Uboreshaji wa taratibu za ununuzi na mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano katika Ujenzi wa Viwanda

kapyela

Member
Feb 13, 2013
11
8
UBORESHAJI WA TARATIBU ZA UNUNUZI NA MWELEKEO WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KATIKA UJENZI WA VIWANDA

Serikali ya awamu ya tano katika siku zake 100 madarakani ilijikita katika kutengeneza mifumo inayopunguza mnyonyoro wa maamzi jambo ambalo lilipelekea pesa za maendeleo kufika kwa wakati na miradi mingi kukamilika kwa wakati.

Kwa muktadha huu, ni jambo la kupongeza kwa serikali kubadili sera mbalimbali za uwekezaji nchini zilizojikita kuondoa mnyororo unaotakiwa ufuatwe ili mwekezaji apate kibali cha uwekezaji na ukazi nchini jambo ambalo limepelekea miradi miradi mingi kufanyika kwa wakati. Kwa kuanzia naomba nitoe mtiririko wa sera zilizoboreshwa hapa nchini.

Mosi, Sera ya Madini, itakumbukwa kuwa kabla ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani mchango wa sekta ya madini kwenye pato la taifa ulikuwa mdogo sana lkn baada ya maboresho ya sera ya madini ambapo hapo awali ni aslimia 3 tu serikali ilikuwa inapewa lkn kwa sasa kuna uwiano ambao una mantiki na unaakisiwa na mipango kazi madhubuti.

Mbili, Maboresho ya sera ya Maliasili na Utalii, ni jambo la kupongeza kwa jinsi serikali inavyopiga hatua kwenye mapato yanayotokana na utalii. Zaidi ya asilimia 17 ya pato la taifa linatokana na Utalii jambo ambalo linaleta chachu ya maendeleo na hivyo kuchochea Uwekezaji nchini.

Tatu, Maboresho ya sera ya Ardhi, Nyumba na Makazi ya mwaka 1999. Ni Jambo la kupongeza kwa viwanja vingi kupimwa na hivyo kuongeza kodi kwa nchi, maeneo ya Uwekezaji kutambuiliwa, Mipongo miji kufanyika kwa ustadi mkubwa jambo ambalo linachochea pia utalii wa ndani.

Nne, Maboresho ya sera ya Mazingira ya mwaka 2004. Ni jambo la kupongezwa kwa sera hii kufanyiwa maboresho ya muhimu ili kutunza mazingira yetu. Fauna na Flora ni muhimu kutunzwa maana 'EXTINCTION' ya mimea mbalimbali ni kwasababu mazingira yanakuwa hayatunzwi ipasavyo. Mabadiliko ya Hali ya Hewa (Climate Change) yanasababishwa na mazingira kutokutunzwa ipasavyo. Ozone layer ikapasuka inaweza kusababisha joto hapa duniani kuongezeka na hivyo kuleta madhara makubwa na hiyo imeanza kuonekana katika maeneo mengi ambapo joto linaongezeka kwa kasi kubwa.

Tano, Maboresho ya Sera ya Uwekezaji, Uwekezaji ninaozungumzia ni wa viwanda. Hapo zamani kidogo uwekezaji ulikuwa umegubikwa na mnyonyoro wa Rushwa kubwa sana lakini serikali ya awamu ya TANO imeondoa hiyo sintofahamu na kupelekea mambo kufanyika kwa wakati na kwa Ufanisi mkubwa.

Sita, Maboresha ya sera za mikataba, hapo zamani utiaji saini wa mikataba ulikuwa umegubikwa na rushwa sana mpaka kupelekea zoezi hilo kufanyika ughaibuni ikiambatano ya perdiem kubwa sana. Lakini kwa sasa tumeshuhudia MABORESHO makubwa na ya dhati. Tunapaswa sana kuipongeza serikali ya awamu ya Tano Chini ya Dr. JPM.

Saba, Sera na Sheria za Kodi, tumeshuhudia kwa miaka hii mitano kodi nyingi ambazo sio za Lazima zimeondolewa. Hii TAX WEAVER imesaidia wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuhamasika kutoa kodi jambo ambalo limeleta ongezeko la mapato nchini.

Lazima ifahamike kuwa huwezi ukawa na UCHUMI imara kama hajatunga sera na SHERIA za kukufikisha huko. Mara nyingi urasimu unapelekea shughuli nyingi kutokufanyika kwa wakati. Lakini kwa miaka hii mitano tumeshuhudia mnyororo wa maamzi ukipunguzwa kwa kiwango kikubwa jambo ambalo limeleta ufanisi kwa kuongeza kasi na kuleta chachu ya mafanikio yalifikiwa na serikali.

Kupinga Rushwa ndani ya CHAMA na serikali, hili si jambo dogo Rushwa ni adui wa haki. Palipo na Rushwa hakuna Haki. Lakini lazima ifahamike kuwa swala la Rushwa ni Mtambuka, mpaka RUSHWA kufikia asilimia ambayo mataifa makubwa yanatambua na kuona mchango si jambo dogo. Ni ukweli ulio wazi kuwa Mataifa ya Afrika yamegubikwa sana na Rushwa, MARA nyingi wa viongozi walioshika nyazifa kubwa serikalini. Lakini RAIS wetu amethubutu kwa vitendo kupinga rushwa kwa VITENDO.

Swala la Usambazaji UMEME vijijini, kabla ya Dr. JPM kuingia madarakani ni vijiji zaidi ya 3000 vilikuwa vimesambaziwa UMEME, lakini mpaka sasa vijiji zaidi ya 9000 vina UMEME, jambo ambalo linachochea ujenzi wa viwanda. Na hivyo kuchechea ongezeko la mapato kwa taifa.

Ujenzi wa Reli, Kama ambavyo mikoa yote ya Tanzania imeunganishwa na LAMI ndivyo ambavyo maono ya Mhe RAIS yapo upande wa Reli. Kama Mikoa yote nchini ikiunganishwa na Reli maana yake 'life span' ya barabara zetu itaongezeka na hivyo kuleta ufanisi katika Usafirishaji.

Ujenzi wa Kilometer zaidi ya 2000 za barabara, ni jambo la kupengeza kwa barabara nyingi kutandazwa lami hili litaleta Ufanisi katika usafirishaji wa mazao. Kongole nyingi kwa Mhe RAIS.

Ununuzi wa ndege, Mara nyingi ni ukweli ulio wazi kuwa ndege huchochea utalii na Uwekezaji jambo ambalo linaleta chachu ya maendeleo na hivyo kuongeza pato la taifa.

Ujenzi wa Hospitali za kanda, vituo vya afya na zahanati, ni jambo la kupongeza kwa ili kufanyika na hivyo kupunguza vifo ambavyo vinazuirika. Kongole kwa JPM

Ujenzi wa madaraja chini na ya juu. ni jambo la kupungeza jiji kama la Dar es Salaam mara nyingi linafoleni unapojengwa flyovers kwenye makutano ya barabara unapunguza foleni na hivyo kuleta maendeleo thabiti.

Ujenzi wa kituo cha Kufua Umeme zaidi ya MEGAWAT 2100, sasa ktk historia Tanzania inakuwa na ziada ya Umeme jambo ambalo linachochea ujenzi wa viwanda.

Ujenzi wa Viwanda, jambo hili linapaswa kupongezwa zaidi ya viwanda 3000 vimejengwa nchi nzima vikihusishwa viwanda vidogo, vya kati na VIKUBWA. Unapokuwa unazalisha bidhaa ndani ya nchi maana yake unaexport zaidi kuliko kuimport jambo ambalo linaongeza pesa za KIGENI na hivyo kukuza thamani ya fedha na kuleta chachu ya MAENDELEO.

Inaendelea................

Na Goodluck Goodluck Kapyela,
(BSc, MSc)
 
Back
Top Bottom