msani
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 1,801
- 1,191
Kila unaposoma post za watu kilio chetu kinafanana.......ajira.....ajira....ajira....
Lakini wana jf mi nadhani tumekuwa wabinafsi sana na hatutaki kushirikiana,ni ukweli kwamba hatuna mitaji lakini kuna kazi zingine hazihitaji mitaji kwani kile ulichonacho kichwani ambacho umesomea miaka 3 au hata zaidi ni mtaji tosha iwapo mkikubali kushirikiana na wenzako,...watu hawataki kujiunga pamoja na kuanzisha ofisi yao ambapo kwao mtaji ni akili zao ambazo ni hitaji kubwa kwa jamii na badala yake tunalilia kuajiriwa tu ili tuendelee kuwa maskini na kuwanufaisha wengine kwa msoto ambao tumeusotea wkt tunasoma.
Kuanzisha kampuni yako kweli kuna msoto lakini mshindo wa mafanikio yake hapo baadae ni mkubwa.tunadanganywa kuwa kuna benki ya vijana inaanzishwa ambapo tunaweza kuanzisha biashara zetu lakini hao vijana wanaoongelea huenda usiwe wewe kwani huenda ukawa haupo ktk chama fulani cha siasa kwa hiyo msoto wako utakuwa palepale.mi nawaasa vijana wenzangu tujaribu kujiunga na wenzetu wa fani tofauti tofauti ili tuanze kuuza utalaamu wetu kwa jamii na tusisubiri mambo mepesi mepesi tu.
Najua vijana wengi mtachukia kwa ujumbe huu lakini ndio ukweli kwa mafanikio yako.
Mi nimemaliza chuo mwaka huu lakini tangu awali tulipanga na marafiki zangu kadhaa wa karibu wa fani tofauti ili tuanzishe kampuni yetu kwa kuwa huduma zetu hazihitaji mtaji mkubwa bali ni samani za ndani na kulipia ofisi,lakini tulipo maliza wengi waliogopa na kudai kuwa kozi zao zinauzika mjini kwa hiyo bora wakafanye kazi za kuajiriwa na tukabaki wawili lakini mchakato wetu unaendelea vizuri.
Naombeni tusiwe na mawazo ya kutafuta mamilioni ili tuanzishe ofisi zetu ambazo kwa hizo tutakuwa tumejiajiri!!!!!!
Msidhani mi ni mtoto wa fisadi kwa kutoa mawazo hayo.....maana ninachokifanya hata mzazi wangu hajui na sijarudi kijijini kwetu ingawa nasisitizwa nirudi kijijini ila ni kubaki hapahapa mjini kubanana mpaka kieleweke
inawezekanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa wana jf maana ajira imekuwa kilio kwetu,tujiunge ili nasi tutoe ajira kwa hao wenye mawazo bado ya kuajiriwa,waendelee kusubiri