Ubora wa wabunge wetu uko chini kuliko matumaini yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubora wa wabunge wetu uko chini kuliko matumaini yangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MchunguZI, Jun 28, 2011.

 1. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Jamani! Tukubali kwamba ubora wa wabunge wetu uko chini kuliko tunavyotegemea. Tofauti na bunge la Uganda na Kenya, kwa kulinganisha michango yao bungeni. Tatizo kubwa kabisa liko chama tawala, CCM.

  Hali nionayo na michango tunayoiona na kusikia Bungeni, inafadhaisha. Wabunge wengi na hasa hawa wa viti maalumu kama ukiwapa kuandika michango yao kwa maandishi, utaishia kuwapa maksi chini ya nusu.

  Wanaonekana kufahamu matatizo ya wananchi lakini hawawezi kupanga maelezo kwa ufahamu. Ni kama wote ni darasa la 12 division zero! Baadaye naona wanaishia kusifia Chama, spika mwanamke na Rais ili wapate makofi.

  Hatutafika. Tuongeze ubora wa wabunge badala ya idadi ya wabunge. Niskiavyo kwa Uganda mbunge lazima awe ni graduate! Sisi bado ni kujua kusoma na kuandika.
   
Loading...