• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Elections 2010 Ubunge 2010: Mrema, Mbatia na Suzan Lyimo kupambana ktk Jimbo la Vunjo?

Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,596
Points
2,000
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,596 2,000
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema ambaye ameombwa kugombea ubunge Jimbo la Vunjo lililopo mkoani Kilimanjaro mwaka 2010 amekubali kugombea nafasi hiyo ikiwa atatakiwa hivyo na Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumwandikia barua Mrema ya kumtaka kugombea jimbo hilo, aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo hilo kati ya mwaka 2000 na 2005, Jesse Makundi alisema kuwa ameandika barua hiyo Februari 8 mwaka huu na kuikabidhi jana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, John Komba ili amkabidhi Mrema.

Alisema lengo la kumwomba kugombea nafasi hiyo, ni kutokana na mgawanyiko wa vyama vya upinzani ambao wameshajipanga kugombea jimbo hilo hali inayoonekana itaifanya CCM kupata ushindi jimboni humo.

Tayari Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia ameshatangaza kugombea jimbo hilo na kwa mujibu wa Makundi, Mbunge wa Viti Maalumu wa Chadema, Susan Lyimo atagombea jimbo hilo mwaka 2010.

Kwa upande wake, Mrema aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu akiwa mkoani Kilimanjaro kuwa yupo tayari kugombea nafasi hiyo ikiwa atapitishwa na Mkutano Mkuu wa Chama chake.

"Hilo jambo kubwa inabidi Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu waangalie hali ya siasa nchini na baadaye Mkutano Mkuu utatoa uamuzi kama nigombee au nisigombee nafasi hiyo, mimi nitatekeleza maamuzi ya Mkutano Mkuu" alisema Mrema.

Akitoa sababu za kumtaka Mrema agombee nafasi hiyo, Makundi alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuona katika jimbo hilo anahitajika mtu mwenye nguvu kisiasa ambaye ni tishio kwa CCM na mpambanaji asiyekata tamaa.

Mrema atakuwa Mwenyekiti wa nne kugombea nafasi ya ubunge. Tayari Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameshatangaza kugombea Jimbo la Hai, Mbatia atagombea Vunjo na kwa sasa Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo ni Mbunge wa Bariadi Mashariki.


Source: HabariLeo
 
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined
Jan 18, 2007
Messages
14,596
Points
2,000
Ben Saanane

Ben Saanane

Verified Member
Joined Jan 18, 2007
14,596 2,000
sorry wakuu,
source ni gazeti la habari leo
 
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Messages
4,234
Points
0
Yona F. Maro

Yona F. Maro

R I P
Joined Nov 2, 2006
4,234 0
Hao wakubali democrasia ichukuwe mkondo wao kwa wao kuamua kuachia vijana nafasi hizo wenye mawazo mapya wao wawe kama washauri tu katika vyama vyao na serikali kwa ujumla sasa kama wao wanataka ubunge nani atajenga chama ??
 

Forum statistics

Threads 1,405,396
Members 531,983
Posts 34,485,175
Top