Ubunge ni chamtoto issue ni je? Upo kamati gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubunge ni chamtoto issue ni je? Upo kamati gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjenda Chilo, Jun 5, 2012.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Wanabodi hebu tuchangie hili. Inasemekana mshahara wa ubunge plus mfuko wa jimbo si kitu, mihela mingi inapatikana kwenye hizi kamati wanazoziunda. Inawezekana japo bado hukumu hili la mbunge wa Bahi kuomba rushwa limechelewa sana.

  Naambiwa wabunge wengi wamekuwa wakijipatia mamilioni kwa njia hii either kwa kuweka mazingira au kwa kuwekewa mazingira ili kulainisha uungwaji mkono wa bajeti za taasisi za umma.

  Moja ya vilainishi vinavyowanasa waheshimiwa ni kuandaliwa ziara nje zisizo na manufaa yeyote huku wataalam wakinyimwa fedha za kwenda kuongeza ujuzi huko ng'ambo. Ukitaka kuamini angalia ni wabunge wangapi wanakosa ziara za ng'ambo baada ya kumaliza vikao vyao pale dodoma.

  Tumekuwa tukimlaumu JK na safari zake lkn bora yeye anaenda kutembeza bakuli kuliko kumpa ziara mbunge wa darasa la saba na kutumia mamilioni kwenda kujifunza kitu ambacho hatakielewa. Hii ofisi ya bunge ikiweka matumizi yake hadharani tunaweza kuzimia. Naona ni kama vile nani kumfunga paka kengele?

  Watz tunaumizana sana jamani, inamaana watu wameshindwa kutafuta na kuvumbua biashara inayolipa zaidi ya siasa? wachumia tumbo taratibu jamani mnatuumiza.
   
 2. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  100% Tawileeeeeeeeeeee
   
 3. U

  Utatu JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  UKWELI MTUPU!

  Kwa idadi tu ya wabunge wanaozurura huko ng'ambo. Njaa na akili hafifu zinatuumiza na zitatuumiza kwa muda mrefu sana. Ila wao watasema hawajavunja sheria - kama ile issue ya Uingereza na madai ya wabunge wao, ambao wengine lakini waliishia jela.

  Kwani hayo mahesabu ya bunge si yanatakiwa yawe wazi? Per diem zikoje? Yanakaguliwa na nani?

  Kila mwenye nia njema aamke. Tena haraka, tulipigie kelele hili suala.
   
 4. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Ni kweli mkuu. hapa kuna issue ya kukamatana mkomba mboga kati ya bunge na serikali, ila ukweli ni kupigania ili huo ugali na mboga tule wote. Yani sisi, wao na wale kwa pamoja
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mhe. Augustino Lyatonga Mrema kaondoka juzi usiku kwenda UK ziara ya kikazi
   
Loading...