Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
Upo kwenye wodi mahututi aka ICU, aka Intensive Care Unit... kupumua kwako kwa mashine, mirija ya maji inapita mkono wa shoto, mkono wa kulia mrija wa damu. Mrija mwingine unapitia puani kusaidia kuondoa accumulated fluids tumboni, na mrija mwingine (catheter) unakusaidia kutoa haja ndogo. Inshort hujielewi hujitambui, (Umezimika)!
...siku ya siku unaibuka na kushangaa shangaa 'imekuwaje'! hujavunjika kiungo chochote zaidi ya mchubuko kidooogo usoni. unazidi kushangaa kuna watu wamekizunguka kitanda chako, hao watu wanakusemesha kana kwamba wanakujua saaana, wanakwambia ulipata ajali, 'kazi ya mungu', hujaumia sana! Unawashangaa...
...baada ya siku kadhaa unawatambua baadhi ya watu wazima waliokuwepo, baba, mama, isipokuwa huyo mwanamke ambaye amembeba mtoto mgongoni ambaye kila akija anakuita "mume wangu", na katoto kengine pembezoni ya kitanda anayekuita baba!... unazidi kushangaa!
Memory imefutika, hakuna kumbukumbu iliyobakia kichwani! memory ya miaka mitatu iliyopita imekwenda!
Hii inasababishwa na nini?
waganga na wauguzi, hii ndio matokeo ya ile 'kaputi-nzima' mnayoiita 'milk of amnesia'?