Mwanapropaganda
JF-Expert Member
- Aug 19, 2014
- 4,235
- 2,501
Nimeona mwaka huu wanawake wale wasiojiheshimu na waliopoteza heshima kwenye jamii wanatangaza nia ya kugombea ubunge wa viti maalum.
Kuitwa mbunge kunaenda sambamba na kuitwa mheshimiwa, jina/cheo kinachoonekana kuwa na hadhi ya juu nchini Tanzania.
Kilichonishangaza ni kuwa watu waliojijengea picha mbaya kwenye jamii ndio wanaokimbilia kazi hiyo ya uheshimiwa! tunawezaje kuwa na waheshimiwa wasiojiheshimu?
Siku zote nidhamu ndio sifa ya kiongozi, hata mwanafunzi wa shule ya msingi anajua hivyo, ndio maana ili uweze kuwa kiranja wa shule au darasani unatakiwa kwanza uwe na sifa nzuri kama kielelezo kwa wengine, watu wajifunze kutoka kwako, Sasa hao watu wanawafundisha nini wanawake wenzao walioko kwenye jamii hasa watoto wetu wadogo?
Mtu ameshindwa kujikomboa kifikra atawezaje kukomboa wengine, mtu aliyepoteza dira ya maisha hawezi kuwapa dira ya kimaendeleo watu walio moyo wa kujituma.
Sasa hivi Tanzania siasa imekuwa rahisi ndio na kila mtu anayejiona ni maarufu anaweza kujiingiza ili kusaka fursa ya ubunge.
Katika uchaguzi mkuu ujao kutakuwa na idadi kubwa ya wanamuziki, wacheza filamu na vichekesho watakaotaka na wao kuwa wawakilishi wa nafasi ya viti vya ubunge huku wengi wa wanawake kukimbilia viti maalum.
Ni vyema vyama vya kisiasa kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata wawakilishi viti maalum ukaangalia kwanza historia ya mtu kwenye jamii yake na uwezo wake kisiasa maana hakuna nafasi ya wananchi kuwapima kama walivyo wabunge wa kugombea majimboni ambao jamii inaweza kuwakataa kupitia sanduku la kura.
Ni afadhari tu kuviondoa viti maalum au kuwapa watu wenye ulemavu kama wafugaji na wakulima watakaowakilisha sekta zinauzotegemewa kwa ustawi wa uchumi wa nchi.
Wanawake sasa wanaweza, fursa zipo sawa kwenye elimu na ajira kwanini waendelee kukomalia viti maalum? tatizo la nchi yetu kitu kikishawekwa hakitolewi hata kionekane kimepitwa na wakati.
Siasa za vyama ndio inatuletea viongozi wa serikali, wabunge ndio wanakuja kuwa mawaziri.
Watu wanaopitishwa kuwa wabunge ndio hao hao watakaotutungia sheria.
Baadae msije mkalalamika kusikia kuna wabunge wanatetea hoja ya cameroun bungeni ili kuihalalishs iwe sheria, kumbe tatizo ni ninyi wenyewe ndio mliwapeleka huko.
Tunataka wabunge wenye nidhamu, uelewa mzuri na wanaojiheshimu.