Ubovu wa barabara kutoka mataa ya Chang'ombe (VETA) hadi kona ya Uwanja wa Taifa

TUPAMBANE

Member
Jan 25, 2021
62
88
Hii barabara kwa Muda mrefu sana imekuwa ikizalisha foleni kutokana na ubovu wa hiyo barabara. Ukianzia kipande cha kutoka kona ya uwanja wa taifa au ukianzia JKT Kuelekea VETA hiki kipande kimekuwa kikitupatia sana usumbufu sisi Abiria na watembea kwa miguu kipande hiki kinazalisha foleni kubwa kutokana na miundombinu ya barabara kuwa mibovu.

Ombi langu kwa Mkuu wa Mkoa au wenye Mamlaka ninaomba hicho kipande cha barabara kutoka kona ya uwanja wa Taifa kwenda mataa ya VETA kijengwe kwa kiwango cha zege maana kipande hichi kina maji maji mengi hivyo itakuwa ndio suluhisho lake. Pia ninaomba wahusika watengeneze mitaro mikubwa ambayo itapunguza wingi wa maji kutoka katika maeneo mbalimbali.
 
Back
Top Bottom