Habari za muda huu wana bodi.
Moja kwa moja nijikite katika mada leo mchana nimepata kutumia bidhaa hii mpya sokoni kutoka kampuni ya uzalishaji wa vyakula, vinywaji na vitu vingine (inayosimamiwa na Mohamed Dewji)
BEI YA BIDHAA
Bidhaa hii mpya sokoni inaenda kwa bei ya Sh 300 tu pesa taslimu ya kitanzania hivyo kuifanya iweze kupenya ipasavyo kwa watumiaji wengi yaani watu wa market tunasema ametumia penetration pricing strategy kuifanya bidhaa yake ikubalike kwa haraka ili kutengeneza customer base kubwa ukilinganisha na bei ya Azam ukwaju inayouzwa kwa Tsh 600 kwa 500 Tsh.
BIDHAA YENYEWE
Uongo mbaya na nisiwe mnafiki katika sehemu Mo alipofeli na team yake ni katika product hii kwa 100% zipo nyingine pia japo makosa yake sio makubwa sana kama hii,kwanza kabisa ubovu wa bidhaa hii ni
1. Ladha ya bidhaa
Sijajua fomula iliyotumika kutengeneza hii kitu asee yaani haieleweki ni chungu au tamu yani ladha yake ni mbaya kiukweli haielezeki watengeneza juice na lamba lamba wa mtaani wanatengeneza vitu vizuri zaidi ya hii ya Mo mara 200.
2. Muonekano wa bidhaa
Kiukweli bidhaa ya Mo inamuonekano mbaya sana (yaani namaanisha packaging yake imekaa kilocal sana) mithili ya kinywaji pendwa cha vijana wa mtaani au wapiga debe kinachoitwa double kick hivyo kupoteza mvuto na hamu machoni kwa mtumiaji.
UBUNIFU
Kiukweli Nimekuwa insipred sana na vitu Mo anavyofanya japo huwa nakwazika sana pale ninapoona anakosa ubunifu katika bidhaa badala yake anakopi kila kitu kwa mshindani wake Azam.
Mfano: MO PASSION= AZAM JUICE/AZAM COLA, UHAI=MASAFI, AZAM ENERGY DRINK= MO ENERGY, AZAM UKWAJU = MO UKWAJU
Ila pia katika bidhaa za unga na mafuta. Kiukweli MO amekosa watu wa Business Reserch na Marketing walio na weledi wakujua kitu gani soko linaitaji badala ya kusubiri mwingine alipowekeza juhudi zake ndipo na yeye apate wigo wa kukopi watu wa biashara wanasema kwa ufupi sio mtu wa kurisk sana.
Ni mtu anaetegea mpinzani aanzishe jambo yeye aje kukopi ila pia nlitegemea akikopi ideas aje na vitu bora kuliko mshindani wake mfano COCA COLA na PEPSI badala yake jina ndilo linauza kuliko bidhaa yenyewe.
NB: Ubora wa kitu unapimwa na bei pia kwa watu wa segment fulani hivyo kuweka price ndogo sio suruhisho bali kwa watu wengine uchukulia bidhaa kuwa ni mbovu sana.
Nawasilisha wanabodi