Ubunge Afrika Mashariki: Majina ya wagombea wa CHADEMA na CUF yakataliwa na msimamizi wa uchaguzi

PRODA LTD

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
1,005
1,333
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI


IMETOLEWA NA:
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI
S.L.P 941
DODOMA

3 APRILI, 2017

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA

TAARIFA KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA WA UJUMBE WA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

1. Tarehe 17 Machi, 2017 nilitoa Tangazo kwenye Gazeti la Serikali Namba 376 kuhusu Siku ya uteuzi na Siku ya Uchaguzi. Katika Tangazo hilo, nilipanga Siku ya tarehe 30 Machi, 2017, saa Kumi (10.00) Jioni kuwa Siku ya Uteuzi wa Wagombea na pia siku ya tarehe 04 Aprili, 2017 saa Tano (5.00) Asubuhi kuwa Siku ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki.

2. Aidha, natoa shukrani zangu za dhati kwa wadau wote hususan Vyama vyote vya siasa nchini kwa ushirikiano mzuri nilioupata kutoka kwao katika zoezi zima la mchakato wa uteuzi wa wagombea.

3. Vile vile, navipongeza na kuvishukuru vyama vyote vya siasa vyenye haki ya kushiriki uchaguzi kwa kuendesha mchakato wa uteuzi wa wagombea kwa uwazi na demokrasia kubwa.

4. Pia navishukuru vyombo vya habari na wanahabari wote kwa ujumla kwa kuhabarisha umma kuhusu mchakato huu muhimu kwa Bunge na Taifa kwa ujumla.

5. Kipekee nawashukuru na kuwapongeza wananchi wote waliojitokeza kupitia vyama vyao kugombea katika uchaguzi huu ambapo jumla ya Watu 505 walijitokeza kugombea kupitia vyama vifuatavyo:

A. CCM- Wagombea - 471;

B. CHADEMA- Wagombea - 17;

C. CUF-Wagombea - 8;

D. NCCR-MAGEUZI - Wagombea 3; na

E. ACT-WAZALENDO - Wagombea-6.

6. Wagombea hao walichujwa na Vyama vyao na kupata majina ya watu 20 waliopitishwa kugombea kwa mchanganuo ufuatao:

A. CCM-Wagombea 12;

B. CHADEMA-Wagombea 2;

C. CUF-Wagombea-4;

D. NCCR-MAGEUZI-Mgombea 1; na

E. ACT-WAZALENDO-Mgombea 1.

7. Kati ya Wagombea hao Wanaume ni 12 na Wanawake ni 8 kwa Mchanganuo ufuatao:

A. CCM-Wanawake 6 na Wanaume 6;

B. CHADEMA- Wanawake na Wanaume 2;

C. CUF-Mwanamke 1 na Wanaume 3;

D. NCCR-MAGEUZI-Mwanamke 1 na Wanaume 0; na

E. ACT-WAZALENDO-Wanawake 0 na Mwanaume 1.

8. Majina hayo ya Wagombea yaliwasilishwa na Vyama vyao kwangu tarehe 30 Machi, 2017 kabla ya Saa 10 Jioni kama masharti ya Kanuni ya 5(4) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.

9. Baada ya hatua hiyo, nilifanya uchambuzi wa Nyaraka zilizowasilishwa ili kujiridhisha na uzingatiwaji wa masharti ya uteuzi wa Wagombea kwa mujibu Ibara ya 50 ya Mkataba, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 Sheria ya Uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki na Kanuni 5(1), (2) na (3) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016. Ufuatao ni Mchanganuo wa maombi ya kugombea katika Makundi ya Uchaguzi:

KUNDI A: WANAWAKE

1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM

2. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM

KUNDI B: ZANZIBAR

1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME ME CCM

2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA KE CCM

3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH ME CCM

4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI KE CCM4

KUNDI C: VYAMA VYA UPINZANI

1. Ndg. Ezekia Dibogo WENJE - ME - CHADEMA

2. Ndg. Habibu Mohamed MNYAA - ME - CUF

3. Ndg. Lawrence Kego MASHA - ME - CHADEMA

4. Ndg. Nderakindo Perpetua KESSY - KE - NCCR

5. Prof. Kitila MKUMBO - ME - ACT

6. Ndg. Sonia Jumaa MAGOGO - KE - CUF

7. Ndg. Thomas D.C MALIMA - ME - CUF

8. Ndg. Twaha Issa TASLIMA - ME - CUF

KUNDI D: TANZANIA BARA

1.Ndg. Adam Omai KIMBISA - ME - CCM

2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM

3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM

4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM

5. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM

6. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM

10. Matokeo ya uchambuzi wa nyaraka za uteuzi wa Wagombea zilizowasilishwa na Chama cha Mapinduzi yanaonesha kuwa wagombea wote wamekidhi vigezo na masharti ya uchaguzi. Ifuatayo ni orodha ya Wagombea hao katika makundi waliyoomba kugombea:

I. WAGOMBEA WALIOKIDHI MASHARTI NA KUTEULIWA

KUNDI A: WANAWAKE

1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM

2. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM

KUNDI B: ZANZIBAR

1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME - ME - CCM

2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA - KE - CCM

3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH - ME - CCM

4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI - KE - CCM

KUNDI D: TANZANIA BARA

1. Ndg. Adam Omari KIMBISA - ME - CCM

2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM

3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM

4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM

5. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM

6. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM

II. UTEUZI WA WAGOMBEA KATIKA KUNDI C -VYAMA VYA UPINZANI

11. Uteuzi wa Wagombea katika Kundi C (Vyama vya Upinzani) haujafanyika kutokana na mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwenye nyaraka za uteuzi wa wagombea ambayo yanakiuka masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki ya Mwaka 2011 iliyotungwa na Bunge la Afrika Mashariki. Muhtasari wa mapungufu yaliyobainishwa kwa Vyama husika ni kama ifuatavyo:

1. CHADEMA

Uteuzi haujazingatia jinsia ili kuwezesha utekelezaji wa masharti ya Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (The East African Legislative Assembly Elections Act, 2011) ya angalua theluthi moja (1/3) ya wajumbe 9 ioneshe uwepo wa jinsia zote mbili (at least one third of the elected members shall reflect either gender).

Fomu za maombi ya wagombea hazipo.

Orodha ya waombaji haipo.

Fomu ya matokeo ya kura haipo.

2. CUF

Uteuzi haujazingatia jinsia ili kuwezesha utekelezaji wa masharti ya Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya a Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (The East African Legislative Assembly Elections Act, 2011) ya angalua theluthi moja (1/3) ya wajumbe 9 ioneshe uwepo wa jinsia zote mbili (at least one third of the elected members shall reflect either gender).

Fomu za Uteuzi wa Wagombea zimewasilishwa na mamlaka mbili tofauti.

Wagombea wawili hawana uthibitisho wa Uraia.

Fomu ya uthibitisho wa hiari ya kugombea haipo kwa wagombea wote.

Orodha ya waombaji haipo kwa Mgombea mmoja.

Fomu ya matokeo ya kura kwa wagombea wote haipo.

Fomu ya Mahudhurio kwa mgombea mmoja haipo.

12. Mapungufu hayo yamenifanya nishindwe kufanya uteuzi wa Wagombea katika kundi hilo, hivyo nimeviandikia barua vyama vyenye haki ya kugombea katika Kundi hilo kuvitaka kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa na kuwasilisha majina na nyaraka zinazohitajika ofisini kwangu Dodoma Siku ya tarehe 4 Aprili, 2017 kabla ya saa 7:00 Mchana.

13. Uteuzi wa Wagombea katika KUNDI C (Vyama vya Upinzani) utafanyika tarehe 4 Aprili, 2017 wakati wowote kuanzia saa saba kamili (7:00) mchana mara baada ya kupokea na kuchambua nyaraka zitakazowasilishwa kwangu na Vyama husika.

14. Kutokana na matokeo ya uchambuzi huo na kwa kuzingatia masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Masharti ya Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki, Kanuni ya 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge na Kanuni ya 5(1)(2) na (3) ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 na Mwongozo wa Spika kuhusu Mgawanyo wa Kura zinazotakiwa kupigwa katika kila Kundi, kwa mamlaka niliyopewa kama Msimamizi wa Uchaguzi NATANGAZA na kutoa TAARIFA kwa Umma kwamba, wafuatao ndio waliokidhi vigezo na masharti ya kuteuliwa kugombea Uchaguzi wa Wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki uliopangwa kufanyika tarehe 4 Aprili, 2017 kwa mchanganuo ufuatao:

KUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE

1. Ndg. Happiness Elias LUGIKO - KE - CCM

2. Ndg. Zainabu Rashidi Mfaume KAWAWA - KE - CCM

KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR

1. Ndg. Abdullah Hasnu MAKAME - ME - CCM

2. Ndg. Maryam Ussi YAHYA - KE - CCM

3. Ndg. Mohamed Yusuf NUH - ME - CCM

4. Ndg. Rabia Hamid MOHAMEDI - KE - CCM

KUNDI D: WAGOMBEA WA TANZANIA BARA

1. Ndg. Adam Omari KIMBISA - ME - CCM

2. Ndg. Anamringi Issay MACHA - ME - CCM

3. Ndg. Charles Makongoro NYERERE - ME - CCM

4. Dkt. Ngwaru Jumanne MAGHEMBE - ME - CCM

5. Ndg. Fancy Haji NKUHI - KE - CCM

6. Ndg. Happiness Ngoti MGALULA - KE - CCM

Dr. Thomas D. Kashililah

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI

3 Aprili, 2017
 

Attachments

  • 1491214876-UCHAGUZI WA EALA.pdf
    186 KB · Views: 135
Vyama vingine vinatakiwa kufanya marekebisho au havitashiriki
Kwani Zenj mbona siku zinasonga? Nani ana imani na viongozi wawe wa bunge au Serikali? Turudi chama kimoja tuu kieleweke basi.
 
Hii ni aibu kubwa sana Kwa vyama vya Chadema na Cuf huu unguli wa wabasheria upo kwenye kesi za uchochezi tu. Chama kinashindwa kabisa Kuwa organized kiasi hiki weledi na uwezo wao upo wapi? Hivi hawa watu wangepewa nchi mambo madogo kama haya wanashindwa au kwakuwa walikuwa na majina mfukoni very very shameful. Na hili wapiga makofi na wasiojielewa wanaweza kuona ni jambo dogo lakini ccm limewapa milage kubwa mno.
 
Kila siku LISSU anajua sheria sasa hata hili dogo ameshindwa kukisaidia CHAMA???au kwa sababu RUZUKU hakuna kwenye hili au kwa sababu MBOWE alikuja na majina yake mfukoni????aibu tupu
Ila kwenye hili siwezi mlaumu LISSU ni ubabe wa kaka MBOWE as usual
Sasa itabidi WENJE amuachie SEPETU.......au WENJE amuachie MASHA maana MASHA alimuachia LISSU TLS....patamu hapo......
 
Kumbe wamepewa muda kurekebisha mapungufu!! Kichwa cha habari bwana!
 
Mbona jambo dogo tu litarekebishwa na kutolewa ufafanuzi kelele nyiiingiii.
 
CHADEMA
form ya maombi ya uchaguzi haipo

form inayonesha waombaji haipo ( Hana alingia nayo yeye mawili tu)

form inayonesha matokeo ya kura haipo (Itakuwepo vipi wakat mbowe kawaptisha yeye wawil)

Chama cha jamiiforums,Istagram,facebook, chama xha Tundu na mbowe hawatambui hata sheria duuh Aibu sana.

Wagombea wamepitishwa kiubabe na mwenyekiti cha kudumu bwana Mbowe
 
Back
Top Bottom