Ubunge Tanzania ni ulaji tu hakuna faida kwa nchi

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Watanzania tunadanganya na wabunge kwa kujifanya kama vile wanatusaidia. Bunge kwa mfumo wa sasa ndiyo sehemu ya matumizi bila faida yeyote kwa taifa

1. Kwanza Budget ambazo wanatumia muda kujadili na kuchukua pesa nyingi serikali kwenye utekelezaji hawatumii pesa kama walivyopanga. Hivyo wanapiga kelele bungeni kuombea agenda zao lakini hakuna kinacho amuliwa kutokana na mijadala. Zaidi ya miaka mitano sasa budget ni asilimia chini ya 35% ya pesa inatolewa kutokana na budget. Sasa mijadala na upotevu pesa wa nini kama serikali haifuati budget na mapendekezo

2. Hawana maamuzi yeyote kwenye majimbo yao, maamuzi ya kodi ni ya serikali na sio wabunge na hata meya ana nguvu kuliko mbunge kwenye matumizi ya pesa

Bunge lingetakiwa kuwa dogo na matumizi kupunguzwa kama tumeamua kutokuwasikiliza badala ya kupoteza pesa za wananchi. Nashangaa wamaotumia pesa kujifanya wataka kusaidia watu kwamba mtu wa chama fulani atabadilisha sehemu. Kama serikali haifuati budget ya Bunge mbunge unaleta vipi maendeleo kama sio kudanganyana. Hakuna utapeli mkubwa Watanzania tunafanyiwa kama ubunge.

Kama mapendekezo na budget za bunge hazifuatwi tusishangae wale wabunge wa zamani kama Mkono walikuwa hawaongei maana walikuwepo kulinda tu biashara zao. Walijua mawazo yao ni bure tu. Ubunge ni ulaji mkubwa kama wewe unataka kusaidia nchi fanya biashara, anzisha NGO, somesha watu, saidia hospitali n.k
 
Write your reply...wakuu wa mikoa wangetosha kufanya kazi za wabunge kwani hakuna haja ya wawakilishi rais anatosha kwani ndiye last say
 
Napendekeza wakuu wa mikoa na wilaya watosha kabisa,na wanachapa kazi sana bora wao wangekuwa wanapata pesa nyingi kuliko hawa wabunge, haiji kwenye akili yangu bunge linatumia pesa nyingi, pesa ambayo serikal ingefanyia maendeleo ya nchi.ki ukwel mm pia sioni hao wanaojiita wabunge Kama wanamchango mkubwa, anayefanya kazi Ni serkali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukikaa ukafikiri bila kuingiza ukada,ulichoongea kina ukweli mkubwa Sana,ndio maana wengine wanalia bungeni si ajili ya wananchi bali kwa ajili ya matumbo yao.
 
Mpaka mtu analia bungeni basi ujue kuna ulaji mkubwa Magufuli nakuomba uvunje katiba ufute uchaguzi mkuu mpaka 2025 maana wabunge wamekuangusha ...wamekaa kukusifu wakati hiyo kazi inaweza fanywa nawatu kama Makonda yakukusifu Uongo
 
huo ndo ukweli,hakuna cha maana pale. ndo maana hata jiwe kawadharau. wengine wananunuliwa kama mboga
 
Back
Top Bottom