OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,191
- 103,713
Abdulazizi Abood (CCM) amepitishwa kama mgombea pekee katika Jimbo hilo baada ya wagombea wa upinzani kukatwa kwasababu ya makosa yaliyobainika kwenye ujazaji wa fomu
Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Morogoro mjini amewafutilia mbali wagombea wote wa vyama vya upinzani akiwemo Devotha Minja wa CHADEMA na kumbakiza Abdulaziz Abood wa CCM kuwa mgombea pekee, kwa madai kuwa wagombea wa upinzani walikosea kujaza fomu.
Tayari Msimamizi huyo amemtangaza Abood kupita bila kupingwa. Hii ina maana kuwa hatafanya kampeni wala kupigiwa kura bali atasubiri kuapishwa tu.
Wagombea waliokatwa ni wa CHADEMA, ACT Wazalendo, CUF na CHAUMA. Hata hivyo CHADEMA wamesema watakata rufaa kupinga maamuzi hayo.!