Ubongo wa mwanamke hufanya kazi kwa haraka zaidi kuliko ubongo wa mwanaume

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,906
6,693
Ubongo wa mwanamke ni mdogo kwa 8% kuliko ubongo wa mwanaume.

Lakini unamuungano wa mawasiliano mzuri na wenye haraka zaidi kuliko wa mwanaume na ndio maana mwanamke anaweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja bila kukosea (multitasking).

Mfano:
kwa wakati huo huo mwanamke anaweza kupika
anaangalia TV
Anasuka na yote hayo hufanya kwa ufanisi.

Lakini kwa mwanaume ata deal na kimoja kwanza anahamia kingine, kutokana na ubongo wake ni mkubwa kuliko wa mwanamke.

Na ubongo wa mwanamke hutafsiri kwa haraka taarifa kutoka kwenye neva za milango ya fahamu mara 10 zaidi ya ubongo wa mwanaume.

Ndio maana mwanamke huwa na maamuzi ya haraka zaidi kwa sababu ubongo wake hutafsiri kwa haraka zaidi.

Ila katika 100% ya maamuzi ya mwanamke 45% ndio huwa sahihi na 55% huwa sio sahihi hii ni kutokana na uharaka wa ubongo kutafsiri information from nervous.

Mfano: mwanamke katika mahusiano ya mapenzi au mahusiano yoyote mwanamke ndiye huwa wa kwanza kushawishika kwa haraka zaidi na kuvunja mahusiano,

Hii ni kwa sababu ubongo wake ni mdogo hutafsiri kwa haraka zaidi na hupoteza kumbukumbu kwa haraka kuliko ubongo wa mwanaume.

Ubongo wa mwanaume hupokea taarifa na kuitafsiri kwa speed ya nusu ya mwanamke mara 5.
Mwanaume hufikiria kwa kina zaidi na kuchukua maamuzi ya kufanya kitendo,
hii ni kwa sababu ubongo wa mwanaume uko slow kutafsiri, kutokana na ukubwa wake

Ukubwa na udogo wa ubongo ndio hufanya mzunguko wa taarifa kwa muda kutokana na ukubwa na udogo.

Kwa hali hiyo ndio maana maamuzi ya mwanamke ni maamuzi ya haraka zaidi kuliko mwanaume.

Ndio maana mwanamke anaweza kukugundua wewe mwanaume kama unachati na mchepuko (hawara) au sio mchepuko.

Kama unavyoona hapo kwenye picha , mwanamke amehisi kuwa mume wake anachati na mchepuko tayari kwa haraka sana amepanda juu ya firiji kuhakikisha..
Hii ni kwasababu ubongo wake ni mdogo umepokea taarifa na kutafsiri kwa haraka na kufanya maamuzi ya kwenda kuhakikisha.

Tuishi nao tukiwa tunafahamu hivyo, hata vitabu vya dini vinasema tuishi nao kwa akili, sio kwamba hawana akili la hasha! bali ndio nilivyoelezea hapo juu kisayansi.


FB_IMG_1623551048704.jpg
 
Dah..ni ukweli mtupu lakini mbona kwenye tendo la ndoa mambo ni tofauti? Ubongo mkubwa wa mwanaume wenye spindi ndogo ya kupokea taarifa na kutafsiri ndo huwa unawahi zaid kumfanya amalize round kabla ya mwanamke
 
Aisee bora nipite nahisi nitawakosea...hahahaha yani juuya wepesi wote huo wa kutafsir taarifa lakini maamuz asilimia kubwa c sahihi
 
Mwanamke unaweza kumtoa mbali, ukamuwezesha mengi, akasahau yote kwa dakika moja akaenda zake , kumbe masikini wanasahau upesi !!...
 
Kumbe ndo maana wanamuamini kila mtu kwa haraka kupitia maneno tu mwisho wa siku wema wao unawaponza wanatapeliwa na muda mwingine kunyanyaswa, hata watu vikoba wanaanzaga na wanawake mwsho wa siku ukirud nyumban unakuta sebule nyeupe ishabebwa kisa rejesho
 
Mimi kuna kipindi nilihis mume wangu ana uzezeta...unampelekea shida anaweza itatua kwa wiki nzima...! Dah ngumu sana kuishi na mtu mzito aisee.

Hahaha sasa naanza amini...tulizaliwa twins me na ke...sasa tukivurunda huko tukiitwa mm nishajitetea zamani na kuanza kulia kbs kuondoa amani pale .mwenzangu anaishia kupigwa😆😆!

Mimi yaliwahi nikuta siku 1 tu maishani ..nikajifanya nna akili kumbe nhiiii🤣! Mpk leo ile incidence huwa nataman niifix ila ndo ishatoka hiyo!

Kazi iendelee!
 
1623571884271.png


Hapo anawasomesha watu wawili kwa wakati mmoja na kila mmoja anapata somo lake tofauti na mwenzake
 
Mbona mimi niko tofauti hasa hapo kwenye kuchukua maamuzi nachukua muda mrefu sana kuamua jambo!
 
Back
Top Bottom