Ubungo flyover: Barabara ya juu kutokea Kimara kwenda mjini pale mwisho inakoishia panahitaji marekebisho

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Ukitokea Kimara kama unapita juu kwenda mjini pale mwisho flyover inakoishia mbele kidogo kuna mtaa (traffic light). Hii taa kuna muda zinafanya kunakuwa na foleni hadi juu kule kwenye flyover kabisa. Leo asubuhi kulikuwa na foleni hadi mwanzo wa daraja lenyewe (Tanesco) hii ni kwa yanayoenda tu mjini.

Mamlaka husika tunomba kama mfanye mpango wa kutatua hili au kama kuna uwezekano magari yanayopita juu kufika pale stendi ya mkoa yanyooshe au kama kuna magari yanayotoka Kimara kama yanaenda kuingia Ubungo stendi yawe yanapita chini tu; haina haja yapite juu alafu yakifika mbele yanaenda kusimama kusubiri taa ziruhusu alafu huku nyuma yanasababiha foleni.

Ni hayo tu, asanteni.

Maendeleo hayana chama.
 
Stand itahamishwa pale baada ya ile ya mbezi kukamilika wala usiwe na shaka.

Pamoja na hayo, ujenzi bado unaendelea
 
Back
Top Bottom