Ubomoaji ulikuwa ni lazima ila mbomoaji kabomoa na anaendelea kubomoa kwa 'pupa'

Mbuyimayi

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
575
1,147
Naomba nitoe salamu zangu kwa wote wana jamvi

Na nikiri kutoka moyoni leo ndo siku yangu ya kwanza ku 'post' mada hapa japokuwa ni 'muhenga' kwa kupitia na kuchangia hapa na pale ktk 'nyuzi' za wana jamii wengine

Tukirudi katika mada na kama kichwa cha habari kinavyojieleza, huyu mbomoaji alikuwa anapaswa na ingekuwa ni ajabu sana kama asingebomoa ili kujenga upya kwa misingi inayokubalika katika dunia ya kisasa

Tatizo moja tu alibomoa na anaendelea kubomoa kwa 'pupa' na mbaya anaweza kujikuta na dalili zinaonyesha ujengaji wake unaweza kuwa na mapungufu maana hajui wapi pa kuanzia na nini cha kuchukua katika ujenzi huu mpya na mbaya pia muda nao wa kukamilisha ujenzi sio 'rafiki' sana kwake na kwetu tunaotaka hiyo dunia mpya

Wasalam
 
  • Thanks
Reactions: PNC
na kuna panya walikuwa wanatafutwa kwa udi na uvumba,wamepatikana lakini wamewaponza wasiohusika....
 
na kuna panya walikuwa wanatafutwa kwa udi na uvumba,wamepatikana lakini wamewaponza wasiohusika....

Huu ubomoaji haujali hata taratibu na kanuni za kubomoa na ujenzi kwa ujumla ,matofali na misumari inatupwa ovyo tu bila kujali hata wapita njia tu wanaweza umizwa na hawahusiki kwa namna yoyote na 'rabsha' za kubomoa
 
Back
Top Bottom