na maisha ya eneo hili. 1. Kwanza niligundua kuwa kuna dhuluma kubwa inafanywa na baadhi ya vijana “wababe” ya kutoza ushuru wafanyabiashara wadogowadogo hasa akina Mama Ntilie ambao hawana uwezo wa kutunishiana misuli. a. Katika suala la ushuru niligundua wale wababe hawalipi chochote lakini wale wanyonge kila siku wanalipa zaidi ya shilingi 2,000/=2. Pili, niligundua baadhi ya vijana wanaovizia watu wanapokuwa wamebanwa na haja ndogo na kujisaidia pembezoni mwa. Hili ndio jambo lililonidhi kuliko yote kutokana na kuwa vijana hawa “wahuni” wanajificha kwa lengo la kuvizia anayejisaidia halafu wanamtoza pesa kiasi wanachotaka waoa. Nilichogundua vijana hawa “wahuni” wanajifanya wamewekwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusimamia usafi kwa kushirikiana na kituo cha polisi cha Ubungo Terminalb. Faini ya kujisaidia ni shilingi 50,000/= ingawa ikiwa una nguvu ya mabishano na msuli wa kusimama nao hata shilingi 5,000 inakubalikac. Cha kushangaza hakuna mabango yoyote yanayoonyesha kuwa ni marufuku kujisadia maeneo hayod. Pia vijana hawa hawana mavazi yoyote rasmi ya kujitambulisha kuwa wao wana jukumu Fulani. Ni vijana waliokaa kihuni na kuvaa kaoshi chafu na ni wachafu kwa ujumla na wavuta bangi3. Jambo jingine nililogundua ni suala la wizi mdogomdogo maeneo hayo hasa unaowakumba akina dada hasa maeneo ya bonde la Songas ambapo vijana wa “kihuni na wavuta kambi” wameweka makazi yaoa. Ni eneo hatari kupita baada ya saa mbili usikuRAI YANGU KWA SERIKALI IWE MAKINI KATIKA KUWEKA TARATIBU AMBAZO ZITAFUATWA NA KILA MWANANCHI. HII NCHI INAELEKEA PABAYA HATA KAMA NI SUALA LA UGUMU WA MAISHA BASI ISIWE NDIO BAADHI YA WATU KUISHI KIJANJA NA KUDHULUMU WENGINE MALI NA UHAI WAO.
   
 2. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu hao vijana siyo machizi wengine wanatumwa na wakubwa au kushirikiana na wakubwa fulan.

  Hii serikali yetu na vyombo vya usalama ni mabwege sana kwenye mambo ya msingi kama haya badala ndiyo waelekeze nguvu huku matokeo yake hutumia garama kubwa kuwaadabisha raia wanaodai haki zao.Wakisikia maandamano ndiyo masaburi huwa washa kweli kweli kwenda kuwaadabisha.

  Mifisadi imeshindikana kuwaadabisha hata hawa vimbora wavuta bange na wanywa gongo??
   
 3. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  lile eneo ni hatari sana, sijui kwa nini hakuna askari wa kulinda usalama.
  siku moja nilishuhudia jamaa anakwapuliwa walet mfukoni, yaani waliipita kama kunguru vile,
  halafu wakakimbilia darajani, ni kitendo cha dakika 1 tu jamaa aliduwaa asijue la kufanya.
   
 4. B

  Bonge JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 868
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 80
  mtu huwezi kufikiria mwenyewe kutokukojoa hovyohovyo barabarani mpaka uwekewe bango la "usikojoe hapa" !!!!!!
   
 5. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Hilo la kujisaidia nadhani huhitaji bango kukukumbusha kwamba usijisaidie sehemu isiyo choo....
   
 6. N

  NYAGI DRY JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  kati ya maeneo hatari hapa dar ubungo darajan ni moja wapo!
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Adhabu ya kujisaidia hovyo waongeze bei iwe 100,000/=

  Vyoo vipo ndani ya kituo cha daladala, visafi vina maji ya kutosha, lakini mitaa inanuka vinyesi na mikojo.
   
 8. Wisdom

  Wisdom JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 473
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakukumbuka sana, we ndo tuikukuamata ukikojoa pale karibu na daraja pembeni kidogo ya kile ki car wash cha kizushi, MUACHE KUCHAFUA MAZINGIRA
   
 9. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwa kuwakamata wanaochafua mazingira kwa kukojoa na kujisaidia hovyo wako sahihi, ila hizo pesa wanazowatoza kama faini zinapelekwa wapi???, ingekuwa jambo jema kama zingetumika kuboresha hayo mazingira.
   
Loading...