Ubomoaji waliojenga kwenye vyanzo vya maji usibague

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Kwa ufupi
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy aliyetaka kujua kwanini baadhi ya watu waliojenga ndani ya mita 60 kutoka Ziwa Tanganyika wameachwa tofauti na matakwa ya sheria.

By Julius Mnganga, Mwananchi

Dodoma. Wataalamu wa mazingira wameagizwa kutofanya ubaguzi wanapobomoa nyumba za waliojenga karibu na vyanzo vya maji.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alipokuwa anajibu swali la Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy aliyetaka kujua kwanini baadhi ya watu waliojenga ndani ya mita 60 kutoka Ziwa Tanganyika wameachwa tofauti na matakwa ya sheria.

"Wataalamu wetu wanapaswa kuacha (ubaguzi) double standards wanapotekeleza suala hili. Utekelezaji wa sheria lazima uwe sawa kwa watu wote," amesema Jaffo.

Ametahadharisha kwamba ziwa hilo lipo hatarini kutoweka kwani lilivyo sasa ni tofauti na miaka 20 iliyopita. "Wananchi wanapaswa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji," amesisitiza.
 
Mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji zinawahusu watu kama akina Mbowe na viongozi wengine wa upinzani ambao wanapinga madudu ya serikali.
 
Mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji zinawahusu watu kama akina Mbowe na viongozi wengine wa upinzani ambao wanapinga madudu ya serikali.

Tunajua hilo.Na si kweli kwamba wamejenga kwenye vyanzo vya Maji ni ubaguzi na Visasi. Aliye nacho anacho tu,kumnyang'anya hamuwezi.
 
Kwa wale walalahoi hawana pakwenda wange fikiriwa pia angalau kupewa mud wajiandae kutafuta makazi mapya
 
Back
Top Bottom