Ubungo kura za maoni zapigwa upya; Kipi warioba CHALI KAWE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubungo kura za maoni zapigwa upya; Kipi warioba CHALI KAWE

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pdidy, Aug 4, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,572
  Likes Received: 5,760
  Trophy Points: 280
  MCHAKATO wa kuwatafuta wagombea ubunge katika majimbo manane ya Mkoa wa Dar es Salaam, umeendelea kukumbwa na vituko vya rushwa za hapa na pale na kulazimisha Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kufanya doria usiku kucha na kuwatia mbaroni wapambe 14 wa mmoja wa wagombea.

  Wakati TAKUKUTRU wakiwakamata wapambe hao 14 maofisa wa taasisi hiyo wameponea chupuchupu kupigwa na baadhi ya wapambe wa wagombea hao baada ya kuzingirwa na kundi la wapambe na kulazimika kuomba msaada wa Jeshi la Polisi.

  Matukio ya rushwa yalionekana kutawala zaidi katika Jimbo la Ubungo huku mmoja wa wagombea akitajwa kugawa fedha waziwazi na kutumia jina la Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba wana CCM wa matawi ya Makabe na Msumi A na B kutomwacha kwa madai kuwa itakuwa aibu kwa mwenyekiti huyo wa CCM kwa kuwa anamtaka.

  Majira ilishuhudia maofisa zaidi ya wanane wa TAKUKURU wa Kinondoni wakiwa na magari mawili wakizunguka maeneo ya upigaji kura tangu asubuhi hadi saa 10 jioni huku kukiwa na wasiwasi wa wapambe wa mgombea huyo kuwazunguka."Hali ni mbaya sana, hivi nchi hii imefikia hatua ya mtu asiyekuwa na fedha kutopewa uongozi hata kama anafaa?," alihoji Bi. Mary Mwaisope aliyejitambulisha kuwa kada wa CCM anayekerwa na rushwa."Leo hapa watu hawajalala, usiku kucha kulikuwa na mshikemshike wa kugawa fedha na kanga, hata sasa unaona TAKUKURU wanavyozunguka hali ni mbaya sana, angalia magari ya kifahari yanavyoleta watu hapa bila kujua wanafuata nini na wanatoka wapi," alisema.

  Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Bw. John Kabale alithibitisha kukamatwa kwa watu 14 katika eneo la Makabe na mtu mmoja kutoka eneo la Mkongeni kwa tuhuma za rushwa katika msako uliofanyika usiku wa kumkia jana."Baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa matukio ya rushwa tulijipanga na kuanza doria, tulifanikiwa kuwatia mbaroni watu 14 katika eneo la Makabe na Msumi A na B, baada ya kuona tumezungukwa sana na watu wengi nilimpigia simu RCO (Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa) wa Mkoa wa Kinondoni alitusaidia kwa haraka sana.

  Baada ya kuwahoji watuhumiwa tunaendelea kutafuta ushaidi, tukipata tutawahoji wagombea maana ni wajanja kweli wanatumia wapambe, wao wanakaa mbali."Tuliwakamata na sh. 380,000 wakiwa wanajiandaa kuanza kuwagongea wapiga kura na kuwagawiwa nyumba kwa nyumba, wengine walikimbia kwa kutumia gari namba T640 BBC na kutokomea kabisa," alisema Bw. KabaleAliwashukuru wananchi kwa ushirikiano kwa kutoa taarifa na vyombo vya habari hususan gazeti la Majira kuendelea kufuatilia kwa karibu matukio ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni na kuweka wazi kwamba tabia hiyo inapaswa kuendelea bila kukoma.

  Wakati hayo yakiendelea baadhi ya wana-CCM waliwatupia lawama viongozi wao wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni kushindwa kusimamia taratibu za kura za maoni na kuhoji uhalali wa eneo hilo la Makabe yenye wanachama zaidi ya 800 na msumi A na B kushindwa kupiga kura kwa kucheleweshewa masanduku.

  Walisema kitendo hicho ni dalili ya viongozi hao kumbeba mmoja wa wagombea anayetuhumiwa kutoa rushwa na kutumia jina la Rais Kikwete kuwarubuni wananchi kumpigia kura huku wakitishia kukihama chama hicho iwapo matokeo yatakwenda kinyume na matarajio yao.Walisema hawaoni sababu ya maeneo ya Kibamba ambayo ni mbali zaidi kufikishikiwa vifaa mapema siku ya Jumapili huku wahusika wakiruka eneo lao na kuleta vifaa saa tisa jioni, hivyo kusababisha wasitishe kazi hiyo hadi jana.

  Wana CCM hao ambao baadhi yao walikiri wazi kupewa rushwa ya fedha na kanga, walidai kwamba licha ya kupokea vitu hivyo wasingemchagua kiongozi huyo waliyemtaja kwa jina na badala yake watachukua hatua iwapo atachaguliwa kwa kuwa hafai kuwaongoza.Hata hivyo Majira ilipomtafuta mgombea aliyetajwa kugawa rushwa na wapambe wake kutiwa mbaroni na TAKUKURU hakupokea simu yake ya kiganjani hadi tunakwenda mtamboni.

  Jimbo la KinondoniMbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azzan ameshinda katika kura za maoni katika Jimbo la Kinondoni kwa kupata kura 6,192 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Bw. Mustafa Muro aliyepata kura 3,055 na kufuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji aliyepata kura 2,830.Jimbo la KaweBi. Angela Kiziga ameshinda katika kura hizo baada ya kupata kura 3,140 kwa kumshinda Kipi Warioba ambaye alipata kura 2,752.

  Jimbo la Ilala

  Kwa upande wa Jimbo la Ilala kazi hiyo pia ilikuwa kitendwawili kigumu baada ya Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya hiyo Bw. Harun Mkalimoto kuiambia Majira kwamba jana walikuwa wakiendelea kupiga kura katika matawi yote ya Kata ya Jangwani huku tawi moja la Kariakoo ukitarajiwa kumaliza mchakato huo leo.Majimarefu awa majimarefu Korogwe Mganga wa tiba za jadi, Bw. Stephen Ngonyani maarufu kama Majimarefu ameibuka kidedea baada ya kuwashinda wenzake 16 kwenye kinyang'anyiro cha Jimbo la Korogwe Vijijini kwa kura 12,441. Bw. Ngonyani ambaye kwenye kampeni zake hakuwaficha watu kuwa yeye yake ni darasa la saba, alimbwaga msomi na mchumi mwenye Shahada ya Uzamivu, Dkt. Edmund Mndolwa aliyepata kura 2, 286, huku akiwaacha midomo wazi baadhi ya watu.

  Mbunge wa jimbo hilo mwaka 2000 hadi 2005 Bw. Mussa Lupatu alishika nafasi ya tatu kwa kura 1,579 na Mbunge aliyemaliza muda wake, Injinia Laus Mhina alishikanafasi ya nne kwa kura 1,362. Baadhi ya watu waliohojiana na mwandishi wa habari hizi walisema wao sio wajinga kumchagua mtu wa darasa la saba, bali wanaelewa umuhimu wa Bw. Ngonyani hasa kwenye shughuli za kijamii. "Tumechoka na wasomi, tangu uhuru ndiyo wamekuwa wawakilishi wetu, ngoja tumpeleke mtu tunayefanana naye, lakini watu wasubiri muda sio mrefu mafanikio ya Korogwe Vijijini," alisema mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Bw. Omar, mkazi wa Kijiji cha Bwiko.

  Katika uchaguzi huo, Rais Jakaya Kikwete amepoteza Manaibu Waziri wake watatu katika mkoa wa Tanga baada ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza kudondoka. Bi. Mahiza ambaye aliwania ubunge Jimbo la Mkinga alipata kura 9,182 na kupigwa mweleka na Bw. Dustan Kitandula aliyepata 10,867. Mshindi wa tatu ni Bw. Athuman Ngenya aliyepata kura 1,666. Kama haitoshi aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Aisha Kigoda amepigwa mweleka wa aina yake baada ya Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Kilindi, Bi. Beatrice Shelukindo kupata kura zaidi ya asilimia 90 mbele ya wagombea wanane.

  Mbunge wa Handeni aliyemaliza muda wake Dkt. Abdallah Kigoda amewagaragaza wenzake tisa baada ya kupata kura 11,227, akifuatiwa na Dkt. Mohamed Mhita aliyepata kura4,318, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Bw. Simon Lupatu.Mbunge wa Mlalo aliyemaliza muda wake Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi ameshinda kwenye kinyang'anyiro kwa kupata kura 2,813 na kuwabwaga wenzanke 11 akiwemoBw. Moez Kanji aliyepata kura 2,106. Mbunge kwa miaka 15 wa jimbo hilo, Bw. Charles Kagonji alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 1,676, huku Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Bw. Rodgers Shemwelekwaakishika nafasi ya nne kwa kura 1,076.

  Pwani watakiwa kuvunja makundiKatibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo Fikirini Masokola amewataka wagombea wote ambao wameshindwa katika kura za maoni za kuwapata wagombea kwa ngazi ya ubunge katika jimbo la Chalinze mjini hapa kuvunja makundi ili kukinusuru chama katika uchaguzi ujao wa wabunge na madiwani.Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akitangaza rasmi matokeo ya kura za maoni kwa wabunge wa jimbo la Chalinze na la Bagamoyo jana kwenye makao makuu ya chama mjini Bagamoyo.

  "Kabla ya kura za maoni kulikuwa na makundi kwa wagombea na wapambe wao ambapo mara baada ya kupigwa kwa kura za maoni sasa ninawataka wagombea na wapambe waokuvunja makundi hayo na kuwa kitu kimoja, hasa kwa wale ambao hawakubahatika kuongoza kwenye kura hizo," alisema katibu huyo. Alisema kuwa wapinzani huwa wanatumia makundi kama yalivyokuwa na kuwachukuwa wanachama wetu. Katibu huyo aliongeza kuwa kutokana na tathimini ambayo ameifanya walaya ya Bagamoyo wanachama wa CUF na wa CHADEMA hawafiki hata 700, ila wakati wa kupiga kura wanapata nyingi, kitu ambacho ni cha kukitazamasana.Kwa mujibu wa matokeo hayo, Dkt. Shukuru Kawambwaamemshinda Bw. Andrew Kasambara kwa kupata kura 6,170 sawa na asilimia 86.4 dhidi ya kura 969 sawa na asilimia 13.6 za Bw. Kasambara.

  Jimbo la Chalinze ambalo lilikuwa na wagombea 10, aliyeongoza na Said Bwanamdogo aliyejizolea kura 8,083 sawa na asilimia 44.5 akifuatiwa na Bw. Iman Madega (4,240), Ramadhan Maneno (3,727) na wengine chini ya kura 400.Imeandaliwa na Yusuf Mussa, Korogwe; Edgar Nazar, Bagamoyo
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ama kweli tutajionea mengi. Hata hivyo namsifu JK kwa kuachia mambo yaende kama yalivyo bila ya kumbeba yeyote. Hii ndo demcracy,
  HApo bado watu watamlaumu JK, Sasa sijui walitaka afanyeje, na wengine wangetaamani haya mambo yafichwe kama yalivyokuwa yakifanyika. Lakini JK amekuja na transparent. Well done.
   
 3. e

  eddy JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2015
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,399
  Likes Received: 3,781
  Trophy Points: 280
  Safari hii Kipi Warioba naona kajipanga sawasawa.
   
 4. K

  Kamuche JF-Expert Member

  #4
  Aug 4, 2015
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Zilipendwa Kumbe?
   
 5. k

  kababaa1 JF-Expert Member

  #5
  Aug 4, 2015
  Joined: Jul 26, 2013
  Messages: 362
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 60
  VIP rombo mkuu
   
 6. J

  J.I.M.S1237 Member

  #6
  Aug 4, 2015
  Joined: Jul 27, 2015
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kajitahd kuacha mambo yasemwe watu wajue, waamue wakijua pumba ni ipi na mchele ni upi.
   
Loading...