Ubunge wa Viti maalumu na wa kuteuliwa ufutwe hauna tija yoyote

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
FB_IMG_16310283739465730.jpg



Inasikitisha sana kuona nchi masikini kama hii bado inafuja hela za umma kwa kasi ya ajabu, nchi fukara isiyojiweza Vyeo hewa vimejazana mfano hai ni wabunge wa viti maalumu na wabunge wa kuteuliwa na Rais,

hawa watu hawana tija yoyote kwa Taifa zaidi ya kupewa mishahara ya bure tu, Nchi masikini kama hii ambayo vijijini zahanati zinaendeshwa na muhudumu mmoja tu akiugua zahanati inafungwa , inashangaza kuona tumekumbatia mambo yasiyo na tija

watu sampuli ha pole pole wana nini cha maana mule bungeni?

Akina halima mdee wana tija ipi bungeni? wanamuwakilisha nani?

wabunge zaidi ya 100 bungeni wasio na majimbo wanamuwakilisha nani? hizi sio dharau kweli hizi?

zaidi ya bilioni moja kila mwezi zinapotea kwa watu wasio na kazi yyte wanalishwa bure tu, Mwanaume kama polepole ana nguvu kabisa za kujitaftia kipato why analishwa bure?

hiyo bilioni moja na zaidi inayopotea kwa kuwapa watu kama akina halima mdee wasio na majimbo wala hawamuwakilishi mtu yoyote hivi hiyo hela kwa mwezi inalipa walimu wangapi wa sayansi? situngekua tumemaliza tatizo la uhaba wa waalimu?

ndio maana CCM hawataki katiba mpya, hii nchi inapaswa kupinduliwa kijeshi tu hakuna namna
 
Kila siku tunakamuliwa kodi na tozo za ajabu ajabu ili kuwalisha watu ambao hawana tija yoyote kwetu. Hata hili Bunge sioni umuhimu wake kwa utawala huu wa CCM,ikiwa wanapitisha sheria kimazingaombwe bila kujitambua hadi zikituumiza ndiyo wanashtuka kuwa zilipitapitaje huu ni uwenda wazimu kabisa.
tatizo tunawaendekeza sana wanatuona sisi wajinga sasa ngoja
 
Naunga mkono hoja! Hizo hela kama hazina kazi bora tungegawana tu ili kila Mtanzania aambulie, hata kama ni shilingi 500! Kuliko kuwanufaisha watu wachache tu.

Au tungemkabidhi Hashim Rungwe ili awe anatuandalia pilau nyama kila wiki/mwezi! Ingependeza sana.
 
Naunga mkono hoja! Hizo hela kama hazina kazi bora tungegawana tu ili kila Mtanzania aambulie, hata kama ni shilingi 500! Kuliko kuwanufaisha watu wachache tu.

Au tungemkabidhi Hashim Rungwe ili awe anatuandalia pilau nyama kila wiki/mwezi! Ingependeza sana.
kabisa
 
Hata wa majimbo ni wengi sana. Hela nyingi zinatumika kuhudumia viongozi na sio kuletea maendeleo wananchi. Utakuta kuna jimbo la mjini na vijijini. Hapo hapo kuna madiwani na wakuu wa wilaya. Wote wanashughulikia kero hizo hizo za wananchi kwa gharama kubwa. Idadi ya wabunge wa majimbo ipungue pia.
 
Kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya! Ma DAS na Ma RAS! Hivi nao wana kazi gani? Kama hao Wakuu wa Mikoa na Wilaya, ndiyo muda wote wako busy kulinda maslahi ya ccm!!

Hii nchi ni tajiri sana iwapo serikali itakua na matumizi bora ya fedha za walipa kodi.
 
Nilifikiri hapo uliposisitiza Nchi fukara ungeunganisha na lile tukio la Dokta kumfumua Mgonjwa nyuzi....ufukara unatoa na ufahamu kisa elfu kumi tu.
 
Back
Top Bottom