Uboreshaji wa Jiji la Dar es salaam kupitia mradi wa DMDP

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1569476244012.png

MRADI wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam “Dar es Salaam Metropolitan Development Project” (DMDP) unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI unaendelea kutekelezwa katika Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya kwanza ya utekelezaji.

Mradi huo umetokana na serikali kuingia mkataba na Benki ya Dunia wa thamani ya dola za Marekani milioni 300 kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano.

Sio fedha hizo tu tulizopata kwa ajili ya mradi huo tumepata pia dola za Marekani milioni tano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya nchi za Nordic na serikali inachangia dola za Marekani milioni 25.3 kwa ajili ya mradi huo.

Madhumuni ya mradi wa DMDP ni kukabiliana na changamoto zinazolikabili Jiji la Dar es Salaam kwa kutilia mkazo uboreshaji wa huduma za jamii kama miundombinu ; na kujenga uwezo wa manispaa za jiji katika utoaji huduma, kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kukabili matukio makubwa ya dharura.

Kabla ya kuanza kwa mradi huo, ulifanyika usanifu mbalimbali na kufuata vigezo muhimu bila kuangalia umaarufu wa eneo na itikadi na miradi hiyo itaunganishwa katika maeneo ya watu wenye kipato kidogo na yaliyojengwa kiholela pamoja na kuunganisha wilaya na mkoa.

Fedha hizo zimegawanywa katika manispaa zote za Jiji ambazo watatumia kujenga barabara za mlisho (feeder road) zenye urefu wa kilometa 65.6, ujenzi wa mitaro mikubwa yenye urefu wa kilometa 31.8 na ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 145.

Manispaa ya Kinondoni ni moja kati ya Halmashauri za Jiji la Dar es salaam ambapo mradi unatekelezwa. Kupitia Mradi huu wa DMDP, mabadiliko makubwa yameanza kuonekana na kuleta faraja na matumaini makubwa kwa wananchi wa Manispaa hiyo na Jiji kwa ujumla. Miundombinu ya Barabara, Madaraja na Mifereji ya Maji inajengwa kwa kiwango bora kabisa kwa usimamizi wa karibu wa Ofisi ya Rais Tamisemi.

Mandhari katika mitaa ya Kinondoni imeanza kubadilika na kutatua kero za wananchi hasa katika swala zima la uboreshaji wa miundo mbinu na huduma za kijamii.

1569476199992.png

Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Utekelezaji umegawanyika katika Mafungu saba (Seven Packages) kama ifuatavyo: –

Fungu 1: Ujenzi wa barabara tano za Sokoni-Makumbusho, MMK, Nzasa, Viwandani na Tanesco – Soko la Samaki, zenye urefu wa kilometa 11.92 (11.92 km);

Fungu 2: Ujenzi wa barabara tano ambazo ni Makanya, Tandale – Kisiwani, Simu 2000, Kilimani, Kilongawima, na CBD Makumbusho zenye urefu wa kilometa 6.73 (6.73 km);

Fungu 3: Ujenzi wa barabara Nne za External, Kisukuru, Majichumvi – Kilungule na Kilungule – Korogwe zenye urefu wa kilometa 6.73 (6.73 km);

Fungu 4: Mto Sinza: Ujenzi wa miundombinu ya mafuriko na mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa kilometa 7.5 (7.5 km);

Fungu 5: Uboreshaji wa miundombinu katika makazi holela ya Tandale, mifereji na barabara na zenye urefu wa kilometa 5.1 (5.1km) na Mburahati zenye urefu wa kilomita 2.9 (2.9 km);

Fungu 6: Uboreshaji wa miundombinu katika Makazi Holela ya Mwananyamala, mifereji na barabara na zenye urefu wa kilometa zenye urefu wa kilomita 6.1 (6.1 km); na

Fungu 7: Usanifu wa barabara nyingine tano ambazo ni Shekilango, Muhimbili Hospitali, Magomeni Mapipa – Urafiki, Moroko – Kawe na Makumbusho – Mwanamboka, zenye urefu wa kilometa 15 (15 km).

Mradi wa DMDP pia unalenga kuimarisha upatikanaji wa fedha, kugawa Mamlaka, kuboresha uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za Serikali za Mitaa na kuboresha usimamizi wa mifumo ya uhamisho kati ya Serikali

Mradi wa DMDP unalenga kuimarisha mifumo ya usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Jiji la Dar-es-Salaam ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi kwa wakati na mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, yaani kuanzia mwaka 2015-2020.

Manispaa ya Ilala ni miongoni mwa Halmashauri tatu zilizopo Dar-es-Salaam ambazo zipo kwenye utekelezaji wa mradi wa DMDP, ambapo mradi huu unatekelezwa katika vipengele vinne. Utekelezaji wa vipengele hivyo ni kama ufuatao:

1) Eneo la Miundombinu

Kwenye kipengele hiki, mradi utagusa maeneo mawili, ambayo ni;

a) Barabara za mitaani, ambapo kwa Manispaa ya Ilala zitajengwa barabara zenye urefu wa kilomita 13.

b) Uboreshaji wa miferiji ya maji ya mvua

2) Uboreshaji wa makazi holela

Katika eneo hili kutakuwa na uboreshaji kwenye barabara, mifereji, masoko, vyoo vya Umma, vizimba vya taka na magari ya kukusanyia taka na kata zitazonufaika na mradi ni Kata ya Kiwalani ambayo itakuwa na barabara yenye urefu wa kilomita 14, Kata ya Ukonga itakuwa na barabara ya kilomita 6 na Kata ya Gongolamboto kilomita 4.

3) Kuimarisha na kujenga uwezo wa Taasisi

Katika eneo hili, mradi utahusika na ujengaji wa uwezo kwa Watumishi wa Manispaa ya Ilala, kuimarisha mfumo wa ukusanyaji mapato.

4) Kutoa msaada wa utekelezaji wa mradi

Katika eneo hili kampuni zitakazotoa msaada wa utekelezaji ni UWP, Lea Associates.
 
Mbona hamna linalosemwa kuhusu uboreshaji na upanuzi wa mtandao wa kukusanya maji taka au kwa lugha ya wenyewe "sewerage system"?

Hauwezi kuwa na mji wa kisasa unaojali afya ya wakazi wake kama utaendelea kutegemea "septic tanks" na "soak pits".

Nilitegemea hili lingepewa kipaumbele kuliko hata barabara kwa sababu mitandao hii inatakiwa kupita chini ya barabara. Ni vigumu sana kuiweka baada ya barabara kujengwa.

Amandla........
 
Mbona Temeke hasa viunga vya mbagara havipewi kipaumbele au haya mambo ya kinondoni tu
Mbona yombo tayari mkuu sasa hivi barabara za mtaani zina lami ya kiwango pamoja uboreshaji wa miundombinu mingine kama madaraja na mitaro, kama allivyosema mtoa mada kwamba miradi hiyo ni endelevu basi hata huko inaweza fika ila cha kunote kwamba haitowezekana kwa jiji zima kila sehemu kwa ujumla
 
View attachment 1216246

MRADI wa Uboreshaji wa Jiji la Dar es Salaam “Dar es Salaam Metropolitan Development Project” (DMDP) unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI unaendelea kutekelezwa katika Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni awamu ya kwanza ya utekelezaji.

Mradi huo umetokana na serikali kuingia mkataba na Benki ya Dunia wa thamani ya dola za Marekani milioni 300 kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano.

Sio fedha hizo tu tulizopata kwa ajili ya mradi huo tumepata pia dola za Marekani milioni tano kutoka Mfuko wa Maendeleo ya nchi za Nordic na serikali inachangia dola za Marekani milioni 25.3 kwa ajili ya mradi huo.

Madhumuni ya mradi wa DMDP ni kukabiliana na changamoto zinazolikabili Jiji la Dar es Salaam kwa kutilia mkazo uboreshaji wa huduma za jamii kama miundombinu ; na kujenga uwezo wa manispaa za jiji katika utoaji huduma, kuchangia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kukabili matukio makubwa ya dharura.

Kabla ya kuanza kwa mradi huo, ulifanyika usanifu mbalimbali na kufuata vigezo muhimu bila kuangalia umaarufu wa eneo na itikadi na miradi hiyo itaunganishwa katika maeneo ya watu wenye kipato kidogo na yaliyojengwa kiholela pamoja na kuunganisha wilaya na mkoa.

Fedha hizo zimegawanywa katika manispaa zote za Jiji ambazo watatumia kujenga barabara za mlisho (feeder road) zenye urefu wa kilometa 65.6, ujenzi wa mitaro mikubwa yenye urefu wa kilometa 31.8 na ujenzi wa barabara za mitaa kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 145.

Manispaa ya Kinondoni ni moja kati ya Halmashauri za Jiji la Dar es salaam ambapo mradi unatekelezwa. Kupitia Mradi huu wa DMDP, mabadiliko makubwa yameanza kuonekana na kuleta faraja na matumaini makubwa kwa wananchi wa Manispaa hiyo na Jiji kwa ujumla. Miundombinu ya Barabara, Madaraja na Mifereji ya Maji inajengwa kwa kiwango bora kabisa kwa usimamizi wa karibu wa Ofisi ya Rais Tamisemi.

Mandhari katika mitaa ya Kinondoni imeanza kubadilika na kutatua kero za wananchi hasa katika swala zima la uboreshaji wa miundo mbinu na huduma za kijamii.

View attachment 1216245

Katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Utekelezaji umegawanyika katika Mafungu saba (Seven Packages) kama ifuatavyo: –

Fungu 1: Ujenzi wa barabara tano za Sokoni-Makumbusho, MMK, Nzasa, Viwandani na Tanesco – Soko la Samaki, zenye urefu wa kilometa 11.92 (11.92 km);

Fungu 2: Ujenzi wa barabara tano ambazo ni Makanya, Tandale – Kisiwani, Simu 2000, Kilimani, Kilongawima, na CBD Makumbusho zenye urefu wa kilometa 6.73 (6.73 km);

Fungu 3: Ujenzi wa barabara Nne za External, Kisukuru, Majichumvi – Kilungule na Kilungule – Korogwe zenye urefu wa kilometa 6.73 (6.73 km);

Fungu 4: Mto Sinza: Ujenzi wa miundombinu ya mafuriko na mifereji ya maji ya mvua yenye urefu wa kilometa 7.5 (7.5 km);

Fungu 5: Uboreshaji wa miundombinu katika makazi holela ya Tandale, mifereji na barabara na zenye urefu wa kilometa 5.1 (5.1km) na Mburahati zenye urefu wa kilomita 2.9 (2.9 km);

Fungu 6: Uboreshaji wa miundombinu katika Makazi Holela ya Mwananyamala, mifereji na barabara na zenye urefu wa kilometa zenye urefu wa kilomita 6.1 (6.1 km); na

Fungu 7: Usanifu wa barabara nyingine tano ambazo ni Shekilango, Muhimbili Hospitali, Magomeni Mapipa – Urafiki, Moroko – Kawe na Makumbusho – Mwanamboka, zenye urefu wa kilometa 15 (15 km).

Mradi wa DMDP pia unalenga kuimarisha upatikanaji wa fedha, kugawa Mamlaka, kuboresha uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za Serikali za Mitaa na kuboresha usimamizi wa mifumo ya uhamisho kati ya Serikali

Mradi wa DMDP unalenga kuimarisha mifumo ya usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Jiji la Dar-es-Salaam ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma kwa Wananchi kwa wakati na mradi huu umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano, yaani kuanzia mwaka 2015-2020.

Manispaa ya Ilala ni miongoni mwa Halmashauri tatu zilizopo Dar-es-Salaam ambazo zipo kwenye utekelezaji wa mradi wa DMDP, ambapo mradi huu unatekelezwa katika vipengele vinne. Utekelezaji wa vipengele hivyo ni kama ufuatao:

1) Eneo la Miundombinu

Kwenye kipengele hiki, mradi utagusa maeneo mawili, ambayo ni;

a) Barabara za mitaani, ambapo kwa Manispaa ya Ilala zitajengwa barabara zenye urefu wa kilomita 13.

b) Uboreshaji wa miferiji ya maji ya mvua

2) Uboreshaji wa makazi holela

Katika eneo hili kutakuwa na uboreshaji kwenye barabara, mifereji, masoko, vyoo vya Umma, vizimba vya taka na magari ya kukusanyia taka na kata zitazonufaika na mradi ni Kata ya Kiwalani ambayo itakuwa na barabara yenye urefu wa kilomita 14, Kata ya Ukonga itakuwa na barabara ya kilomita 6 na Kata ya Gongolamboto kilomita 4.

3) Kuimarisha na kujenga uwezo wa Taasisi

Katika eneo hili, mradi utahusika na ujengaji wa uwezo kwa Watumishi wa Manispaa ya Ilala, kuimarisha mfumo wa ukusanyaji mapato.

4) Kutoa msaada wa utekelezaji wa mradi

Katika eneo hili kampuni zitakazotoa msaada wa utekelezaji ni UWP, Lea Associates.
Fungu la 4 limeingiliwa kisiasa, mwanzoni ilikuwa mto sinza ujengwe kuanzia mandela mpaka jangwani na michoro ilikuwa tiyari. Baada ya serikali kukosa hela za kulipa fidia kama yalivyokuwa makubaliano, michoro ilibadilishwa na sasa ujenzi wa kingo za mto utaanzia shekilango. Hapo tatizo la maafuriko litabaki pale pale.
 
Hela zote hizo billions of Tshs alafu hata mto Msimbazi siuoni wakiupanua na kuwekea ukingo ili kipindi cha mvua mafuriko yote yaende baharini. Jamani msipojenga na kupanua mto Msimbazi, Dar itabakia na mafuriko kila wakati, maji mengi yanavamia hadi Posta sbb mto Msimbazi umezibwa sana na makaazi ya watu pamoja na magugu maji kibao, wangeujenga huo mto kipindi hiki cha kiangazi haraka haraka, kuna tatizo gani? 😓 Pia wangevunja kabisa kile kituo cha mwendokasi pale Msimbazi katikati ya mto, yaani waliojenga sijui walimjengea nani anapanda pale.. Kwanza inablock maji ya mto, hawa ma contractor wengine, sijui macho hawaoni?
 
Kwa wakurya kwa yule kiongozi wa waasi aliyekimbilia unaibu waziri wa TAMISEMI mbona hata tundu la choo halionekani?

Waitara kapotea sana. Sijui kaishia wapi huyu mtu.
 
Saizi ni zaidi ya miezi 4 wakandarasi hawajalipwa.... Pamoja na wahandisi washauri.... Inasemekana serikali ilichukua fedha hizo na kuzitumia, sasa Hazina mzigo hautoki. WB wanaelekea kumind manake ni tofauti na makubaliano
 
Back
Top Bottom