Suala la kupoteza kumbukumbu likoje

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
Upo kwenye wodi mahututi aka ICU, aka Intensive Care Unit... kupumua kwako kwa mashine, mirija ya maji inapita mkono wa shoto, mkono wa kulia mrija wa damu. Mrija mwingine unapitia puani kusaidia kuondoa accumulated fluids tumboni, na mrija mwingine (catheter) unakusaidia kutoa haja ndogo. Inshort hujielewi hujitambui, (Umezimika)!

...siku ya siku unaibuka na kushangaa shangaa 'imekuwaje'! hujavunjika kiungo chochote zaidi ya mchubuko kidooogo usoni. unazidi kushangaa kuna watu wamekizunguka kitanda chako, hao watu wanakusemesha kana kwamba wanakujua saaana, wanakwambia ulipata ajali, 'kazi ya mungu', hujaumia sana! Unawashangaa...

...baada ya siku kadhaa unawatambua baadhi ya watu wazima waliokuwepo, baba, mama, isipokuwa huyo mwanamke ambaye amembeba mtoto mgongoni ambaye kila akija anakuita "mume wangu", na katoto kengine pembezoni ya kitanda anayekuita baba!... unazidi kushangaa!

Memory imefutika, hakuna kumbukumbu iliyobakia kichwani! memory ya miaka mitatu iliyopita imekwenda!

Hii inasababishwa na nini?

waganga na wauguzi, hii ndio matokeo ya ile 'kaputi-nzima' mnayoiita 'milk of amnesia'?
 
mchongoma, swali hapo juu sina utaalam wa kulijibu hata kidogo. nadhani ni swali gumu na lenye kuhitaji a complex knowledge jinsi ubongo unavyofanya kazi.

ninavyojua this is still an ongoing research, hata huko maulaya bado hawajajua kifasaha jinsi ubongo unavyo store memory. kila kilichopo pahala pengi ni speculations. kuna wanaodai ubongo unarecord matukio kama picha, yaani jumla jumla..(kama zip files hivi au pdf) na wengine wanasema unarecord bits moja moja (kama vile kwenye digital signal ambapo bits za data zinakuwa scrambled then combined at the end - multiplexing).... utanisamehe mifano yangu hii ya kujitungia maana ni ya ICT. But i hope umenipata.

SteveD.
 
...naaam, darasa kubwa linalohitaji tafakari pana na hekima bila kuchanganya imani na sayansi, achilia mbali fikra za mambo ya giza...

store ya memory na roho bado ni kitendawili...

...ila kina mama wengi wanaojifungua kwa njia ya caesar (kisu) wanadai wanapoteza kumbukumbu fulani kufuatia matumizi ya nusukaputi wakati wa Operation.

nashangaa kama hakuna Anaethesiologist, pharmacist, au hata Chemist anayepitia kusoma JF? kama yupo aje atuhabarishe habari hii...
 
Back
Top Bottom