Ubinafsishjai na hali ya Mtanzania

Salum Sanane

Member
Apr 14, 2013
30
4
Nimekuwa najiuliza bila kupata majibu yaliyo sahihi,ndiyo maana leo naileta hoja yangu hii ili nisaidiwe.
Suala la ubinafsishaji nimekuwa nalilinganisha na unyanyasaji mkubwa kwa watanzania hasa wa hali ya chini. Si vibaya nikisema kuwa ni juhudi za makusudi zilizoandaliwa kwa lengo la kumjengea maisha yasiyo na matumaini.
Mashirika mengi ya umma kabla hayajabinafsishwa yalikuwa yametoa ajira ya kutosha,na mara baada ya kubinafsishwa yalikufa au kupoteza muelekeo na hivyo kuwalazimu watumishi kuhangaika kutafuta mbinu mbadala za kuwawezesha kujikimu. Hali hii ni tatizo kubwa kwa mtanzania wa kawaida.
Mbali na mashirika ya umma, wavumbuzi wa migodi ya madini ni wananchi wenyewe. Kutokana na hali yao mbaya ya maisha wanajitahidi kutafuta ufumbuzi na hatimae kubahatisha kuangukia maeneo yanayopatikana madini. Badala ya kuwaboreshea ili nao wanufaike na ajira yao,serikali ikibaini tu kuwa madini yanapatikana inabinafsisha na kuwaacha wakiendelea kutaabika.
Maswali yangu ni haya:
1. Serikali inamjali mwananchi wake?
2. Mwananchi afanye kazi gani itakayoishawishi serikali kuuthamini utu wake?
3. Kuna sababu yoyote ya msingi ya kuendeleza dhulma hii?
Naomba ndugu zangu wenye uelewa mkubwa mnisaidie majibu ya maswali haya. Lakini pia hoja yangu ni hii: HAKUNA MSINGI WOWOTE WA SERIKALI KUDHIBITI NJIA ZOTE ZA MAPATO NA KUMWACHA MWANANCHI AKITAABIKA.
 
Kaka, haya ndio mambo ambayo Mtanzania anatakiwa kujiuliza wakati wa kuchagua viongozi wa kisiasa na hasa wale wa uwakilishi katika mamlaka za utungaji na upangaji sera za kitaifa. Kwa maoni yangu Benjamin Mkapa alikurupuka na kutuburuza kwenye sera za ubinafsishaji wa vyanzo vikuu vya uchumi. Kwa ubovu wa washauri wake, alikubali kuingia katika mikataba iliyo waacha Watanzania wengi bila ajira na kutuletea wageni ambao wakanufaika na ajira ambazo Watanzania walistahili na marupuprupu ya ajabu wakituacha tunahangaika kutafuta namna ya kuwasitiri vijana wetu. Hadi leo sioni Mwanasiasa, Mchumi, wala Msomi ambaye anaonyesha dira ya kuleta matumaini katika hili. Ndio maana watu kama kina Lowasa anaishia kuhubiri makanisani kwamba ukosefu wa ajira kwa vijana ni bomu linalosubiri kulipuka
 
Uko sawa,umenisaidia juu ya ukweli wa siasa za nchi hii. Nilichojifunza kutoka kwako ni ubovu,ubinafsi na uroho wa wanasiasa wa nchi hii.
Nakumbuka rerikali ya awamu ya pili ililiona hili ndipo wachimbaji wadogo waliporuhusiwa kuendelea na juhudi zan. Istoshe badala ya usumbufu wa kuuya kwa kujificha kama ilivyokuwa enzi zile za mwalimu,soko la madini liliwekwa wazi humuhumu nchini. Mzunguuko wa pesa uliongezeka na serikali ilinufaika na mauzo ya madini.
Katika awamu hiyohiyo mkulima aliangaliwa angalau kwa kiwango kidogo,hata kufikia watu wengi kuhamia vijijini kwa hiari.(akumbukwe mzee wa ruksa).
Badala ya kupongeza neema hizo tukaanza kumbeza,kumtukana na hata kumkejeli. Na kubwa zaidi kusema nchi imeuzwa.
Ukweli usiopingika umeshaonekana wazi na kujulikana ni nani ameuza nchi hii. Tujujie ujahili wetu wa kubeza mazuri na kusifu maovu.
 
Niko wazi sana na sikatawaliwa na nidhamu ya woga,usinifikirie chochote kuhusu woga.
Awali ya yote nimekuunga mkono kwa kubainisha wazi kuwa Benjamin Mkapa alitaingiza katika ubinafsishaji kwa kukurupuka. Labda niende kinyume na wewe kidogo niseme aliangalia maslahi yake binafsi.
Aliwabana sana wananchi na kuwaachia sehemu ndogo tu ya pesa kwa kisingizio cha kukusanya pesa hazina na kukuza uchumi.
Wakati anadai kukuza uchumi shilingi ya Tanzania ikiendelea kuporomoka,kilimo kinapoteza disa na hali za wananchi kuzidi kushuka.
Lakini kitu ninachokishangaa zaidi ni kuona serikali ya awamu ya nne inarithi na kuendeleza yaleyale ya awamu ya tatu. Sijui iliona ubora gani mpaka ikatamani kurithi.
Kwa kuwa mimi na wewe tunakubaliana juu ya hoja hii naomba utoe suluhisho.
 
Back
Top Bottom