Uchaguzi 2020 Ubovu wa Vyama vya Upinzani: Sababu 10 kwanini wapinzani wanyimwe kura mwaka huu 2020

MKINGUZI

Member
Apr 17, 2015
40
85
1. Sera zao ni za ushari, hila, fujo ghiliba za kubomoa na kutengeneza Tanzania ya machafuko kwani kwao amani tuliyonayo si kitu kwao isipokuwa tamaa za madaraka.

2. Wakati Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakipitisha bajeti za kimaendeleo Bungeni, wao Wapinzani walikuwa na kazi ya kususia vikao, utoro Bungeni na kupinga mikakati ya kimaendeleo ya nchi. Bajeti zote zimepitishwa kwa kura za ndio za Wabunge wa CCM, wao kazi yao ni kutoa shilingi na kusema hapana ili kukwamisha bajeti

3. Kuna vyama vimejipambanua wazi wazi wakishika dola wataingiza nchi kwenye sera ya ushoga ya kuamini kwenye ndoa ya jinsia moja.

4. Wakati Rais Magufuli akidhibiti rasilimali zetu zitunufaishe sisi Watanzania wao vyama vya upinzani waliungana na Mabeberu kupinga hatua hiyo kwa hoja kuwa tutashtakiwa, tutafilisiwa na tuliwasikia wakitamka hivyo wazi wazi. Wanaamini rasilimali zetu ni haki ya Mabeberu na si Watanzania

4. Wamesema kwa kauli za majukwaani wakishika dola watasimamisha miradi yote ya kimkakati ya kukiza uchumi iliyoanzishwa na Rais Magufuli kwani hawaamini kwenye maendeleo ya vitu ambayo kimsingi ndio maendeleo ya Watu.

5. Wapinzani wanaamini vyura ni bora zaidi kuliko Watanzania kupata umeme wa uhakika kutoka Mto Rufiji utakaozalisha megawatts 2115. Bora Watanzania wasiwe na umeme wa uhakika, wabaki gizani ili wasikie sauti za vyura.

5. Kwao vyama vya upinzani wanaona mahitaji ya Watanzania ni Bunge live, Watu kutukana hovyo na sio tena elimu bure, huduma bora za afya nk. Wallah, tuna Wapinzani wa hovyo kweli nchi hii.

6. Wanapinga fedha kuelekezwa kwenye miradi ya kimaendeleo zaidi na badala yake wanataka fedha iongezwe kwenye vitafunwa, posho, semina na warsha. Kwao Wapinzani bora yao ni vitumbua na maandazi maofisini kwa wachache kuliko ujenzi wa barabara, madaraja, hospitali, kupeleka umeme na maji vijijini kwa manufaa ya wengi.

7. Kwao wanaamini katika sera ya kutugawa kikanda ili watugawe Watanzania kwa misingi ya ukabila, udini, urangi ili waweze kushirikiana na Mabeberu kututawala na kutunyonya. Hizi ni sera za mawakala wa Mabeberu walizonazo wwpinzani kuuza nchi.

8. Jukwani wananadi ilani ya afya zao binafsi na kuomba michango ya kampeni. Ni dhahiri wakichaguliwa watajali maslahi yao binafsi kwanza kuliko ya Watanzania.

9. Waliowachagua Wapinzani 2015 waliishia kupata majuto ya kusikia malumbano ya vyama vyao kuliko maendeleo; Upingaji wa maendeleo ikiwemo kususia vikao na kutopitisha bajeti za kimaendeleo; viongozi wao wa upinzani kutokuonekana majimboni kutwa wanashinda Mahakamani kisutu wakipigania wasiyoyahaidi kwa wapiga kura wao, usaliti mkubwa huu. Kuchagua Wapinzani ni kuchagua majuto.

10. Ilani zao Wapinzani zimejaa mahitaji yao binafsi Wanasiasa kuliko mahitaji ya kimaendeleo ya Wananchi. Wakati wakihaha na sera za Bunge live, mara Katiba wao CCM wanaeleza namna watakavyowajengea miundombinu, watakavyo toa huduma za kijamii kiufanisi zaidi kila sehemu .

Mpaka sasa dalili zote za kisayansi kiushindi zinaonyesha Watanzania kuchagua vitendo vya CCM na sio maneno matupu ya upinzani. Wamekataa kufanya majaribio ama kurudishwa kwenye kundi la Watu maskini na badala yake wanakomaa waingie uchumi wa kati kati na kuendelea.

Kila sehemu jambo la ushindi kwa Rais Magufuli, ushindi kwa Wabunge na Madiwani wa CCM, yametiki.

*Shilatu, E.J*
 
UVCCM katika ubora wake. Hii yote ni baada tu ya tamko la Katibu Mkuu wao.
 
Wafanyakazi ( walimu, wajeda ,watumishi mbali mbali), waliofukuzwa kazi, mama ntilie, boda boda, wamachinga, waliokosa ajira na wanyonge wote hao wanawachora tu. Ila yaliyopo moyoni ni kwenye sanduku la kura , pale meza itakopogeuzwa juu chini.

Tuendelee kupiga kampeni ,. Mwaka huu mtapigwa chini kimya kimya.
 
Nyie ndio wasiokuwa na akili wa nchi hii kutokana na kuwa na shida nyingi mno kiasi cha kushindwa hata kufikiri na kuona umaskini wenu unasababishwa na ccm. Mkoa gani unatoka?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom