UBUNGE: Dili ya kibiashara, au mwito wa kuhudumia wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UBUNGE: Dili ya kibiashara, au mwito wa kuhudumia wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bongolander, Feb 22, 2010.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Wakuu tunapoelekea 2010, kuna kauli ambazo naomba mzifuatilie sana.

  1. Nimeombwa na wazee, na wananchi wa jimbo fulani nigombee.
  2. Baada ya kushauriana na watu fulani nikashawishika kuchukua fomu
  3. Baada ya kuona mbunge aliyepo hajafanya lolote nimeamua kuchukua fomu.
  4....
  5...

  Hawa jamaa wanaojitokeza bila sisi wenyewe kufahamu wanakotoka, wana lengo kweli la kutuoigania? wanalengo kweli la kutusadia au ndio kupigania tu, kiinua mgongo and a like. Wanaweza kujitokeza kweli kama tukisema wabunge hawatalipwa mshahara, wagombee kutokana na uzalendo?
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  PESONAL INTERESTS and wealth lust is a driving force in their damn move!
  Hawana jipya hawa!
  Aibu mchana kweupe!
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Bongolander,

  Kitu chochote anachofanya mwanadamu kunakuwa na interests zake binafsi. Mtu unapogombea siasa au unapoomba kazi fulani kunakuwa na interests za aina fulani upande wako.

  Mimi ningekushauri usome Maslow's hierarchy of needs na anatoa majibu ya swali lako.

  Hizo needs za mwanadamu ndio zinatofautiana kuanzia zile needs za kutaka kula tu na kushiba mpaka zile za kujivunia kuona umefanikisha jambo fulani katika jamii.

  Kinachotakiwa mahali popote ni balance nzuri kati ya your own needs na needs za jamii unayotaka kuitumikia. Kama ni kazini basi balance kati ya your own interesrs/needs na zile za mwajiri wako.

  Hata motives za watu kuamua kufanya jambo fulani zinatofautiana sana lakini kisichopingika ni kwamba katika kila jambo analofanya mwanadamu kunakuwa na motive ya aina fulani mbele yake. Kitu kigumu ni kujua kama huyo mtu kweli yuko motivated na kusaidia jamii au kuna mambo mengine ya siri yaliyojificha nyuma yake.

  Ndio maana elimu kwa raia ni muhimu sana ili waweze kutofautisha wasanii wa kisiasa na wale watu ambao kweli wako motivated na kusaidia jamii wanayotaka kuitumikia.
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,753
  Trophy Points: 280
  Mkuu mtanzania,

  Hapo umemaliza. Kwanza kabisa mbunge anayetaka kugombea bila yeye mwenyewe kuwa na maslahi hafai.Lazima awe na maslahi ila maslahi yasiathiri ustawi wa jamii inayomzunguka au uwakilishi wa jamii inayomzunguka
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapa umenena, lakini kinasikitisha sana kuona wanatumiwa wengine. Hizo kauli za kusema nimeombwa, nimetumwa, nimesukumwa ni uongo tu. As we move closer towards 2010 utasikia kauli nyingi sana za namna hiyo. Nilipoanzisha thread hii sikuwa na uhakika kama watu watatumia cheap politics ya namna hii, sasa hivi naona baadhi ya watu tayari wameanza kusema wameombwa, wamesukumwa, wanahitajiwa kugombea...lakini kama ulivyosema wanaoneana zaidi wana personal interest na wanatumia wengine kama madaraja tu.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,699
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Money money pessaaaa, moneyeeeee eeee... Wimbo huo. Asante
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 35,996
  Likes Received: 6,820
  Trophy Points: 280
  nenda MAKUMIRA kamtumike BWANA WA MAJESHI YESU KRISTO
   
 8. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 573
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Inasemakana zaidi ya 40% ya wakuu wa wilaya wana nia ya kugombea ubunge maeneo tofauti ya Tanzania! wakuu wa mikoa ya zaidi ya kumi nao hali kadhalika!Mawaziri wote hilo halina mjadala!Imekuwa ajira !na uu utaratibu wa kutenganisha biashara na siasa ukishakuwepo wasiyo kuwa na ajira wataomba ajira ya ubunge!
  Mie kwa mtazamo wangu wengi wa wanaotaka ubunge ni kwa maslahi yao binafsi kuliko kwa wananchi!
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni vyote,wapo ki dili kwa ticketi ya kukutetea.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Mar 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Yote mawili yanawezekana
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Inategema na tabia ya mtu kwa CCM ni biashara kwanza wito baadae, kwa upinzania wito, kutumikia wananchi na biashara ya mwisho, Inategemea mtu, CHAMA, Malengo na Tabia binafsi, Katiba , na muda
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mkuu labda siio fair kuwanyooshea vidole wabunge wa CCM, naona wabunge ni wabunge tu bila kujali vyama vyao. Lakini point yako inaeleweka vizuri, yaani wao cha kwanza ni maslahi binafsi.

  Kama maslahi binafsi ni kwanza lini wanakuwa wameridhika na kuanza kuwaridhisha wengine? Inaonekana kuna wengine hawaridhiki wanaendelea na kuendelea kugombea ubunge wananeemeka na kuneemeka, lakini majimbo yao yako katika hali ile ile aliyoiacha mkoloni, au mbaya kuliko hata ya aliyoiacha mkoloni.
   
 13. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ubunge ni deal la kibiashara
   
 14. j

  jojig Member

  #14
  Mar 7, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni personal interests ndo always zinawasukumu kwenye ubunge.nothing else uchungu sidhani kama upo na kama upo ni kwa wachache sana.kwa nini wengine huwa mwanzo wa bunge la kwanza mpaka la mwisho huwa hawachangii hata kitu kimoja achilia mbali kutembelea wananchi wao kwenye majimbo? Pia ni kwa nini huwa wanalala kwa waganga wa kienyeji wakati wa uchaguzi?? mimi naamini kabisa ni personal interests japo kuna wenye kuitumia vizuri hii chance here i mean mtu kama mo dewji ni mbunge mfano kwa wote kwa sababu anasaidia sana kule singida japo hata yeye im sure in one way or another kuna njia ananufaika ikizingatiwa kuwa huyu ni entrepreneur mkubwa sana nchini.
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mkuu kama kuna win-win situation nadhani tungekuwa mbali sana. Lakini kilichopo ni kwamba we are being used, and the situation is vote, lose and let him win. Hakuna ubaya wa kuwa na mbunge anterprenuer as long as he deliver the goods.

  Ukiangalia wabunge wengi sana wakiingia ubunge wanatajirika sana, na constituents wanaendelea kuwa hoi, sana sana wananufaika pale uchaguzi unapokaribia. Na hata wabunge wanaosemwa kuwa wanasaidia majimboni kwao, ni kuwapa kilo moja ya sukari, kanga, simu za mkononi au suti na vitu vingine vidogo vidogo, kitu ambacho binafsi sioni kama ni kusaidia.
  By the way mbunge kuwasaidia constituents kwa hela zake za mfukoni kunatia shaka sana, hasa ukzingatia kuwa kila anayewezeka anataka return. NI afhadahri atumie fedha za serikali kuleta maendeleo kwa constituents.
   
 16. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Personal interest and lust for wealth is the driving force for any human being. Even you must due what you do for some personal interest. Au kuna mtu anapenda umaskini mkuu?

  The problem is that being an MP has too many perks that people see it as a source to gain wealth. If you want to get rid of the problem of wealth seeking individuals then simple solution si to reduce the perks. Mtu analipwa mamilioni kwa mwezi aache kutaka ubunge? Lets be for real they are humans and greed is human nature.

  That is why in Nyerere's time there were more patriotic leaders because there was less for them to gain personally. In that case only people trully committed to serving the people would seek the positions. If today being an MP meant earning mere wages then most people would seek employment in the public sector where now people are earning big money.
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Lyatonga Mrema kisha sema kuwa UBUNGE ndio dili, maana yake ni kuwa Ubunge katika nyanja za uwekezaji ndio unalipa!! Mtu yeyote anayewekeza katika shuhuri isiyo lipa ni punguani; kwahiyo mtu yeyote kwa mazingira yetu anayetaka kugombea Ubunge ajue kuwa ni biashara na kama ni biashara lazima awe na mtaji wa kutosha. Mfumo wa sasa wa kuchagua viongozi unawapa nafasi wale tu wenye uwezo wa fedha hata kamma dhamila yao sio kuwatetea wananchi katika shida zao za kijamii!!
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,971
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 0
  Kama ubunge kuhudumia wanachi waambie wagombee udiwani uone??au waambie wabunge wanaonaje wabadilishe sheria sifa ya MBUNGE ni lazima awe amekuwa DIWANI.

  Yes kama ni kusaidia wananchi katika level ya udiwani ndio wanachi walipo.

  hahhahah
   
 19. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii ni suggestion nzuri sana, kuna haja ya kuiasilisha kwenye masharti ya kugombea ubunge. Nadhani itakuwa vizuri sana kuwa na masharti kama hayo, haiwezekani mtu from no where anaingia kwenye siasa, eti kisa hela inamruhusu. Na kauli zao za ajabu sana...

  ....watu wameniomba nigombee, wazee wamenishauri, wanajimbo wamenisukuma, kutokana na shida za wananchi nimeshawishika....fix tupu. Lengo kubwa kwao ni kuchuma pesa tu.

  Mtu anaishi wilaya ya Temeke kwa miaka karibu yote na anakumbana na shida za temeke kwa miaka karibu yote ahalfu anasema anaenda kuwasaidia kujiendeleza watu wa Kapalamsenga, wapi na wapi? uzito wa mtungi aujuae ni kata. Inabidi tuanze kuwawekea no hawa watu.
   
 20. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mtanzania umeongea vizuri kuwa kila mtu ana interests zake lakini kwa swala la ubunge sidhani kama suala la personal interests linapewa uzito zaidi hasa upande wa kuisaidia jamii
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...