figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,486
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho kinatarajiwa kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kupinga uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki - East African Legislative Assembly(EALA), kutokana na Bunge kukataa majina yaliyowasilishwa na chama hicho kwa ajili ya nafasi mbili za Chadema za wabunge wa Afrika Mashariki kwa madai kuwa chama hicho hakikuzingatia suala la jinsia.
Kwa mujibu wa Chadema kanuni zinataka theluthi moja ya wabunge wote (9) wa jumuiya hiyo kutoka Tanzania na siyo kutoka kwa kila chama. Kesi ya msingi itataka tafsiri ya theluthi moja.
Maamuzi hayo yamefikiwa leo usiku na kikao cha wabunge wa Chadema waliokutana mjini Dodoma.
======
Mwanasheria wa CHADEMA ametolea Ufafanuzi wa Kisheria
Tundu Lissu said:Tumetangaziwa na Katibu wa Bunge kwamba kwenye uchaguzi huu wa EALA sisi CHADEMA tuna haki ya kupata nafasi 2.
Tumetangazia wanachama wetu wote wajitokeze kuchukua fomu za uteuzi. Wamechukua fomu wanachama 17, wamepigiwa kura na Kamati Kuu ya Chama wakashinda wanachama 2.
Tungewaacha walioshinda tukachukua wengine mngesemaje??? Hatufuati demokrasia, sio???
Kanuni za Uchaguzi zinaelekeza kwamba tunaweza kupeleka majina kuanzia 1 hadi 3 kwa kila nafasi. Tumepeleka majina 2 ya walioshinda. Hatujakosea kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.
Kanuni zinaelekeza kwamba theluthi 1 ya WALIOCHAGULIWA, sio WALIOGOMBEA, ni sharti wawe wanawake. Ili kupata theluthi 1 hiyo ni sharti usubiri matokeo ya uchaguzi, sio kabla. Hapa pia hatujakosea kanuni yoyote.
Kanuni zinasema pia kwamba sharti hili la jinsia litafuatwa 'KWA KAADRI INAVYOWEZEKANA.' Kwa nafasi zetu 2, sharti la kuwa na theluthi 1 ya jinsia haliwezekani. Kwa CUF sharti hilo haliwezekani pia kwa sababu wana nafasi 1. Hatujakosea chochote hapa.
MaCCM wana nafasi 6, kwao sharti la uwakilishi wa jinsia linawezakana. Ndio maana wameleta wagombea watakaokidhi sharti hilo.
Kamati ya Kanuni ilipokutana siku ya Jumamosi hakukuwa na ugomvi wowote katika uwakilishi wa jinsia. Kwa sababu vyama vyote vyenye haki vilikuwa vimetimiza masharti yote ya kanuni.
Ugomvi pekee ulioletwa kwenye Kamati ulikuwa MaCCM walitaka kulazimisha kuwapenyeza ACT kwenye uchaguzi huu wakati hawana haki ya kuwa na wagombea.
Tulipowashinda wakaleta hoja ya namna ya kuwapigia kura wagombea wetu 2 na 1 wa CUF, wakitaka wapigiwe kura za ndio au hapana.
Tukawashinda tena kwamba huo sio utaratibu wa Kanuni zetu kwani Kanuni zinasema mgombea asiye na mpinzani hapigiwi kura bali anahesabika kuwa amechaguliwa bila kupingwa.
Hawakuwa na jibu.
Jana wameleta huu ugomvi wa uwakilishi wa jinsia ambao ni wa kutengeneza kabisa.
Lengo lao kuu siku zote ni moja tu: MaCCM ndio wawe waamuzi wa nani atatuwakilisha sisi wapinzani kwenye vyombo hivi.
Ndivyo ilivyokuwa mwaka 2002 na 2007 kwa CUF na mwaka 2012 kwa CHADEMA. Na ndivyo wanavyotaka kutufanyia UKAWA mwaka huu.
Tumekataa na tutaendelea kukataa dhuluma hii hadi haki itakapopatikana.
Je, hatukuwa na wagombea wanawake waliojitokeza???
Walikuwepo wawili. Walipigiwa kura kwenye Kamati Kuu na kila mmoja wao alipata kura 0.
Tungewapitisha mngetuambiaje leo kama sio matusi kwamba ni mabibi zetu???