Ubunge Viti Maalum: Je, CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF wataapata wangapi?

gango2

JF-Expert Member
Aug 31, 2011
1,892
2,000
Habari zenu ndugu wanajamii forum:

Kwanza kabisa naomba niwape hongera|pole kwa wale wote walioshinda|kushindwa uchaguzi.

Pili naomba nije moja kwa moja kwenye maada hapo juu! Tumeona huku kwetu bara CUF wameambulia jimbo 1 na chadema wameambulia jimbo 1 huku ACT hawajapata kitu. Sasa tumekuwa tukijiuliza sana je vipi kuhusu viti maalumu hivi vyama vitatu vitapata angalau wabunge??

Binafsi ninafanya reference ya kilichofanyika mwaka 2015 so naomba mwenye uelewa zaidi atatujuza.

Kwa mujibu wa mwaka 2015 uteuzi ulihusisha vyama angalau vilivyopata 5% ya kura zote halali za wabunge kama matakwa ya katiba yanavyotaka. kwa hivyo kunauwezekano vyama vitavyopata angalau 5% ya kura halali za ubunge ndivyo vitavyohusika.

Sasa uteuzi unafanyika vipi?
Inachukuliwa idadi ya kura halali za wabunge za chama husika inagawanywa na jumla ya kura zote halali za wabunge wa vyama hivi jibu linazidishwa na idadi ya wabunge wa viti maalumu wanaohitajika (kwa mujibu ya tovuti ya bunge ni 102, ingawa mwaka 2015 walikuwa 113)

Kwa kufanya reference hii, nafikiri chadema bado wananafasi ya kuwa na wabunge zaidi ya 15 bungeni kwani wanakura nyingi halali za wabunge.

Baada ya kupata idadi ya wabunge kwa kila chamaTume hufanya uteuzi kwa kufuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na Katibu wa Chama husika.

(Naomba kama kama nitakuwa nimekosea au kuna mtu anajua zaidi anaweza kutujuza)
 
Alvin Slain

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
6,381
2,000
Vyama vya CHADEMA na Act hawatambui uchaguzi uliompaka Maguful madaraka, Hivyo kwa sasa hatutambui uchaguzi kufanyika 28 oct2020.
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,424
2,000
Habari zenu ndugu wanajamii forum:

Kwanza kabisa naomba niwape hongera|pole kwa wale wote walioshinda|kushindwa uchaguzi.

Pili naomba nije moja kwa moja kwenye maada hapo juu! Tumeona huku kwetu bara CUF wameambulia jimbo 1 na chadema wameambulia jimbo 1 huku ACT hawajapata kitu. Sasa tumekuwa tukijiuliza sana je vipi kuhusu viti maalumu hivi vyama vitatu vitapata angalau wabunge??

Binafsi ninafanya reference ya kilichofanyika mwaka 2015 so naomba mwenye uelewa zaidi atatujuza.

Kwa mujibu wa mwaka 2015 uteuzi ulihusisha vyama angalau vilivyopata 5% ya kura zote halali za wabunge kama matakwa ya katiba yanavyotaka. kwa hivyo kunauwezekano vyama vitavyopata angalau 5% ya kura halali za ubunge ndivyo vitavyohusika.

Sasa uteuzi unafanyika vipi?

Inachukuliwa idadi ya kura halali za wabunge za chama husika inagawanywa na jumla ya kura zote halali za wabunge wa vyama hivi jibu linazidishwa na idadi ya wabunge wa viti maalumu wanaohitajika (kwa mujibu ya tovuti ya bunge ni 102, ingawa mwaka 2015 walikuwa 113)

Kwa kufanya reference hii, nafikiri chadema bado wananafasi ya kuwa na wabunge zaidi ya 15 bungeni kwani wanakura nyingi halali za wabunge.

Baada ya kupata idadi ya wabunge kwa kila chamaTume hufanya uteuzi kwa kufuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na Katibu wa Chama husika.

(Naomba kama kama nitakuwa nimekosea au kuna mtu anajua zaidi anaweza kutujuza)

Mpaka sasa hivi msimamo uko hivi

Viti vya Ubunge vilivyogombewa 264
CUF wabunge 3
ACT wabunge 4
CHADEMA mbunge 1
CCM wabunge 256

Haya tusubirie sasa viti maalum
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom