Ubovu wa barabara ya Mombasa kwa Mkolemba

Ivan said

Member
Feb 14, 2021
83
107
Ukitazama barabara ya Mombasa kwa mkolemba jimbo la ukonga utajiuliza yu wapi Jerry Slaa mbunge wa jimbo la Ukonga?. Upo wapi mheshimiwa mbunge au unasubiri 2025 tena uje na porojo hewa kwetu sisi wananchi tunaotaabika kwa ubovu wa barabara ya Mombasa, Moshi bar, Kwa Mkolemba, Kanyigo, Mwembeni hadi njia panda ya Msongola?.

Hivi ni kwa nini hauji utuambie bungeni mlikuwa mnajadili na kupitisha nini?.

Hivi ni kw nini hauji kutuambia 1.5 Bilioni ambazo mama amesikia kilio chetu zitatumika kutengeneza barabara/njia za mitaa ipi na IPI?.

Behold Jerry Silaa (MB) Ukonga Dar es Salaam.
 
... ndio maana tunatakiwa kulipa kodi (mafuta, vocha, miamala, n.k.) barabara zijengwe.
 
... ndio maana tunatakiwa kulipa kodi (mafuta, vocha, miamala, n.k.) barabara zijengwe.
Na ni muda wakuwatambua wale wazalendo kwelikweli keanu watajitolea wao wakatwe mara mbili ya wengine.
 
Kwa kweli hiyo barabara ni mbovu sana, na ina umuhimu wa kutosha,
a. Magari yanayopita ni mengi ndio maana kuna vituo vya mafuta vya kutosha kutoka Mombasa mpaka Mwembeni vipo vitano.
b. Inaelekea kwenye hospitali ya wilaya ya Msongola. Wagonjwa wanahitaji urahisi wa kufika hospitali ama kuwahishwa kwenye rufaa hospitali za juu.
c. Junction hapo Mwembeni ndio nyumbani kwa Naibu Waziri Tamisemi anayeshughulikia barabara Mh Mwita Waitara(Mb), na alishapigia sana chapuo barabara hiyo akiwa mbunge wa Jimbo hilo, hivyo uwakilishi ni mkubwa zaidi ya Jerry Slaa peke yake wanatakiwa kupiga collabo.
d. Hiyo barabara inatoka kwa wazalishaji wakubwa wa Mayai na Mbogamboga ambazo kutokana na delicacy na perishability yake, zinahitaji uharaka wa kufika sokoni.
 
Back
Top Bottom