Ubovu wa elimu yetu, tatizo letu ni wizi na ufisadi, kutumiwa na mashirka ya kimataifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubovu wa elimu yetu, tatizo letu ni wizi na ufisadi, kutumiwa na mashirka ya kimataifa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Miwatamu, Oct 13, 2012.

 1. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133


  Kilio kikubwa mashule ni ukosefu wa vitabu, watoto wamekuwa wakisoma kwa shida kutoka na vitabu vya kuchangia au kutokuwepo vituba kabisa,wakati huo huo, vinaibuka tuhuma kwamba viongozi wa serikalikatika sekta husika wamekula rushwa ili kutoa tenda za vitabu. Bofya school books scandal

  Baada ya kusoma hii habari nimejiuliza maswali mengi sana, ya kwamba ni ninikikwazo cha kutokuwa na vitabu mashuleni? Je ni kikwako cha pesa au kikwazo cha kiutendaji/uongozi?
  Binafsi kwa sasa nashawishika kusema tunatatizo kubwa kwenye kiongozi kuliko kifedha, kwa maana nyingine ni kwamba kuendelea kufanya mipango yoyote kwa sasa ni sawa na kuchota maji kwa kutumia tenga!!!!


  Tunachota maji kwa kutumia tenga kwa kigezo kwamba kila pesa inapopatikana kwa ajili ya miradi mbalimbali katika Taifa letu, kuna wajanja wanajua jinsi ya kuiiba na kuitafuna, ili tatizo la wizi linaangaliwa kama kitu cha kawaida. kinachofanyika ni pesa kutafutwa na wajanja kupora tena na tena
  Je kama tungekuwa na viongozi wenye busara nadhani wange shughulikia tatizo la kukosekana kwa maadili na wizi/ufisadi kwanza kuliko kuendelea kusaka hela ambazo mara zote zinaishia mikononi mwa wapolaji. Tatizo la Madawati, vitabu na mengineyo yanaweza kutatuliwa kama tunaondoa tatizo wezi wa mali za umma.

  posted by lifeofmshaba lifeofmshaba at 22:20:00 Wednesday, July 04, 2012

   
Loading...