Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
- Thread starter
- #21
Umetoa ushauri mzuri sana.Ni bahati mbaya sana tunatumia muda mwingi kujadili mapungufu na kauli za mkulu huku tukitumia muda kidogo sana kuwashauri wapinzani ni nini cha kufanya kujabiliana na hii hali iliyopo sasa.Bila kujali wewe ni Zitto kweli au Zitto photocopy kwani sioni kama ni verified user acha tu nikupe ushauri wangu. Kwa sasa hakuna demokrasia na wananchi wote tunaona. Ila mimi nimeshauri, ninashauri na nitaendelea kushauri kwa sasa ni vyema mkipata nafasi ndogo hiyo hiyo inayopatikana jaribuni kujikita kwenye siasa za maendeleo wangalau kwa 65% na asilimia iliyobaki 35% ndio iwe siasa za madaraka.
Kwanini nasema hivyo? Rais wa sasa sio muumini wa demokrasia na sehemu kubwa taasisi hazifuati sheria bali anachotaka rais. Ndio maana unaona siasa sasa hivi mnafanya anavyotaka rais na sio sheria inavyotaka. Kuna mambo mengi ya kunadi mnapokuwa majukwaani. Mfano kuhakikisha kila familia ya mkulima inakuwa na wangalau heka 2 za kilimo cha kisasa. Kushusha bei za vifaa vya ujenzi ili kila mtu ajenge nyumba bora. Upande wa afya ahidini mtakapopata madaraka mtajenga kila kijiji/kata zahanati. Elimu ni mpaka chuo kikuu bure, kurejesha mahusiano mema kati ya serekali na wafanya biashara. Ajira kwa wingi
Kwenye siasa za madaraka ahidini kufufua mchakato wa katiba mpya tena ya rasimu ya Warioba. Kurejesha demokrasia kama ilivyokuwa kabla ya awamu hii ya tano kuingia madarakani. Hakikisheni mnaweka watu kwenye vipindi vya televisioni na redio wenye kuweza kuhubiri maendeleo na siasa za madaraka. Sasa hivi mnaonekana kuhubiri siasa za madaraka zaidi kwani ccm sasa hivi inawafanya kujihami zaidi kuliko kushambulia huku ccm chini ya Magufuli ikiwa na madhaifu kibao. Maisha ni magumu kumebaki vitisho na uchumi unazidi kudorora.
NB: siku hizi wewe huonekani kwenye mijadala ya TV, sijui shida ni nini. Jipangeni japo tunajua ni ngumu ila tumieni nafasi hiyo finyu kwani tayari udhaifu wa Magufuli kiuchumi na kidemokrasia sasa uko wazi zaidi. Huku kwenye mitandao njoo na hizo verified ID wekeni mambo na sisi tuko nyuma yenu.
Tunatumia muda mwingi kukosoa serikali badala ya kutumia muda mwingi kuwashauri wapinzani the way forward.
Pia na wapinzani kwa sasa wanapaswa kukutana na kuweka mikakati ya pamoja ya nama ya kukabiliana na hali hii.
Tusijikite tu katika kukosoa kauli na matendo ya mheshimiwa bali sasa tujikite zaidi katika kubuni mbinu zitakazotuwezesha kutumia mapungufu hayo kuiodhoofisha CCM.