Mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika hivi karibuni yamenifanya niwe na maswali hasa baada ya Dr. Shein kuanza kuteua wateule wake.
Juzi aliteua wajumbe 8 wa Baraza la Wawakilishi kama Katiba ya Zanzibar inavyomtaka. Mmoja wa wateule hao ni Balozi Seif Ali Idd. Huyu mteule kwa bahati nzuri alikuwa tayari ni Mbunge Mteule/mchaguliwa wa Jimbo la Kitope Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Jana Dr. Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa SMZ. Mpaka hapo tayari huyu Mzee ana post 3. Mara nyingi vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano na Vikao vya Baraza la Wawakilishi huwa vinafanyika kwa karibu wakati mmoja, je huyu Mzee atawawakilisha wananchi wake wa Kitope au ataenda kuhudhuria vikao vya Baraza ili kumwakilisha Rais?
Kimuundo [correct me if I am wrong], Kiongozi wa serikali kwenye Baraza la Wawakilishi ni Waziri Kiongozi, je, protokali hapa inakaaje maana Makamu wa Pili wa Rais nae ni mmoja wa wajumbe wa baraza la wawakilishi. Who is senior wanapokuwa huko ndani ya vikao vya Baraza la Wawakilishi?