Uchaguzi 2020 Ubunge yawa kama mishemishe za ajira, mkoa wa Mara watia nia 462

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,095
103,337
Screenshot_20200717-180759_Chrome.jpg


Fursa za ajira zinapotoka waombaji wanakuwa lundo sana, inaweza kutoka nafasi moja wakaomba watu 400. Ndicho kinachotokea kwenye kura za maoni kwa sasa.

Tazama Mkoa wa Mara watia nia 462. Ni kweli hawa wote wana wito na uwezo wa kutunga sheria na kusimamia serikali? Au wanasaka nini hasa.

Bado najiuliza, ila majibu ya awali yanaonyesha kwamba Bunge na nafasi ya mbunge imerahisishwa sana,imekosa hadhi iliyotukuka. Hii ni aibu kubwa kuona kila mtu anajiona anafaa kuwa mbunge. Wengine huwezi kuwafikiria hata ujumbe wa mtaa ila wamechukua fomu.

Nampongeza Rais kwa kupiga chini wale wote wenye tamaa ya madaraka.
 
Back
Top Bottom