Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,896
- 6,912
UBOMOAJI NYUMBA ZA MAKAZI DAR SERIKALI INAKIUKA HAKI ZA MSINGI KIBINADAMU?
Ujenzi maeneo ya mijini kisheria kibali cha ujenzi lazima kitolewe. Kwa utaratibu huo halmashauri ya jiji ambayo ina dhamana itakuwa imejiridhisha kwamba ujenzi huo haujakiuka sheria za makazi jijini wala kuingilia maeneo nyeti ya umma.
Pamoja na haki hizo za halmashauri za miji, watu binafsi au makampuni binafsi wanaporuhusiwa kujenga maeneo hatarishi kama mafuriko, mitetemo ya ardhi au maafa mengine ya hali ya hewa huainishwa kwa hoja kwamba they are doing on their own risk.
Ndio maana nyumba yo yote maafa yatokanayo na hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi au vita na machafuko hakuna kinga ya dhamani kwa bima.
Mafuriko ni matokeo ya msimu na tena si kila mwaka, na ni ya muda mfupi. Yatapita na watu wataendelea na maisha yao. Mbona nyumba zilizo kwenye miinuko huezuliwa mapaa tokana na mvua za kusulisuli? Nako watahamishwa?
Miaka minenne iliyopita nilishuhudia mafuriko miji mingi sana Marekani, tujuavyo bara la Ulaya na Marekani wanamapokeo ya kujenga miji kandokando ya mito mikubwa. Mfano jiji la Nashvelle, TN, liko kando ya Cumbaland River. Karibu jiji lote lilifunikwa na mafuriko. Cha kushangaza maeneo yaliyokuwa lake-pond mabondeni kabisa yamejengwa majengo mengi na real estate ya ghorofa tano mpaka sita kupangisha tenants baada ya mafuriko kutokea, jiji limeruhusu on their own risk.
1) Je, kinachoendelea bomoabomoa dar kwa wenye makazi serikali imefikiria fidia?
2) La sivyo si kuwarudisha watu kuwa homeless? 3) Kipi bora watu kuwa homeless au kuwa na makazi wakivumilia homa za mafuriko ya muda mfupi?
4) Serikali ilikuwa wapi hadi watu wanajenga na kuishi miaka yote hii?
5) Je, nikiibebesha serikali lawama kwa kinachoendelea ni makosa?